Huu ndo Ushahidi wa Nchi za Magharibi zinavyotusaidia. Anayewatukana na kuwasimanga muonee huruma sana!

Mbona mambo kibao yanaenda kwa ushirikiano wa China na mambo yanasonga??
Kwanini wamagharibi wasifanye kama China we do business with mutual benefit??
Shida yako akili kisoda.
Una akili mgando.
China anawasaidia nini kwenye maisha yenu ya kila siku hapa?

Kuwaletea bidhaa feki na kukisupport chama cha Mapinduzi?
 
Swali fikirishi je tukijiwekea malengo na kuacha kulea ufisadi hatuwezi kuzipata hizo pesa?
 
kama MUNGU akiamua, huenda nikawa Rais Jamhuri ya Muungano wa Tanzania(JMT)2045.nawaomba kabisa wana_JF kwa upendo kabisa kama mtakua HAI basi mnichague.mko tayari?na hii ni 21st century, na imebaki 21 year$?
 
kama MUNGU akiamua, huenda nikawa Rais Jamhuri ya Muungano wa Tanzania(JMT)2045.nawaomba kabisa wana_JF kwa upendo kabisa kama mtakua HAI basi mnichague.
Kwa tume ipi, inayo teuliwa na Rais, sina kumbukumbu za kutosha kuhusu fungu la uwendeshaji wake kama wako huru nalo
 
Ndio inaweza ila kuna sheria yoyote Canada ama Nchi yoyote ya Kidemokrasia kuitisha nchi ama mtu yoyote adrop kesi sababu ya Misaada?
 
Nani ameongelea nini kuhusu kumfukuza mtu?
 
China anawasaidia nini kwenye maisha yenu ya kila siku hapa?

Kuwaletea bidhaa feki na kukisupport chama cha Mapinduzi?
Reli ya Tazara amekujengea China.
Smart fone amekuletea China.
Madaraja amekujengea China.
Miundombinu barabara amekujengea China.
Soko lako la parachichi kubwa moja wapo ni China.

Wakati huo USA hakukufanyia lolote wewe.
Anakutega kwa misaada ya vyandarua.
Hata huijui dunia ikoje China ndio amekuletea globalisation.

China ni business man masuala ya wewe na chama chako shughulika nacho mwenyewe.
 
Ndio inaweza ila kuna sheria yoyote Canada ama Nchi yoyote ya Kidemokrasia kuitisha nchi ama mtu yoyote adrop kesi sababu ya Misaada?
Hiyo haihitaji kuwa sheria, na wala si kitisho.

Kwa sababu Tanzania haina haki ya kupewa msaada na Canada.

Canada inaweza kuamua kuacha kuisaidia Tanzania kwa sababu yoyote, au bila sababu.

Laumu viongozi wako kwa kufanya Tanzania itegemee misaada ya Canada.

Usiilaumu Canada kwa kupanga inatoa vipi misaada yake.
 
Reli ya TAZARA alijenga ndiyo kama mkopo!

Hiyo mihndombinu hatujengea bure tena anatukopesha. Tena mbaya zaidi anatupiga maana anatujengea miondominu yenye viwango duni vya ubora tena kwa mikopo umiza yenye interest mbaya sana!

Hakuna msaada wa ujenzi anaoufanya mchina. Mchina yupo kibiashara tena kaa ajili ya kutuibia
 
Kukwepa kodi ni kosa la jinai, kuzuia mtu asipelekwe Mahakamani pia ni jinai ama hili ni jinai akifanya tu China na tutamwita Dikteta ila wakifanya mabwana zetu tunajitoa ufahamu na kukata mauno?

Reverse hii situation Mtanzania yupo Canada kakwepa kodi, then China Aingilie kati kama Canada wanamfunga huyo Mtanzania basi China ana stop viwanda vya Canada China, Dunia nzima ingeimba.
 
Ila huyu Mama kidiplomasia anaturudisha kwa jiwe.Alafu naona kakwepa mkutano wa UNGA kamtuma Majaliwa!🤣🤣🤣
 
Hiyo kodi yenyewe unayoisema ilikiwa ni kichekesho cha dunia nzima.

Ilikuwa sawa na habari ya "Amini Usiamini" katika gazeti la Mfanyakazi la miaka ya 1980.

Zaidi, narudia, serikali ya Canada ina haki ya kutoa na kusitisha misaada inavyotaka.

Laumu viongozi wako kwa kufanya taifa lako litegemee misaada ya Canda.

Usiilaumu serikali ya Canda kwa kuamua isaidie wapi na wapi isitishe misaada.
 
Sawa mkuu, tuna mitizamo tofauti kuhusu hili, labda sijui maana sahihi ya kusaidiwa. Mbona tunawasumbua na kuwapigia magoti kila kukicha hata kwa mambo ambayo kama tungekuwa serious tungayafanya wenyewe?. Kwa nini wanapata ujasiri wa kutukemea kwa mambo yetu ya ndani ya nchi na hawawezi kuthubutu kufanya hivyo kwa nchi zinazojitegemea.
Tatizo ni sisi au ni wao? kwamba bado tunahitaji kusaidiwa hata ujenzi wa vyoo mashuleni? bado tunahitaji kusaidiwa hata kupambana na Malaria na magonjwa mengine ya umaskini? Kwa nini hata huyo mchina aje tena kutusaidia reli ta TAZARA miaka takribani 50 baada ya kusaidia ujenzi wake. Kiongozi akisimama na kuwapiga mkwara hao watu anakuwa anaongea kwa dhati toka moyoni au anajifaragua tu. Ni lini wamewahi kuja kutuomba watusaidie hayo wanayotusaidia?
 
Alifanya kipi cha maana? Yote uliyoandika/ kuuliza ni mashudu tu
Wewe sema hujui sio kwamba ni mashudu.
Uliuliza kuna ushahidi gani kama wanaotuletea misaada wananufaika zaidi.Nikakuuliza hayo maswali kukupa jibu.
Mwishowe unakana tena!??

Hizi hatua za muda mfupi ndani ya miaka mitano nani alizifanya tukazipiga??
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…