Huu mjadala wa kususia bidhaa na huduma ni hatari kwa uchumi wa nchi

Ni njia ya amani iliyofanikiwa sana kote ulimwenguni dhidi ya watawala dhalimu.

Naona mwisho wa kiburi na jeuri ya CCM(pesa)
 
This time tumejifunza haitatokea tena kurudi nyuma,tunasusia bidhaa moja kwa moja,ccm wakose hela jeuri kisha!

Wanatumia nguvu,sisi tunatumia akili.
 
Kama Mbowe akili imestaafu muacheni huru, mnamuogopa nini sasa?

Mwenye akili anadhibitiwa kwa kufungwa ila wewe usie na akili wanakuacha huru maana hauna madhara yoyote.
 
Achana na walevi wa faru john hao, kwani twitter kunauzwa bidhaa? Waliwahi kuhamasisha eti wana- Chadema wasusie mtandao wa Vodacom lkn walipokuwa na kesi wakahukumiwa kulipa faini wakatoa namba za simu za Vodacom kukusanyia michango, huo si ni uendawazimu..!!
 
Ni njia ya amani iliyofanikiwa sana kote ulimwenguni dhidi ya watawala dhalimu.

Naona mwisho wa kiburi na jeuri ya CCM(pesa)
Susieni hospitalini, ukikuta doctor ni mwana CCM ahirisha kutibiwa urudi nyumbani na kama itawezekana msiende hata huko hospitalini maana mtachangamana na Wana CCM.
 

Hao watu wa vijijini wenyewe wanafuata lolote linaloamuliwa mjini. Kama mngekuwa mnawathamini hao watu wa vijijini viongozi nao wangeishi huko vijijini.
 
Sio CHADEMA ni wananchi wote. Kwa sasa kipigo ni kwa UVCCM na Bavicha. Sote tuko jiko moja. Msoto kwa kwenda mbele.
 
Susieni hospitalini, ukikuta doctor ni mwana CCM ahirisha kutibiwa urudi nyumbani na kama itawezekana msiende hata huko hospitalini maana mtachangamana na Wana CCM.

Hospitali ambazo haziendekezi uccm ni za kumwaga boss. Hizi zenye ujinga wa uccm ndio hata panadol hawana.
 

Kama serikali inavyopambana na wananchi kwa kuweka tozo za kuwakomoa. Hii mbinu inaweza kuchukua muda kushika kasi, lakini ikitangazwa vyema lazima Italeta matokeo chanya.
 
Kina Lema walitushawishi tusitumie vodacom sie wajinga tukavunja lain hee kumbe wao hawakuvunjwa
 
Tatizo ukikataa kununua bia halafu serikali ikakuzidishia kodi ya PAYE utakuwa umeacha kunywa bia na umeanza kutwanga maji.

Hizo protests zinaweza kuwa na maana kama zinakuwa targeted against a specific company, or even industry.

Lakini ukiweka protest against the economy kwanza wewe mwenyewe utashindwa kuitimiza.

Kwa sababu yatatokea mambo ambayo hayaepukiki itabidi ukubali matokeo tu.
 
Kenya waliweza 100 percent...muulize Kenyatta...Hadi magari ya kampuni zake ya kusambaza bidhaa yaliharibiwa... Hand shake ilirudisha hali
 
Watu milioni 30 ni wapi?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…