Katika hali ya kuonesha wanannchi wameshamchoka rais wa wanyonge, leo asubuhi wamesikika wakilalamika vikali kwenye daladala baada ya kulazmika kusubiri muda mrefu barabarani kupisha msafara wa rais aliyekuwa akitoka Dar kuelekea Dodoma. Kilichowaudhi sana wanachi waliokuwa wakiwahi kwenye shughuli zao za kila siku sio kulazimika kupisha msafara wa rais kwa sababu hili ni jambo la kawaida; bali ni kitendo cha rais Magufuli kusimama mara kwa mara kila kituo, mfano amesimama ubungo, akasimama Mbezi, Kibaha Mlandizi, n.k hali iliyofanya magari kusubiri kwa muda mrefu wkati yeye akizungumza na wanachi.
Mwananchi mmoja alisikika akisema, "rais wetu ni mbinafsi sana, haoni magari yansubiri zaidi ya saa nzima kumsubiri yeye apite? kwa nini asipite atuache sisi wengine nasi tuwahi kazini?" Mwingine alilalamika, "kwani rais atoke muda huu ambao ni peak hours?kwa nini asitoke walao wakati ambao harakati za barabarani ni chache?" Au kwa nini asitumie helikopta au ndege ili kuonesha kweli kutujali wananchi tunaowahi makazini? Anasimama kila mahali barabarani bial ulazima, kwa nini hawajali kwamba kuna sisi wengine tunawahi hospitalini!
Haya ni malalmiko ya kweli ya wanchi leo asubuhi tulipokwama kwenye foleni kuupisha msafara wa mheshimiwa rais, kipenzi cha wanyonge JPM. Mjumbe hauwawi!