Huu mjadala wa kususia bidhaa na huduma ni hatari kwa uchumi wa nchi

Huu mjadala wa kususia bidhaa na huduma ni hatari kwa uchumi wa nchi

Na wewe unaamini wametengeneza hasara?

Na hata kama wametengeneza hasara ni kwa ajili ya uzembe wao.

Mfano mimi mwaka jana sikuweka salio kabisa sababu ya ughali wa vifurishi vyao.
Sio ugali tu Mimi binafsi nimeshawishi kuanzia bibi babu mama na baba waache kutumia voda kwa sababu ni mtandao wa kinyonyaji na nilifanikiwa wote wanatumia airtel.
 
Naichukia CCM Sana, sitakuwa upande wao. Ila hili la kususia huduma au bidhaa ni wazo ambalo haliwezekani
Sijui kwa nini wamewaza hivyo, inapaswa kuwaza na kufanya Yale yanayowezekana
 
Hili halitafanikiwa Mkuu.

Labda niweke hili wazi! Chadema imeshapoteza mbinu/akili ya kupambana na CCM. MBOWE akili yake imesha staafu. Imma aombe watu wengine wamchoree mipango au atoke aruhusu akili nyengine iingie ifanye kazi. Kwa haya madrama mnayokwenda nayo yaani hamna kitu.
Mambo ni faya
Screenshot_20210802-214105.jpg
 
Sio ugali tu Mimi binafsi nimeshawishi kuanzia bibi babu mama na baba waache kutumia voda kwa sababu ni mtandao wa kinyonyaji na nilifanikiwa wote wanatumia airtel.
Hawatumii sababu ya ghalama zao na hata mimi nmekwambia mwaka jana wote sijaweka salio sababu ya ughali wa vifurushi vyao!

Lakini mtu hawezi kutumia kitu anachokipenda kisa eti ujinga wa siasa
 
Hili halitafanikiwa Mkuu.

Labda niweke hili wazi! Chadema imeshapoteza mbinu/akili ya kupambana na CCM. MBOWE akili yake imesha staafu. Imma aombe watu wengine wamchoree mipango au atoke aruhusu akili nyengine iingie ifanye kazi. Kwa haya madrama mnayokwenda nayo yaani hamna kitu.
Mbona ccm inatumia mabomu na polisi? yenyewe bado ina mbinu ya kupambana na CHADEMA?

Mtu aliyekosa mbinu anaweza kufunguliwa kesi ya ugaidi ?
 
Subiri uone mamilioni ya raia wakubali kujinyima kununua huduma na vitu fulanifulani ili kuinyima serikali kodi, hapo ndo utajua mbinu ya economic boycott inafanya kazi au la!
Hii ni ndoto! Na muotaji pekee ndiye anayedhani ni mazingira halisi.

Ila muda nao ni msema kweli. Unaweza ukawa umepatia nami nimekosea au kinyume chake.
 
Haina impact hapa bongo

labda wale wa online republic
Alipotekwa Dr Ulimboka tulihamasihwa kususia mtandao wa Vodacom kwa kuwa iliaminiwa watekaji wake waliwasiliana kwa kutumia mtandao ule. Hatukuona impact yake. Ben Saanane alivyotoweka tulihamasishwa pia kuisusia Vodacom kwa kuwa alitishwa kwa kupitia mtandao wa Vodacom, ajabu wanaotuhamasisha wao wenyewe wanaendelea kuwa wateja wa mtandao huo.

Hawa watu hawajifunzi?!
 
Hahahaha a good one Mkuu. 👍🏽 Kwa akili yake finyu mbinu za maccm za kubambikia kesi FEKI, kuuwa na kuzuia maandamano na kukataa katiba mpya na Tume huru ya uchaguzi ni AKILI KUBWA.
Mbona ccm inatumia mabomu na polisi? yenyewe bado ina mbinu ya kupambana na CHADEMA?

Mtu aliyekosa mbinu anaweza kufunguliwa kesi ya ugaidi ?
 
Alipotekwa Dr Ulimboka tulihamasihwa kususia mtandao wa Vodacom kwa kuwa iliaminiwa watekaji wake waliwasiliana kwa kutumia mtandao ule. Hatukuona impact yake. Ben Saanane alivyotoweka tulihamasishwa pia kuisusia Vodacom kwa kuwa alitishwa kwa kupitia mtandao wa Vodacom, ajabu wanaotuhamasisha wao wenyewe wanaendelea kuwa wateja wa mtandao huo.

Hawa watu hawajifunzi?!
Sasa hivi Chama cha CHADEMA kiko katika existential threat, kwa hiyo wanachama wake na wapenda demokrasia ndiyo watakaoshiriki kwenye boycott za kiuchumi zaidi kuliko nyie wana CCM. Nyie wana CCM na waunga mkono udhalimu mnaweza kuendelea na maisha yenu kama kawaida, lakini sisi wapenda demokrasia tutapunguza spending ili kuinyima serikali kodi mpaka pale serikali itakapokuja kwenye meza ya mazungumzo!
 
Mbona ccm inatumia mabomu na polisi? yenyewe bado ina mbinu ya kupambana na CHADEMA?

Mtu aliyekosa mbinu anaweza kufunguliwa kesi ya ugaidi ?
Mbowe na Chadema wanapambana na CCM si kwa kutumia nguvu ya raia bali kwa kutumia unafasi wa Chama chao.

Sijui umenielewa?
 
Back
Top Bottom