Jana CCM wamezindua kampeni zao za uchaguzi mkuu ujao wa mwezi Oktoba.
Kama ilivyo ada, wametoa ahadi kadhaa.
Moja ya ahadi zilizo kamata usikivu wangu ni hii ya kuunda tume ya upatanishi [maridhiano] ili kuandaa mazingira ya kuandika katiba mpya.
Hawa watu ni waongo sana. Hawana kabisa nia ya hayo [upatanishi, maridhiano, na katiba mpya].
Mimi nakataa katakata wao kunifanya mimi mjinga, zuzu, na mpumbavu.
Nakataa kwa sababu hao watu [CCM] wapo madarakani kwa zaidi ya miaka 60 sasa na ifikapo 2030, watakuwa wamekaa madarakani kwa karibu miaka 70!
Wangekuwa na nia ya kweli ya kuyafanya hayo mambo, tayari wangekuwa washayafanya kitambo sana.
Katiba mpya ingekuwa ni muhimu kwao, basi ingeandikwa tokea mwaka 1992 tulipoingia katika mfumo wa vyama vingi.
Wao ndo walikuwa madarakani kipindi hicho lakini katiba mpya haikuandikwa.
Baada ya uchaguzi wa mwaka 2010, kelele za katiba mpya zilipozidi, hao hao CCM wakaanzisha mchakato feki wa kuandika katiba mpya.
Bunge la katiba mpya likaundwa. Rasimu ya katiba mpya ikaandikwa.
Kumbuka, haya yote yalianzishwa katika muhula wa pili wa Rais wa wakati huo.
Juhudi zote hizo pamoja na rasilimali zote zilizotumika kwenye huo mchakato, zikapotea bure.
Hakukuwa na cha katiba mpya wala shangazi yake na katiba mpya.
2015 tukapata Rais mpya na serikali mpya. Hoja ya katiba mpya ikatupiliwa mbali.
2021 tukampata huyu Rais aliyepo sasa.
Yeye akasema mambo ya katiba mpya yasubiri kwanza mpaka atengeneze uchumi.
Kichekesho. Ni kana kwamba hajui uhusiano wa katiba mpya iliyo bora na misingi ya kujenga uchumi ulio bora.
Jana wakati akitoa ahadi zake, akadokeza kuwa ataunda tume ya kushughulikia mambo ya katiba mpya!
Whoopdedoo 🤣.
Anatangaza mambo ya katiba mpya akiwa anaingia kwenye muhula wake wa pili.
Classic case of kicking the can down the road.
Kama historia muongozo, basi hakuna cha maana kitachotokea kuhusu kuandika katiba mpya.
2030 ikifika, watakuja na kisingizio kingine. 2035 huyo atayekuwa mgombea wao naye atatoa ahadi kama hiyo. Nayo itakuwa ni hewa tu.
Kama hamniamini, angalieni tu jina la sasa la tume ya uchaguzi.
Kelele zilipozidi, wakabadili tu kidogo jina la hiyo tume. Badala ya kuitwa tume ya taifa ya uchaguzi, wakaongeza neno moja tu, ‘huru’. Ikaanza kuitwa Tume Huru ya Uchaguzi. Kutoka NEC mpaka INEC.
Hawa watu hawana soni kabisa.
Haya, tuje kwenye maridhiano.
Madhila yote kuhusu siasa na wanasiasa, yametokea chini yao.
Wangekuwa ni watendaji haki, kusingekuwepo na haja ya upatanishi na maridhiano.
Miaka yote hiyo wameshindwa kuwatendea vyema watu wengine halafu leo hii kwenye kampeni zao wanasema wataunda tume ya usuluhishi na maridhiano.
Hivi, si yalikuwepo yale mazungumzo ya maridhiano muda si mrefu uliopita?
Kama wameshindwa kuwatendea vizuri Watanzania kwa zaidi ya miaka 60, ndo wataweza kwenye miaka 5 ijayo?
Waende zao huko. Mimi nilishakataa huo uwendawazimu.
Tuombe tu JF iendelee kuwepo kwa miaka mingi ijayo ili tukumbushane.