- Source #1
- View Source #1
Wakuu
Naomba ufafanuzi hapa
Naomba ufafanuzi hapa
- Tunachokijua
- Wanu Ameir ni miongoni mwa watia nia wa uwakilishui kupitia CCM, Jimbo la Makunduchi, Zanzibar. Katika bunge lilipita Wanu alikuwa mbunge wa viti maalum.
Madai
Kumekuwa na ujumbe unaosambazwa katika mitandao mbalimbali inayooenakana kuwa umechapishwa na Rais Samia Suluhu Hassan akieleza kuwa anawataka wajumbe wa Makunduchi wampitishe binti yake ajulikanaye kwa jina la Wanu Hafidhi Ameir kwani anaweza.
Uhalisia wa madai hayo
JamiiCheck imefuatilia na kurishisha kuwa taarifa hiyo si ya kweli.
Ufuatiliaji umebaini kuwa ujumbe huo haujachapishwa na Rais Samia kama inavyoonekana. Ujumbe huo haupo katika ukurasa rasmi wa mtandao wa X (Twitter) wa Rais Samia na wala hajawahi kuchapisha ujumbe unaofanania na huo.
Ujumbe huo ni wa kughushi kwani una mpangilio tofauti, mathalani imetumia mwandiko (fonts) kubwa sana kuliko ilivyo kawaida. Pia screenshot hiyo inaonesha kuwa ina tiki ya blue wakati Rais Samia anatumia utambulisho wa tiki ya kijivu (grey).
Aidha ujumbe huo licha ya kuwa na mapungufu yaliyotajwa hapo juu lakini pia ina makosa ya kiuandishi ikiwemo kukosewa kwa jina la Wanu, ambalo limeandikwa Wahu.