Huu mjadala wa kususia bidhaa na huduma ni hatari kwa uchumi wa nchi

Huu mjadala wa kususia bidhaa na huduma ni hatari kwa uchumi wa nchi

Voda unajua hali yake lakini kwa miaka 5 iliyopita.

Unajua mwaka Jana wametengeneza hasara ya 60 billions?

Kilichopi ni mpesa sio voda, voda ilishakufa kitambo sana .

Na mpesa wakicheza haya matozo inakufa nayo.

Line yangu ya voda ndiyo lkuwa main line ila kwa inapokea peke yake sipigi wala sitext chochote na muda si mrefu nikishaconfirm kwamba cycle yangu wote wanazifahamu namba zangu mbadala then nitaiabandon voda mazima.
 
Kuna mjadala unaendelea space pale twitter aisee kama haya maazimio ya kususia bidhaa na huduma yatafanikiwa hakika itakuwa hatari kwa uchumi.

Ushauri serikali wakutane na wapinzani haraka maana hata mishahara ya mapolisi inaweza kukosa huko mbeleni.

Ni ushauri tu mnaweza kuufanyia kazi au kuupuza ila kama hatua hizi zitafanikiwa hata kwa 25% makusanyo yataporomoka sana.
View attachment 1877729
Aibu
 
Ndio mtapata tabu Sana na hoja zenu za sijui gas,sukari mara luku ,miamala haya mambo hayawahusu Vijijini,, serikali ikiwaambia tumewwka tozo watu wa mjini walipe Ili tuwajengee barabara, zahanati na maji au shule ni makofi kwa kwenda mbele .

Nyie machadema hamjui hata kuchambua bajeti za serikali,hamjui hoja za kutoka nazo mnakomaa na Katiba,nani kijijini anataka Katiba?

Kijijini hata mijini wakiambiwa wanataka walete vita wamefadhiliwa na bwana zeenu Ulaya fasta mnapuuzwa na watu..Hii nchi ina wajinga wengi haijawa tayari kwa vyama vingi,hata wanaotumia mitandao ya kijamii ni watu wa mjini kijijini hawana huo mda.
Wa mjini ndo wana cashflow ya maana na ndo waelewa.
Hawa wana uwezo wa ndani ya siku kadha wa kadha watakazochagua kupunguza kutumia magari yao, kupunguza matumizi ya pombe, kupunguza matumizi ya data, ili kuinyima serikali kodi.
Nakuhakikishia kama watu milioni moja wakiamua kupunguza spending mara tatu tu ndani ya mwezi, makusanyo lazima yashuke
 
Msigwa alikuwa na kampeni ya kususia bidhaa za ASAS pale Iringa.

Hizi ni kama harakati za pimbi tu,hazijawahi kufanikiwa wala kuwa endelevu.
 
Msigwa alikuwa na kampeni ya kususia bidhaa za ASAS pale Iringa.

Hizi ni kama harakati za pimbi tu,hazijawahi kufanikiwa wala kuwa endelevu.
Haijawahi kuwa na uhitaji mkubwa wa kususia, lakini watu wakiwa pushed to the limit itafanikiwa tu, na itapiga penyewe palepale panapouma
 
Mimi nimeanza kitambo sana. Siendi kuangalia mpira viwanja vyote vya mpira wa Miguu vinavyomilikiwa na CCM, siangalii TBCCM, CH10 simpi lift polisi yoyote yule hata km nje kuna nyesha mvua ya mavi. Sisomi UHURU na Mzalendo sijui kwanza kama yapo.
 
Kuna mjadala unaendelea space pale twitter aisee kama haya maazimio ya kususia bidhaa na huduma yatafanikiwa hakika itakuwa hatari kwa uchumi.

Ushauri serikali wakutane na wapinzani haraka maana hata mishahara ya mapolisi inaweza kukosa huko mbeleni.

Ni ushauri tu mnaweza kuufanyia kazi au kuupuza ila kama hatua hizi zitafanikiwa hata kwa 25% makusanyo yataporomoka sana.
View attachment 1877729
Sisi tumesusia huduma za fedha za simu tu ,
 
Nipo Space ya Maria Sarungi ambapo baadhi ya makada wa CHADEMA na Wanaharakati wanajenga hoja juu ya kususia bidhaa na huduma mbalimbali ili kuikosesha serikali mapato.

Wanaanza na kutoa historia ya Boycotting ambapo kwa wakati fulani, watu wa Uingereza walikuwa hawapendezwi na biashara ya Utumwa. Ili kuukomesha, wakaacha kutumia Sukari ambayo ilikuwa ikitengenezwa na Watumwa. Na hivyo ikasabisha kiwanda kufungwa kwa sababu bidhaa hazitoki.

Wanasema kuwa, jamii ya Watanzania wakipunguza matumizi ya bidhaa na huduma kama vile unywaji wa Bia, kupunguza matumizi ya sukari, maji ya kunywa, kupunguza miamala isiyo ya lazima na vyakula katika hoteli zilizosajiliwa.

Wanaamini kuwa kupunguza huko matumizi ya huduma na bidhaa itasababisha serikali kukosa kiasi kikubwa cha mapato.

Na kukosa huko mapato itasababisha serikali ishindwe kujiendesha kwa sababu mapato yamepungua. Na bila shaka, kutafuta namna ya kukaa na wadau na kuzungumza nao ili kuweza kutatua yaliyomo.

Wanaamini kuwa, njia hii ya kususia bidhaa na huduma 'Boycotting' itakuwa na ufanisi kwa sababu hakuna polisi watakaokuja kuwalazimisha watu watumie.

Wanaona kuwa njia hii ni ya amani na hivyo itawalazimisha serikali kurudi katika Misingi ya Utawala bora na kuleta uchocheo wa Katiba mpya.

Je, CHADEMA watafanikiwa kwa njia hii?
Tusiwapuuze kwakua tunaona ni hoja kutoka chadema. Endapo taarifa hii ikawafikia wengi wasiopendezwa na yanayoendelea, amini nakuambia, tusipoziba ufa, tutajenga ukuta

Mambo yanaanzaga kwa utani kama hivi, lakini mwisho wake huwa makubwa na inakua ni too late.

Tatizo tuna viongozi wanaodhani kuupuza madai ya raia wake ndio utawala bora kwakua wamaamini wananchi inatakiwa wakubali kila wanachokiona wao ni sawa hata kama wanaumizwa. Ubaya ni kwamba hata zile njia rahisi za wananchi kuonyesha kutopendezwa na jambo zinazuiliwa. Kinachofuata ni hawa wananchi kujitafutia njia ambazo wataona zinafaa
 
Kwasabu chadema wapo wachache hawatofanikiwa ,labda wananchi kwa ujumla bila kujali vyama ndio hiyo kitu itawezekana kumbuka walisusia voda mpaka sasa inadunda
Mimi sio chadema na nimeanza kuzungumza na familia yangu. Maana sipendezwi na huu uhuni unaoendelea. Najua hutaamini ila mpaka kadi na vyeti vya ccm ninavyo na ni moja kati ya wanufaika na mfumo uliopo
 
Huu ni uzushi wako mwenyewe, acha kudanganya watu.

Chadema wanaweza kuwa na kasoro kadhaa lakini sio kukosa akili kiasi hiki kwamba wadhani wakisusia bidhaa itakuwa na impact kwenye uchumi kwa sababu hata CCM wakisusia hakuwezi kuwa na impact.

Kwa hiyo hii kitu umejitungia kichwani halafu unaileta hapa ukisingizia Chadema
Sio uzushi. Ni technique ambayo huwa inafanya kazi kama itakua na mwitikio mkubwa
 
Ni kuandamana bila kuumizana na polisi. Hakuna utoto maana unapunguza matumizi yasiyo ya lazima
Nadhani anayesema nhaya ni mtoto maana hata faida ya kusave hela haijui i ststed serikali haitaoata hela zangu kizembe.
 
Hayupo wa kufanya huo ujinga

Mpaka sasa mimi nimesitisha kutuma pesa kwa njia ya muamala ya simu. Na sinunui chochote kwenye duka la mwanaccm, huku ni kishawishi watu wengi kufanya hivyo. Nitanunua kitu kwa mwanaccm inaposhindikana. Pia unahakikisha kushawishi wapinzani hakuna kuhudhuria sherehe wala msiba wa mwanaccm. Jamaa yangu kafiwa na mama yake mwanaccm, nimemwambia natoa mchango tu ila msiba wa mwanaccm sihudhurii. Na kwenye kikao cha mazishi nikalisema hilo wazi. Nilifurahi maana niliwagawa watu kwenye msiba ule. Mjinga mmoja wa ccm anaitumia sms usiku kuwa hivyo sio vizuri kwakuwa sisi ni watanzania. Sijamjibu huo upuuzi.
 
Voda unajua hali yake lakini kwa miaka 5 iliyopita.

Unajua mwaka Jana wametengeneza hasara ya 60 billions?

Kilichopi ni mpesa sio voda, voda ilishakufa kitambo sana .

Na mpesa wakicheza haya matozo inakufa nayo.
Mpesa ndio inajifia maana watumiaji ni sisi ambao tumeshasusa. Situmii tena mpesa wala mfumo wowote wa kifedha wa mitandao ya simu kutokana na tozo. Sio mimi tu, ni wote
 
Hili halitafanikiwa Mkuu.

Labda niweke hili wazi! Chadema imeshapoteza mbinu/akili ya kupambana na CCM. MBOWE akili yake imesha staafu. Imma aombe watu wengine wamchoree mipango au atoke aruhusu akili nyengine iingie ifanye kazi. Kwa haya madrama mnayokwenda nayo yaani hamna kitu.
We ni mjinga sana inamaana huon serekali haitumii jukwaa huru kushinda na chadema alafu unawatuhumu wameshindwa kwa hoja, Tanzania ina wajinga wengi na watu wasiojielewa
 
MDHARAU MWIBA..... MATUMIZI YA NGUVU, KUIBA KURA, UTAWALA USIOFUATA SHERIA NI MASUALA YA KUDAI UHURU WA BINADAMU. ITATEGEMEA CHADEMA ITASHAWISHI ASILIMIA GANI NA BIDHAA ZIPI NA ATHARI GANI ZITAHUSIKA.
 
Back
Top Bottom