Huu ndio muonekano wa behewa la Royal katika treni ya mchongoko ya SGR

Hakika mie nimeduwaa yaani hata behewa za sgr yetu ya kawaida ziko vizuri kuliko hili mchongoko, au kuna watu walichonga mchongo wao kupitia mchongoko huu?
 
hapa utasikia mama anautandika mpaka wananchi wanaloa 😥😥😥😥
 
Hakika mie nimeduwaa yaani hata behewa za sgr yetu ya kawaida ziko vizuri kuliko hili mchongoko, au kuna watu walichonga mchongo wao kupitia mchongoko huu?
🤣😂😂 oyaa yaaani kila unavyojiuliza unaishia kukosa majibu kuna namna viogozi wanatukosea sana
Wanahisi kwenye hii nchi watu wote ni wajinga kumbe sivyo ilivo
 
Bongo wamechomelea vigoda ndiyo wameviweka royal class??
 
Hapo kwenye nauli wanazingua sana, nauli ya daraja lolote kwenye hiyo treni haikutakiwa kuzidi 60,000.
Bongo upunguani hautakuja uishe. Enzi hizo unatafuta chumba cha kukaa, unaambiwa chumba kipo, bei yake ni 35,000 ila ukitaka master (chumba na choo cha peke yako) ni 70,000 hadi 100,000 (Gharama ya cho ni sawa au zaidi ya chumba)

Tafsiri ni kwamba maisha ya bongo ni kama shule au jela tu kiasi kwamba kuwa na choo cha peke yako inachukuliwa kuwa ni anasa.
 
Hao ni viongozi ni mpaka tarehe 3, treni imeondoka na abira wasiozid 300 inamaana hajafikisha hata nusu treni huku zile royal na business za ya kawaida yetu zikiwa ndo Huwa zinawahi kujaa kabla ya daraja la tatu.
Siti za daraja zinavutiq hata kwa macho kuliko hizo royal za mchongoko.
Behewa Moja la mchongoko mnakaaa mpaka watu 90 huku kwenye loco letu hat 50 na Bado viti vyake vimekaaa kiclassic.
Siwez lipia pua tu ya treni mara mbili ya nauli ya kawaida
 
Nawaza tu hapo kwa sisi vibonge na kitambi changu nimekaa hapo kwenye seat halafu mbele yangu akae abiria wa kike mdada mrembo tumeangaliana hivyo safari nzima mie mwepesi wa kusinzia safarini na nikisinzia huwa nakoroma natoa mpaka udenda sambamba na kujamba mara moja moja
Sasa huyo anayekaa mbele yangu hapo si atafanya niogope kusinzia ili kuepuka aibu?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…