Huu Msafara wa Rais Magufuli sijawahi uona

Sijajua hoja yako ni nini hasa; lakini nami kama mwanajamii naomba nijadili hili swala la msafara wa rais( Presidential Motorcade).
Ila kwa ufahamu na uelewa embu tuangalie maeneo mengine wanafanyaje kabla ya kujadili msafara wa rais John Pombe Magufuli

1. Marekani ( United States of America)
Msafara wa raisi wa Marekani unahusisha magari arobaini (40) mpaka magaro hamsini (50). Ukiacha rais msafara wake pia unaweza kuhusisha mke wake, waandishi wa habari(member of the press), Wafanyakazi wa Ikulu (White house officials), watu wa usalama(security) na wageni ama maafisa wengine wa serikali katika wizara mbalimbali kutegemeana na ziara inahusu nini. Wahusika wakuu wa msafara ( Rais, familia yake, wafanyakazi wa ikulu na walinzi) hutumia magari ya kiusalama na yenye silaha ( armoured and configured limousines). Msafara uhusisha magari ya kiulinzi na kuisalama kama ,
USSS Electronic Countermeasures Suburban,timu ya kujibuy mashambulizi ( counter assault team)
na timu ya watu wa usalam,a ( Secret service agents)
Lakini pia uhusisha kikosi cha polisi kwa ajili ya kusafisha njia.
Msafara wa Rais wa Marekani umegawanyika katika sehemu mbili; sehemu ya kwanza inahusisha magari mawili hii huitwa ''secure package'' kunapotokea dharura, hii hutenganishwa kutoka kwenye msafara. Inahusisha limosine mbili zinazolindwa kwa umakini wa hali ya juu.
Sehemu ya pili uhusisha magari yanayosafirisha maafisa wa ikulu ya marekani (white house staff members) na waandishi wa habari.
Nyuma ya msafara huwa kuna gari inayojulikama kama WHCA Road runner ambayo kazi yake ya msingi ni kuwezesha mawasiliano kwa njia ya satellite, ikiwezesha mawasiliano ya sauti (bi-directional voice), nyuma ya gari hii huwa kuna ambulance na gari kadhaa za polisi.
Njia ambayo msafara wa rais unapita huwa inachaguliwa na watu wa usalama wakishirikiana na polisi. Njia za dharura(escape route) huwa zinachaguliwa hata kabla ya ziara ili kujiweka tayari kama kutatokea dharura.

2. Korea Kusini ( South Korea)
Msafara wa raisi wa Korea unahusisha magari kati ya ishirini 20 paka magari thelathini(30). Msafara huwa unabeba Rais, mke wa rais, mawaziri, walinzi, waandishi wa habari, maafisa wa ikulu(blue house officials), wageni, na hata marafiki.
Msafara huwa na magari ya kiulinzi na usalama (configured limousine na armored Cadillac Escalade)
Msafara pia uhusisha kikosi cha kujibu mashambulizi( counter assault team), kikosi cha usalama cha rais, timu ya madaktari, escort ya polisi

Sasa nirudi kwenye bandiko lako; nimegundua kwamba unahisi gari hamsini ni nyingi sana kwenye msafara wa Rais.
Kujua kama ni nyingi ama ni chache inakupasa kujiuliza maswali ya msingi kabla ya kufanya maamuzi

1. Je rais anaenda wapi? (Kama rais anatoka kwenye makazi yake kwenda ikulu idadi ya magari haiwezi kuwa sawa kama anatoka Dar kwenda Tanga)
2. Anakwenda kwa shughuli gani ( kuna nyakati msafara unahusisha wizara zaidi ya tano kutegemeana na shughuli ambazo mheshimiwa anaenda kufanya - rejea ziara yake nyanda za juu kusini)
3. Namba ya magari inaamuliwa na nini ( Kwa nini kuwe na magari kumi au hamsini kwenye msafara)

Kwa kifupi tu kwa kuwa nina mambo mengine ya kufanya nieleze hivi.

Ulinzi wa Rais inaweza kuwa jambo la kwanza kwa umuhimu kuliko mambo mengine yote.
Acha nikubaliane na wewe kwamba msafara ulikuwa na magari 53; je magari haya yapo kwenye msafara kwa shughuli gani?
Unadhani yapo kwa sababu za majigambo na ufahari? Hapana.
Sijajua hoja yako ni nini hasa; lakini nami kama mwanajamii naomba nijadili hili swala la msafara wa rais( Presidential Motorcade).
Ila kwa ufahamu mpana na uelewa embu tuangalie maeneo mengine wanafanyaje kabla ya kujadili msafara wa rais John Pombe Magufuli

1. Marekani ( United States of America)

Msafara wa raisi wa Marekani unahusisha magari arobaini (40) mpaka magari hamsini (50). Ukiacha rais msafara wake pia unaweza kuhusisha mke wake, waandishi wa habari(member of the press), Wafanyakazi wa Ikulu (White house officials), watu wa usalama(security) na wageni ama maafisa wengine wa serikali katika wizara mbalimbali kutegemeana na ziara inahusu nini. Wahusika wakuu wa msafara ( Rais, familia yake, wafanyakazi wa ikulu na walinzi) hutumia magari ya kiusalama na yenye silaha ( armoured and configured limousines). Msafara uhusisha magari ya kiulinzi na kuisalama kama ,
USSS Electronic Countermeasures Suburban,timu ya kujibuy mashambulizi ( counter assault team) na timu ya watu wa usalam,a ( Secret service agents)
Lakini pia uhusisha kikosi cha polisi kwa ajili ya kusafisha njia.

Msafara wa Rais wa Marekani umegawanyika katika sehemu mbili; sehemu ya kwanza inahusisha magari mawili hii huitwa ''secure package'' kunapotokea dharura, hii hutenganishwa kutoka kwenye msafara. Inahusisha limosine mbili zinazolindwa kwa umakini wa hali ya juu.

Sehemu ya pili uhusisha magari yanayosafirisha maafisa wa ikulu ya marekani (white house staff members) na waandishi wa habari.

Nyuma ya msafara huwa kuna gari inayojulikama kama WHCA Road runner ambayo kazi yake ya msingi ni kuwezesha mawasiliano kwa njia ya satellite, ikiwezesha mawasiliano ya sauti (bi-directional voice), nyuma ya gari hii huwa kuna ambulance na gari kadhaa za polisi.

Njia ambayo msafara wa rais unapita huwa inachaguliwa na watu wa usalama wakishirikiana na polisi. Njia za dharura(escape route) huwa zinachaguliwa hata kabla ya ziara ili kujiweka tayari kama kutatokea dharura.

2. Korea Kusini ( South Korea)

Msafara wa raisi wa Korea unahusisha magari kati ya ishirini 20 paka magari thelathini(30). Msafara huwa unabeba Rais, mke wa rais, mawaziri, walinzi, waandishi wa habari, maafisa wa ikulu(blue house officials), wageni, na hata marafiki.
Msafara huwa na magari ya kiulinzi na usalama (configured limousine na armored Cadillac Escalade)
Msafara pia uhusisha kikosi cha kujibu mashambulizi( counter assault team), kikosi cha usalama cha rais, timu ya madaktari, escort ya polisi.

3. Nchi za Afrika
Ni ngumu kupata rekodi sahihi kwa nchi za kiafrika kwa sababu mbalimbali na kutokutabirika kwa misafara ya marais wetu.
Kuna siku Kibaki alitembea na msafara wa magari matano tu lakini mwezi mmoja baadaye akawa na msafara wa magari 40.
Malawi ni miongoni mwa nchi za Kiafrika zinazoweka rekodi ya misafara mirefu zaidi ya raisi lakini pia hili hufanyika mara chache na maelezo huwa hayatolewi kwa nini msafara ni mrefu au mfupi.

Sasa nirudi kwenye bandiko lako; nimegundua kwamba unahisi gari hamsini ni nyingi sana kwenye msafara wa Rais.
Kujua kama ni nyingi ama ni chache inakupasa kujiuliza maswali ya msingi kabla ya kufanya maamuzi
  • Je rais anaenda wapi?
  • Kama rais anatoka kwenye makazi yake kwenda ikulu idadi ya magari haiwezi kuwa sawa kama anatoka Dar kwenda Tanga.
  • Anakwenda kwa shughuli gani?
kuna nyakati msafara unahusisha wizara zaidi ya tano kutegemeana na shughuli ambazo mheshimiwa anaenda kufanya - rejea ziara yake nyanda za juu kusini kwenye ziara za namna hiyo msafara utakuwa mrefu zaidi

Idadi ya magari inaamuliwa na nini?
  • Kwa nini kuwe na magari kumi au hamsini kwenye msafara wa Rais?

Kwa kuwa mimi na wewe hatuna ''access'' kwa kikosi cha Ulinzi wa rais, ni ngumu kufikia hitimisho hapa kwamba hayo magari 53 uliyohesabu yote ni sehemu ya msafara wa Rais ama kuna mengine yameingia kwenye msafara kwa sababu ya kimajukumu ya Wizara, Idara ama taasisi fulani kwenye safari ya Mheshimiwa Rais.

Ahsante kwa majibu bora kabisa.
Nitashangaa sana kama huna kazi hapa mjini.
 
kuna ka ukweli hapo
mfano wa leo pale Ubungo Wizara kibao zilikuwepo mpaka Mfugale na wengine huenda walianzia Ikulu kwa hiyo ilibidi wapande magari ya meusi, wakina Msigwa na Mama wa Rais, km nileo pale Ubungo magari hayakuzidi 15

Uzi umefika page ya 10 jamaa wanajadili mambo ambayo hayana uhakika wowote.
 
Nikiri tu huwa sisomi sana kwenye haya mambo ila kwa jinsi ulivyoandika na mpangilio ilinibidi nimalize bandiko.

Umeandika vyema sana. Hongera kwako, hii ndio Jamii FORUMS.......
 
Mkuu ata na mimi nimekuelewa wewe ulicho andika ila sasa mantiki hamna kabisa..
 
Leo Msafara wa Rais wa wanyonge anayejali kodi za wananchi sijapata uona tangu nizaliwe na Nchi nilizowahi tembelea.

Nimehesabu Magari yamefika 53.
Zote ni V8.

Noma sana.
Umesahau chopper inapita juu.
 
Raisi ni Raisi tuu , huwez kuwa Sawa na raisi , ni halali yake sababu za kiusalama
Usalama gani nchi ya amani na yeye anapendwa sn baada ya kufanya makubwa nchini?
Kinachosemwa hakiineshwi kwa vitendo......
 
Fahari ndie mama wa ujinga.. Nimeukumbuka wimbo wa kimanyema wa GERE MAMA

Jr[emoji769]
Kuna mambo mengi sio fahari ni usalama wa mtu.
Roho ya mtu ina thamani kuiko magari 500 aina ya Toyatoa V8.

Kuna watu kutokana na kazi na misismamo yao wanakuwa hatarini sana wakati wowote.
 
Sema vitu kama hivi tulizoea kuviona kwa wakina Yahya Jammeh,Msafara wa Kenyyata marekani haukuwa na magari Mengi.
Marais wote duniani ni kawaida sana hili,
Ni kawaida kwa rais kuwa na wanausalama,viongz wanaomsindikiza kwenda pengine kwenye tukio husika.

Marekani rais wao alipokuja mbona hamkwongea na walishuka hadi na ma gar yao?

Ukiachana tu na USA,
Yapo mataifa tu hapa Africa ambayo pia ni kawaida sana kwa vitu kama hivi...

So tusishangae sana.

Hata wewe ukiambiwa leo uwe rais lazima ufate Kitu kinaitwa PROTOCOL

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuna mambo mengi sio fahari ni usalama wa mtu.
Roho ya mtu ina thamani kuiko magari 500 aina ya Toyatoa V8.

Kuna watu kutokana na kazi na misismamo yao wanakuwa hatarini sana wakati wowote.
Kwa hiyo roho za akina Ben saa 8 nk hazikuwa na thamani kwake
 
Back
Top Bottom