SI KWELI PreGE2025 Huu ujumbe unaoonekana ni wa Rais Samia kwenda kwa mwanae Wanu

Baada ya kuitathmini taarifa hii, tumebaini kuwa si ya kweli.
Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)
Source #1
View Source #1
Wakuu

Naomba ufafanuzi hapa

 
Tunachokijua
Wanu Ameir ni miongoni mwa watia nia wa uwakilishui kupitia CCM, Jimbo la Makunduchi, Zanzibar. Katika bunge lilipita Wanu alikuwa mbunge wa viti maalum.

Madai

Kumekuwa na ujumbe unaosambazwa katika mitandao mbalimbali inayooenakana kuwa umechapishwa na Rais Samia Suluhu Hassan akieleza kuwa anawataka wajumbe wa Makunduchi wampitishe binti yake ajulikanaye kwa jina la Wanu Hafidhi Ameir kwani anaweza.

Uhalisia wa madai hayo

JamiiCheck imefuatilia na kurishisha kuwa taarifa hiyo si ya kweli.

Ufuatiliaji umebaini kuwa ujumbe huo haujachapishwa na Rais Samia kama inavyoonekana. Ujumbe huo haupo katika ukurasa rasmi wa mtandao wa X (Twitter) wa Rais Samia na wala hajawahi kuchapisha ujumbe unaofanania na huo.

Ujumbe huo ni wa kughushi kwani una mpangilio tofauti, mathalani imetumia mwandiko (fonts) kubwa sana kuliko ilivyo kawaida. Pia screenshot hiyo inaonesha kuwa ina tiki ya blue wakati Rais Samia anatumia utambulisho wa tiki ya kijivu (grey).

Aidha ujumbe huo licha ya kuwa na mapungufu yaliyotajwa hapo juu lakini pia ina makosa ya kiuandishi ikiwemo kukosewa kwa jina la Wanu, ambalo limeandikwa Wahu.
Ndio. Ni yeye anamgawia manyama mwanaye. Wanajikatia minofu tu.
Huo ujumbe hajaandika yeye km yeye ameandika huyo Mwanae na jina lake kalikosea kuandia baada ya kuandika Wanu yeye kajiandika Wahu baada ya kua na kimuhemuhe cha kutaka kwenda bungeni, ila mimi sina baya nae km wanampenda na anawaletea maendeleo basi wampe tu nafasi maana sio kwa ubaya sio sababu Mama yake ni Rais na Mwenyekiti wa Chama ila sababu yeye anaweza kuwaletea maendeleo hao anaoenda kuwawakilisha bungeni na kuzitatua changamoto zao zinazowakabiri
 
AI hiyo mkuu,japo kwenye hili la mwanae kuutaka ubunge alijakaa vyema,kihekima ilibidi amkemee
 
Wewe na familia yenu lini mtakuwa wabunge?
 
Tuna safari NDEFU kama nchi aisee. Huyo mwanae mbona STORI ni ya muda mrefu kwani fulani amekanusha?



Kwishaaaaa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…