Nipo Space ya Maria Sarungi ambapo baadhi ya makada wa CHADEMA na Wanaharakati wanajenga hoja juu ya kususia bidhaa na huduma mbalimbali ili kuikosesha serikali mapato. Wanaanza na kutoa historia ya Boycotting ambapo kwa wakati fulani, watu wa Uingereza walikuwa hawapendezwi na biashara ya Utumwa. Ili kuukomesha, wakaacha kutumia Sukari ambayo ilikuwa ikitengenezwa na Watumwa. Na hivyo ikasabisha kiwanda kufungwa kwa sababu bidhaa hazitoki. Wanasema kuwa, jamii ya Watanzania wakipunguza matumizi ya bidhaa na huduma kama vile unywaji wa Bia, kupunguza matumizi ya sukari, maji ya kunywa, kupunguza miamala isiyo ya lazima na vyakula katika hoteli zilizosajiliwa. Wanaamini kuwa kupunguza huko matumizi ya huduma na bidhaa itasababisha serikali kukosa kiasi kikubwa cha mapato. Na kukosa huko mapato itasababisha serikali ishindwe kujiendesha kwa sababu mapato yamepungua. Na bila shaka, kutafuta namna ya kukaa na wadau na kuzungumza nao ili kuweza kutatua yaliyomo. Wanaamini kuwa, njia hii ya kususia bidhaa na huduma 'Boycotting' itakuwa na ufanisi kwa sababu hakuna polisi watakaokuja kuwalazimisha watu watumie. Wanaona kuwa njia hii ni ya amani na hivyo itawalazimisha serikali kurudi katika Misingi ya Utawala bora na kuleta uchocheo wa Katiba mpya. Je, CHADEMA watafanikiwa kwa njia hii?