Huu ndio muonekano wa David Banda (Mtoto wa Mwanamuziki Madona)

Huu ndio muonekano wa David Banda (Mtoto wa Mwanamuziki Madona)

Screenshot_20220531-093505.png
 
YESU KRISTO na arudi tu mapema aje aibadilishe hii dunia maana maovu na uchafu vimezidi mno.
Na atakapokuja atawanyoosha kweli kweli maana imeandikwa; "naye atawatawala kwa fimbo ya chuma".
Angoje kidogo aisee,wengine ndio tupo tunapaua tupate hata pa kujisitiri,sasa akija shughuli za ujenzi sio ndio zimeishia hapo[emoji3]
 
Hebu Waswahili acheni kuhitimisha msiyoyajua.

Kwanza una uthibitisho gani kama huyo Jamaa kawa Shoga?, au kwa kuwa kavaa hivyo?..huyo huenda ni ulimbukeni tu wa "Masikini akipata...".

Na hata kama amekuwa hivyo unamuingizaje Madona na kutaka kuiondoa nia yake njema ya tangu awali?...kwamba angetaka kuwa Msomi, Msanii au Mwanamichezo bora angemzuia?

Madona sio Mzungu wa kwanza wala wa mwisho kufanya hisani ya aina hiyo, wapo wengi wala hawatangazi na sio Watu Marufu kama Madona.

Ile St Jude ya Arusha inapokea Watoto wasio na uwezo wa kugharamia Masomo ambayo Wenzenu wenye uwezo na nyadhfa wanawasomesha Watoto wao Shule kama zile...sasa utoke huko wewe uanze kubeza Watu wanaosimamia ile Shule kwamba wana nia ovu?.

Sisi Watu Masikini hatujiamini kabisa, tunahisi tunaonewa tu kila wakati.
Unatetea usilolijua! Kumbuka mapadiri wamekuwa wakifanya nini mpaka papa wa sasa kaingilia kati!
 
Back
Top Bottom