GE2025 Huu ni uongo na ni tusi kwa Watanzania wote walio na akili timamu na wanaojielewa!

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

Nyani Ngabu

Platinum Member
Joined
May 15, 2006
Posts
98,439
Reaction score
145,410
Jana CCM wamezindua kampeni zao za uchaguzi mkuu ujao wa mwezi Oktoba.

Kama ilivyo ada, wametoa ahadi kadhaa.

Moja ya ahadi zilizo kamata usikivu wangu ni hii ya kuunda tume ya upatanishi [maridhiano] ili kuandaa mazingira ya kuandika katiba mpya.

Hawa watu ni waongo sana. Hawana kabisa nia ya hayo [upatanishi, maridhiano, na katiba mpya].

Mimi nakataa katakata wao kunifanya mimi mjinga, zuzu, na mpumbavu.

Nakataa kwa sababu hao watu [CCM] wapo madarakani kwa zaidi ya miaka 60 sasa na ifikapo 2030, watakuwa wamekaa madarakani kwa karibu miaka 70!

Wangekuwa na nia ya kweli ya kuyafanya hayo mambo, tayari wangekuwa washayafanya kitambo sana.

Katiba mpya ingekuwa ni muhimu kwao, basi ingeandikwa tokea mwaka 1992 tulipoingia katika mfumo wa vyama vingi.

Wao ndo walikuwa madarakani kipindi hicho lakini katiba mpya haikuandikwa.

Baada ya uchaguzi wa mwaka 2010, kelele za katiba mpya zilipozidi, hao hao CCM wakaanzisha mchakato feki wa kuandika katiba mpya.

Bunge la katiba mpya likaundwa. Rasimu ya katiba mpya ikaandikwa.

Kumbuka, haya yote yalianzishwa katika muhula wa pili wa Rais wa wakati huo.

Juhudi zote hizo pamoja na rasilimali zote zilizotumika kwenye huo mchakato, zikapotea bure.

Hakukuwa na cha katiba mpya wala shangazi yake na katiba mpya.

2015 tukapata Rais mpya na serikali mpya. Hoja ya katiba mpya ikatupiliwa mbali.

2021 tukampata huyu Rais aliyepo sasa.

Yeye akasema mambo ya katiba mpya yasubiri kwanza mpaka atengeneze uchumi.

Kichekesho. Ni kana kwamba hajui uhusiano wa katiba mpya iliyo bora na misingi ya kujenga uchumi ulio bora.

Jana wakati akitoa ahadi zake, akadokeza kuwa ataunda tume ya kushughulikia mambo ya katiba mpya!

Whoopdedoo 🤣.

Anatangaza mambo ya katiba mpya akiwa anaingia kwenye muhula wake wa pili.

Classic case of kicking the can down the road.

Kama historia muongozo, basi hakuna cha maana kitachotokea kuhusu kuandika katiba mpya.

2030 ikifika, watakuja na kisingizio kingine. 2035 huyo atayekuwa mgombea wao naye atatoa ahadi kama hiyo. Nayo itakuwa ni hewa tu.

Kama hamniamini, angalieni tu jina la sasa la tume ya uchaguzi.

Kelele zilipozidi, wakabadili tu kidogo jina la hiyo tume. Badala ya kuitwa tume ya taifa ya uchaguzi, wakaongeza neno moja tu, ‘huru’. Ikaanza kuitwa Tume Huru ya Uchaguzi. Kutoka NEC mpaka INEC.

Hawa watu hawana soni kabisa.

Haya, tuje kwenye maridhiano.

Madhila yote kuhusu siasa na wanasiasa, yametokea chini yao.

Wangekuwa ni watendaji haki, kusingekuwepo na haja ya upatanishi na maridhiano.

Miaka yote hiyo wameshindwa kuwatendea vyema watu wengine halafu leo hii kwenye kampeni zao wanasema wataunda tume ya usuluhishi na maridhiano.

Hivi, si yalikuwepo yale mazungumzo ya maridhiano muda si mrefu uliopita?

Kama wameshindwa kuwatendea vizuri Watanzania kwa zaidi ya miaka 60, ndo wataweza kwenye miaka 5 ijayo?

Waende zao huko. Mimi nilishakataa huo uwendawazimu.

Tuombe tu JF iendelee kuwepo kwa miaka mingi ijayo ili tukumbushane.
 
Wasukuma ni watu wapuuzi sana, yule ndugu yao marehemu alivyoulizwa kuhusu katiba aliyajibu hayahaya aliyojibu Samia lakini kwenye andiko la msukuma mwenzake wala hajatajwa..

Vipi bi mkubwa umemnunulia hata fanicha mpya?
 
Same ‘ol playbook.

That’s why I’m not falling for it.
Safari hii nina uhakika wataleta ''katiba mpya''. Lakini itakuwa mbaya kuliko iliyopo..... kila mtu aweke haya maneno. CCM sasa hivi iko kwenye hali mbaya sana na waliopo madarakani hawatakubali kuweka ushindani wa haki kwa sababu ni kujichimbia kaburi.... wakiondoka watashtakiwa kwa mengi. Hvyo watataka kung'ang'ania kwa muda mrefu kadiri iwezekanavyo... kwa kutumia kila silaha waliyonayo na katiba ni silaha muhimu sana sana....
 
Kwa sentence hii tu Peke yake…, “tume ya upatanishi [maridhiano] ili kuandaa mazingira ya kuandika katiba mpya…” iliyotolewa katika ile hotuba na Samia maana yake katiba mpya hakuna…

kuandaa mazingira gani tena wakati Warioba alisha hoji watu karibia wote nchini na kuja ba bango kitita na katiba pendekezwa…?

Ccm wanaichezea tu nchi na siku ikiripuka wao ndio watakuwa wa kwanza kutiwa viberiti… hilo hawalioni…

Siku huwa hazigandi… waendelee tu na talandira zao, siku zaja upepesi na ngonjera zitaisha…
 
💯%.
 
Jana CCM wamezindua kampeni zao za uchaguzi mkuu ujao wa mwezi Oktoba.

Kama ilivyo ada, wametoa ahadi kadhaa.

Moja ya ahadi zilizo kamata usikivu wangu ni hii ya kuunda tume ya upatanishi [maridhiano] ili kuandaa mazingira ya kuandika katiba mpya.

Hawa watu ni waongo sana. Hawana kabisa nia ya hayo [upatanishi, maridhiano, na katiba mpya].

Mimi nakataa katakata wao kunifanya mimi mjinga, zuzu, na mpumbavu.

Nakataa kwa sababu hao watu [CCM] wapo madarakani kwa zaidi ya miaka 60 sasa na ifikapo 2030, watakuwa wamekaa madarakani kwa karibu miaka 70!

Wangekuwa na nia ya kweli ya kuyafanya hayo mambo, tayari wangekuwa washayafanya kitambo sana.

Katiba mpya ingekuwa ni muhimu kwao, basi ingeandikwa tokea mwaka 1992 tulipoingia katika mfumo wa vyama vingi.

Wao ndo walikuwa madarakani kipindi hicho lakini katiba mpya haikuandikwa.

Baada ya uchaguzi wa mwaka 2010, kelele za katiba mpya zilipozidi, hao hao CCM wakaanzisha mchakato feki wa kuandika katiba mpya.

Bunge la katiba mpya likaundwa. Rasimu ya katiba mpya ikaandikwa.

Kumbuka, haya yote yalianzishwa katika muhula wa pili wa Rais wa wakati huo.

Juhudi zote hizo pamoja na rasilimali zote zilizotumika kwenye huo mchakato, zikapotea bure.

Hakukuwa na cha katiba mpya wala shangazi yake na katiba mpya.

2015 tukapata Rais mpya na serikali mpya. Hoja ya katiba mpya ikatupiliwa mbali.

2021 tukampata huyu Rais aliyepo sasa.

Yeye akasema mambo ya katiba mpya yasubiri kwanza mpaka atengeneze uchumi.

Kichekesho. Ni kana kwamba hajui uhusiano wa katiba mpya iliyo bora na misingi ya kujenga uchumi ulio bora.

Jana wakati akitoa ahadi zake, akadokeza kuwa ataunda tume ya kushughulikia mambo ya katiba mpya!

Whoopdedoo 🤣.

Anatangaza mambo ya katiba mpya akiwa anaingia kwenye muhula wake wa pili.

Classic case of kicking the can down the road.

Kama historia muongozo, basi hakuna cha maana kitachotokea kuhusu kuandika katiba mpya.

2030 ikifika, watakuja na kisingizio kingine. 2035 huyo atayekuwa mgombea wao naye atatoa ahadi kama hiyo. Nayo itakuwa ni hewa tu.

Kama hamniamini, angalieni tu jina la sasa la tume ya uchaguzi.

Kelele zilipozidi, wakabadili tu kidogo jina la hiyo tume. Badala ya kuitwa tume ya taifa ya uchaguzi, wakaongeza neno moja tu, ‘huru’. Ikaanza kuitwa Tume Huru ya Uchaguzi. Kutoka NEC mpaka INEC.

Hawa watu hawana soni kabisa.

Haya, tuje kwenye maridhiano.

Madhila yote kuhusu siasa na wanasiasa, yametokea chini yao.

Wangekuwa ni watendaji haki, kusingekuwepo na haja ya upatanishi na maridhiano.

Miaka yote hiyo wameshindwa kuwatendea vyema watu wengine halafu leo hii kwenye kampeni zao wanasema wataunda tume ya usuluhishi na maridhiano.

Hivi, si yalikuwepo yale mazungumzo ya maridhiano muda si mrefu uliopita?

Kama wameshindwa kuwatendea vizuri Watanzania kwa zaidi ya miaka 60, ndo wataweza kwenye miaka 5 ijayo?

Waende zao huko. Mimi nilishakataa huo uwendawazimu.

Tuombe tu JF iendelee kuwepo kwa miaka mingi ijayo ili tukumbushane.
Hakuna mwanCCM anaeipenda TZ
 
Umeandika kila mstari ni hoja. Kuhusu Tume huru, baada ya kubadili jina la NEC kuwa INEC kukatungwa sheria mpya za uchaguzi zikapitishwa na Bunge. Guess what! sheria hizo hazitumiki uchaguzi huu! hawa ndio wanataka tuandike katiba. Kinachoendelea si kudanganya ni kuchanganyikiwa maana UMMA umegoma na wanajua hilo.

Hivi uchumi ushatengemaa kiasi cha sisi kuandika katiba! waliosema uchumi hawajatuambia lakini leo wana ahadi ya Katiba, ahadi waliyoikataa kwasababu za uchumi!!

Niliposikia hoja ya Katiba nikajua hawa watu wameshikwa pabaya , wana way waya, uongo umefika kikomo.

Sikubali kuwa zuzu hata dakika moja! hawana nia njema wala si wa kuwasikiliza! ni kuwapuuza tu
 
Back
Top Bottom