Huu ugonjwa gani? Nagusa kama kipele kigumu - kinachoteleza na kinachouma ndani ya uke

Huu ugonjwa gani? Nagusa kama kipele kigumu - kinachoteleza na kinachouma ndani ya uke

Habarini za wakati huu memberz wenzangu.

Nimekuja humu kuomba ushauri/ tiba ya ugonjwa unaonisumbua.

Ni takriban mwezi wa 6 huu nagusa mfano wa kipele/kinundu kirefu kinachouma ndani ya uke (nikilala chali nakishika kabisa).

Awali nilidhani huenda ni mchubuko tu nikajua nitapona hvo sikutilia maanani.

Ila kadri siku zinavyozidi kwenda nikaona hakuna dalili ya kupona.

Iko hivi:
Nikifululiza kujaamiana may be wiki, basi hiko kipele huanza kuuma kiasi cha kwamba uume ukiingia nahisi kama nachanika.

Ila nikiacha kujaamiana, huwa sisikii maumivu kabia. Nimekuwa mtumwa wa kutumia mafuta ya mgando wakati wa kujaamiana maana nikisema nisipake kitu naumia sana wakati wa tendo.

Kuna wakati nilipata UTI, nilivyomaliza dozi, nilipata afueni na hiko kipele. Nilikaa kama mwezi bila kuhisi maumivu wakati wa tendo. Ila mwezi ulivyokata tu nikiingiliwa ni maumivu.

Huwa nikilala chali na kuingiza kidole cha shahada ndani ya uke upande wa kulia nakishika, ni kama mfano wa kinyama kinachoteleza ila chenye ugumuugumu.

Sijajua ni nini.
huo muda wote dada yangu kwanini hujaenda kwa gyno? nenda hospitali haraka.
 
AmKATRINA unakaa miezi 6 na ugonjwa ambao huuelewi ukeni kweli..??
Namna kuna magonjwa mengi mno sikuhizi na yanatisha hasa, how can you be comfortable and neglect that..??
watu weusi hawako makini linapokuja suala la afya. ni maneno ya tafiti.
 
Ex wangu nae aliwahi kuwa na ugonjwa kama huo sema yeye kuna vinyama vilikuwa vinaota ukeni vinawasha sana hadi anapata homa akaenda hospital wakavitoa
 
Itakua ni uume unaota kidogo kidogo na wewe utaanza kuwakanda
 
Kwani nani hajui akiumwa anatakiwa kwenda hospitali? Yeye kaleta hapa toa jibu la kitaalamu kama uliishia la saba B kaa kimya.

Ukitoa jibu hapa la kiafya kwa hili swala ni kwamba hujui unacho kiongea. Mambo ya Afya sio ya kiki au uchawa wenu ni serious. Kumwambia aende hospitali kwa swala hili ndiyo ushauri vinginevyo ni utoto na ujinga jinga kama wenu. Inabidi tufungue chemba hapa ya watoto, machawa, na watu wa kiki mtuachie watu serious JF .
 
Ukitoa jibu hapa la kiafya kwa hili swala ni kwamba hujui unacho kiongea. Mambo ya Afya sio ya kiki au uchawa wenu ni serious. Kumwambia aende hospitali kwa swala hili ndiyo ushauri vinginevyo ni utoto na ujinga jinga kama wenu. Inabidi tufungue chemba hapa ya watoto, machawa, na watu wa kiki mtuachie watu serious JF .
Hongera mtu serious lakini mjinga wa mwisho.
 
Hongera mtu serious lakini mjinga wa mwisho.
Wee ARV huwenda mimi humu ndo peke yangu nimekuelewa..

Yani mkuu nimeona toka comment yako ya kwanza wee jamaa ni understanding sana aiseeeee
🙌🙌🙌🙌🙌🙌🙌🙌🙌🙌🙌🙌🙌🙌🙌🙌🙌🙌🙌🙌🙌🙌.....
Unajua mpaka mtu analeta hoja humu jua kuna mengine anahitajui zaidi na ndio mana likaitwa jukwaa la afya means watu wajadili sio kwamba hajui kuwa kuna hospital...

Lakini pia mtu anakuja humu kupata info eg
-Ushauri
-Je kama hospital aende hospital gani..
-Experience ya watu kuhusu huu ugonjwa...

Yapo mengi anayopata humu.. sasa mtu kuangalia na kumwambia kavu nenda hospital hiyo inakua ni repeated point..

So ARV nipo pamoja na wewe kabisa sijaiona wrong yako ipo wapi
🙏🙏🙏🙏🙏🙏🙏🙏🙏🙏🙏🙏🙏🙏👊👊👊👊👊👊😂
 
Mrejesho?
Uwii, kumbe sikuwaletea mrejesho.
Poleni.
Ni hivi, Dokta ameniambia kuwa nina kinyama ambacho kilikuwa kinaanza kuota ukeni, na vile nilivyokuwa nakishika ilikuwa nafanya makosa kwani naweza sababisha bacteria kuzaliana.
Hivo nilipewa dawa ya kuingiza huku kwa bibi kwa muda wa wiki 3, na baada ya maumivu kuisha walienda kukikata.
Ni kinyama kidogo ukubwa wa harage la mbeya (wakati wanakitoa nilipokitazama nikajua wameng'oa antena yangu🤭)
Na nilipouliza kwa nini kiliota wakasema huwa inatokea sana pale unapotumia haya madawa ya kubana uke (na nilikuwa nayatumia sana)
Kwani hujui kiafya yanatengenezwa na nini hivo kupelekea kupata muwasho kisha uvimbe mpaka kupelekea uvimbe kukomaa na kuwa kama kinyama.

Nashukuru nimeshapona na napiga show hata masaa 2 bila kuumia wala kuchubuka.
Na napata starehe sana jamani (kumbe uke ukiwa na afya ndio raha hv)

Hiyo ndio feedback wapendwa wangu.
 
Kwa hio wameondoa masega yote au wamesema kitaota tena kisije kikawa kisunzua ukikata kinaota kikubwa zaidi ya kile
Hapana, wametoa mpaka mzizi na ndio maana nilipewa dawa ya usingizi..
Wamesema uwezekano wa kuota haupo kwa maana wamechimbua mpaka mzizi.
Siku za mwanzo walipokitoa niliporudi nyumbani kukojoa ilikuwa kasheshe.
Kidonda + mkojo wenye chumvi.
Kwahiyo nikawa nikitaka kukojoa naingiza kitambaa huku chini ili hata mkojo ukija angalau maumivu yapungue.
 
Back
Top Bottom