Huu mjadala wa kususia bidhaa na huduma ni hatari kwa uchumi wa nchi

Kweli hawa ni watoto wa watawala wetu.
Hawana cha maana
Najiuliza huko zenji baba wa yule mbona hakumkosoa?
Mzee wa mifupa je
Wamepandwa kuleta machafuko walisoma kwa hela za wazazi wetu wa kijijini halafu wanatunyea
 

Siyo rahisi kihivyo. Kuna wana CHADEMA wengi wanahusika kwenye biashara zinazolengwa, zama zimebadikika.

Labda ilikuwa rahisi kwa waingereza na mataifa mengine enzi hizo kutokana na biashara kuhodhiwa na tabaka ndogo la wajanja hivyo wanufaikaji wa moja kwa moja wakawa wanatokea katika tabaka hilo.

Kwa leo, siyo rahisi kihivyo. Wapo wana CHADEMA wataigomea hilo wazo hadharani na wasio na vyama pia wengi watakataa.

Ngoja Watanzania wapigwe pini vyakutosha kwanza ndo mabadiliko yatakuja.

Kwa sasa hata angetekwa raisi mwenyewe, Watanzania wangeishia kulalamika bila vitendo. Nachojaribu kusema ni kwamba uwoga wa Mtanzania ndiyo pingu ya Mtanzania.

Watu waoga yaani mpaka unashindwa kuelewa hii nchi ilifanikiwa vipi kuwa na wananchi mazwazwa kama hawa.
 
Lazima tutanyooka na itatulazimu kuwaombeni CHADEMA tukawe mezani tuyamalize
 
Reactions: BAK
Ni sehemu ya mbinu za mapambano ya kutafuta HAKI.

Lakini mbinu hii ni lazima iwe imeelekezwa sehemu maalum kwa kuanzia, haiwezi kuwa blanketi la kufunika kila kitu kama inavyoonyeshwa hapa.

Kila aina ya mbinu ya kuleta ukombozi ni lazima ibuniwe, ijadiliwe na ipangwe kufuatana na umuhimu wake na mafanikio yanayoweza kupatikana katika eneo maalum.

Ni kama serikali (CCM) inavyotumia mbinu mbalimbali kuwakandamiza wapinzani, kuna Polisi, kuna Msajiri wa vyama vya siasa, anayetishia kila mara kuwafuta, kuna TBC, n.k..

Kwa hiyo CHADEMA nao ni lazima wabuni mbinu mbalimbali za kuendeleza mapambano.
 
Kwasabu chadema wapo wachache hawatofanikiwa ,labda wananchi kwa ujumla bila kujali vyama ndio hiyo kitu itawezekana kumbuka walisusia voda mpaka sasa inadunda
CDM wachache kwenu.uku kwetu wamejaa fwaa.hawajionyeshi tuu
 
Mahala pake wapi tena ikiwa kauli ya kujenga kama hii inadhatauliwa na hii Serikali dhalimu!?
Unafahamu kwamba ugomvi uliyopo baina ya Marekani na Urusi vilevile ni manufaa kwao?

Kwa sababu ni heri uwe na adui mwenye akili kuliko kuwa na adui mjinga. Hata mbinu za vita ni akili.

Ila ni hatari vilevile kupambana na mtu mjinga. Mimi naamini CCM na vyombo vya dola bado wanawaogopa sana raia.

Kova alisema hakuna uchaguzi uliyompa joto kama wa 2015. Jakaya alisema alidhani CCM inamfia. Chadema na Ukawa walikuwa na nguvu gani? Ni raia tu!

Usipambane na CCM nawe kwa kumuonyeshea msuli hali ya kuwa bado nguvu ndogo! Ni suala la kutumia akili tu kwa kuwekeza mahali ambapo patawaangusha kwa urahisi sana.

Chadema iwekeze kwenye watu kwa maana ni raia wananchi wenyewe kwa wingi. Wakifanya hivyo wanaweza wakampindua CCM.
 
Mkuu haya mapambano dhidi ya maovu mbali mbali nchini kwetu yanayofanywa na hii Serikali haramu ya maccm ni ya Watanzania wote bila kujali itikadi zao. Mfano ni hawa mashangazi Fatma na Maria hawa hawana vyama lakini wanapinga sana maovu ya kila aina na pia wanataka Katiba mpya na Tume huru ya uchaguzi vyote vipatikane kabla ya uchaguzi wa 2025.
Lazima tutanyooka na itatulazimu kuwaombeni CHADEMA tukawe mezani tuyamalize
 
Tunazungumzia kuhusu maovu ya kutisha ndani ya Tanzania yanayofanywa dhidi ya Watanzania na Serikali ambayo haikuchaguliwa na Watanzania. Hayo mambo ya Urusi na Marekani hayahusu kitu hapa. Kafungue uzi wako uyajadili huko.
 
Hili wameangalia kwa upande mmoja kuhusu Serikali kukosa mapato vipi kuhusu hao wafanyabiashara wanaosusiwa mitaji yao ikifa wanawasaidiaje?
 
Kweli hawa ni watoto wa watawala wetu.
Hawana cha maana
Najiuliza huko zenji baba wa yule mbona hakumkosoa?
Mzee wa mifupa je
Wamepandwa kuleta machafuko walisoma kwa hela za wazazi wetu wa kijijini halafu wanatunyea
wapo kaka zao wawili wako kimya kwa muda japo mmoja anawasuport huyu mwingine mwoga kidogo kuuza nchi ngoja tusubiri. hivi watu wanaelwa kweli kodo ipo kwa ajiri ya nani na kwanini? wao wakiumwa swala la matibabu sio issue wala shule halafu sisi tukwamishe serikali isikusanye kodi .
yetu yasiende wakati wao wanauwezo wa kununua bidhaa dubai na wakati mwingine kwa fedha za kodi walizoiba wazazi wao kwa hili watatusamehe.
wengi wetu purchasing power iko chini tunapambana kila siku jinsi ya kumudu maisha ya kawaida wao hapa tulishawavusha na kodi zetu na posho tulizokuwa tunawalipa wazazi wao .
watuambie hasa wanataka nini ilitujue toka mwanzo tunafanyaje na sisi tunapata nini vinginevyo hatuna stress za kijinga
 
Tunazungumzia kuhusu maovu ya kutisha ndani ya Tanzania yanayofanywa dhidi ya Watanzania na Serikali ambayo haikuchaguliwa na Watanzania. Hayo mambo ya Urusi na Marekani hayahusu kitu hapa. Kafungue uzi wako uyajadili huko.
Picha ni mfano halisi wa kitu. Tunatumia mifano ili kuijenga taswira ama picha ya jambo fulani mantiki nzima ipatikane ili ifahamika kwa undani haswa muktadha ni nini!

Unafikiri kwa nini Yesu alikuwa anazungumza kwa mifano?
 
Hivi voda ilivyo sasa ndivyo ilikuwa miaka 5 iliyopita? Unajua voda imetengeneza hasara ya billion 60 mwaka Jana

Unafikiri ni kwanini wametengeneza hasara wakati

Airtel, Tigo na halotel wametengeneza faida?
Mtandao wa voda una gharama kubwa watu wanakimbilia kwenye unafuu sio kwa sababu watu wamesusa
 
Narudia tena mifano yako ya Marekani na Urusi haihusu kitu. Jikite kwenye somo husika.
Picha ni mfano halisi wa kitu. Tunatumia mifano ili kuijenga taswira ama picha ya jambo fulani mantiki nzima ipatikane ili ifahamika kwa undani haswa muktadha ni nini!

Unafikiri kwa nini Yesu alikuwa anazungumza kwa mifano?
 
Kama mf katiba wanayoitaka wangekuja kwa wananchi sisi wa chini sio ile wanyotaka ili wawe watawala.
Tunewambia hatutaki mtoto wa mtawala awe mtawala, waende wafanye kwenye kad zingine sio uongozi.
Wafanye afya, jeshi lkn sio ubunge, u Dc , Rc ministers au ukuu wa nchi.
Wamekula hela zetu, nina uchungu nao sana.
Miaka ya nyuma walikata kwenda kusoma USA wakapeleka wao kwa mgongo wangu mtoto wa mkulima, baadae wakanitoa na kupeleka wao Japan 3 yrs wasidhani sikumbuki. Mafala sana
 
Huo mjadala unaendeshwa na CDM? Acha kutumia mattako kujenga hoja zako Mkuu.
 
Na wewe una waamini watu wa Twitter? Ni kujichangamsha na kuchangamsha genge. Hivi kuna waliowekeza kwenye kujua namna bora kabisa ya kuwavuta watanzania na wakawa serious na hoja zao? Hizi za copy and paste toka maeneo mengine zimegonga mwamba. Tunahitaji wanazuoni wa aina ya Nyerere kuweza kufanya hivyo
 
Mkuu, wewe unawasiwasi gani? Kama huo mpango hautafanikiwa si ndio furaha na ushindi kwako? Wewe tulia tu, acha wanaharakati wajipange namna ya kudhibiti serikali ya madhalimu.
 
Mkuu, wewe unawasiwasi gani? Kama huo mpango hautafanikiwa si ndio furaha na ushindi kwako? Wewe tulia tu, acha wanaharakati wajipange namna ya kudhibiti serikali ya madhalimu.
Mkuu utaniambia wakifanikiwa unikumbushe kwa hapo ni bet.
 
Huu mjadala ni mafanikio makubwa, MABUNGE YA CCM HAYAZIDI 500 lakini yamepitisha tozo za miamala na zinatumika na kutesa mamilioni ya Walalahoi hivi sasa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…