1. Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa Tundu Lissu alikamatwa na kutupwa mahabusu mpaka leo, Watanzania kimya.
2. CHADEMA kimefutiwa Ruzuku yake, Watanzania kimya.
3. Viongozi wa CHADEMA wamevuliwa uongozi wao, Watanzania kimya.
4. CHADEMA kimepigwa marufuku kufanya shughuli za kisiasa, Watanzania kimya.
5. CHADEMA wamezuiliwa kusafiri kwenda nje ya Nchi, Watanzania Kimya.
6. Nasikia Account za CHADEMA zimefungiwa, Watanzania kimya.
Mimi naamini Agenda ya CHADEMA ni Agenda ya Watanzania kwa sababu wanazungumzia mambo yanayowahusu Watanzania wote.
Najiuliza, sisi Watanzania ni MISUKULE au ni watu tunaotembea tu lakini ubongo ulishanyofolewa kitambo?