Huu uongo kuwa nyongo ya mamba ni sumu ulianzishwa na nani?

Huu uongo kuwa nyongo ya mamba ni sumu ulianzishwa na nani?

Na ww umethibitishaje kuwa sio sumu maana utafiti hupingwa kwa utafiti, sio kukurupuka tu.
Kuna utafiti ulisema ni sumu, au umekariri tu huo msemo wa tafiti kupingwa kwa tafiti?
 
Sawa kabisa wala hujakosea je ukiila binadamu inakufanyaje kwa concentration yake?

Kwa mfano sumu ya kwenye meno ya nyoka ni kwaajili ya kuanzisha umeng'enywaji(digestion) ya chakula kutokea ndani ya mwili kwenda nje. Yaan kama sisi binadamu tunatafuna chakuka halafu tumboni kinameng'enywa kutoka ganda la juu kwenda ndani ila nyoka akimng'ata panya anakufa na anaanza kumengenywa toka ndani kuja nje. Ndio maana ni nyoka wachache sana wana uwezo wa kumuua binadamu(kutokana na ukubwa wake) ila ni rahisi sana kupoteza kiungo ulipong'atwa kama mguu au mkono kwakua ile sumu inafanya kazi ya kuanza kudigest uke mguu au mkono kwa ndani

Kwa mfano huo na kwa maelezo yako. Kile nyongo yako inachofanya kwenye chakula ndo hicho hicho nyongo ya mamba inakifanya kwenye mwili wa mtu aliyeila(kwakua ile nyongo inalingana=direct proportional=imeundwa kufanya hivyo kwa viumbe wenye miili/uzito unaolingana na kuzidi wakwetu)
Mkuu hii habari kuwa sumu ya nyoka kazi yake kumeng'enya uliitoa wapi? Sumu ya nyoka ni kwaajili ya kujilinda na kuua. Nyoka kama koboko ana sumu inaitwa neurotoxin hii inaathiri mishipa ya fahamu na kufanya upalalyze. Nyoka kama kifutu ana cytotoxin hizi zinaua cell. Hizi ndiyo zinaozesha mguu. Huwezi ng'atwa na nyoka mwenye neurotoxin halafu mguu ukaoza.
 
Siwezi kula kila kitu ili kujua kama ni sumu au siyo.
Hoja ipo kwenye nyongo ya mamba ni sumu, Inawezekana hakuna ukweli hata chembe kwenye hilo lakini je! Tukubali bila kuwa na evidence yyte? Pinga hoja kwa research sio kwa Empty Righting.
 
Hoja ipo kwenye nyongo ya mamba ni sumu, Inawezekana hakuna ukweli hata chembe kwenye hilo lakini je! Tukubali bila kuwa na evidence yyte? Pinga hoja kwa research sio kwa Empty Righting.
Hoja siyo iwapo sumu ya mamba ni sumu hoja ni huu uongo wa kuwa nyongo ya mamba ni sumu ulitoka wapi?
 
Sawa kabisa wala hujakosea je ukiila binadamu inakufanyaje kwa concentration yake?

Kwa mfano sumu ya kwenye meno ya nyoka ni kwaajili ya kuanzisha umeng'enywaji(digestion) ya chakula kutokea ndani ya mwili kwenda nje. Yaan kama sisi binadamu tunatafuna chakuka halafu tumboni kinameng'enywa kutoka ganda la juu kwenda ndani ila nyoka akimng'ata panya anakufa na anaanza kumengenywa toka ndani kuja nje. Ndio maana ni nyoka wachache sana wana uwezo wa kumuua binadamu(kutokana na ukubwa wake) ila ni rahisi sana kupoteza kiungo ulipong'atwa kama mguu au mkono kwakua ile sumu inafanya kazi ya kuanza kudigest uke mguu au mkono kwa ndani

Kwa mfano huo na kwa maelezo yako. Kile nyongo yako inachofanya kwenye chakula ndo hicho hicho nyongo ya mamba inakifanya kwenye mwili wa mtu aliyeila(kwakua ile nyongo inalingana=direct proportional=imeundwa kufanya hivyo kwa viumbe wenye miili/uzito unaolingana na kuzidi wakwetu)
Hapo umezungumzia nyoka wenye sumu je nyoka kama common egg eater, chatu na rat snake ambao hawana sumu umeng'enyaji kwao hua inakuaje?
 
Mkuu hii habari kuwa sumu ya nyoka kazi yake kumeng'enya uliitoa wapi? Sumu ya nyoka ni kwaajili ya kujilinda na kuua. Nyoka kama koboko ana sumu inaitwa neurotoxin hii inaathiri mishipa ya fahamu na kufanya upalalyze. Nyoka kama kifutu ana cytotoxin hizi zinaua cell. Hizi ndiyo zinaozesha mguu. Huwezi ng'atwa na nyoka mwenye neurotoxin halafu mguu ukaoza.
Aiseee eti sumu ya nyoka ni kwaajili ya kujilinda???

Sawa mkuu. Ila ukae ukijua sumu ya nyoka haijaumbwa kwaajili ya binadamu ndomaana nyoka hawindi binadamu na anakung'ata baada ya kuona ni tishio. Tena hao vifutu mpaka huwa wanatoa sauti ya kuonya kabla kwakua hana mpango na wewe ila kwa ile misosi yake anakua kimya anawinda

Vyovyote iwavyo naomba nikutakie mwaka mpya mwema
 
Nyongo ya mamba siyo sumu.

Mwaka 2015 watu 72 walifariki Msumbiji na ikadaiwa walichanganyiwa nyongo kwenye pombe.

Lakini siyo kweli. Kwanza chanzo kikaonekana siyo nyongo ya mamba. Na hata hivyo huko huko msumbiji huikausha na kuisaga nyongo ya mamba na kuisafirisha china ambako hutumika kama kiongeza nguvu za tendo.

Yep yaani badala ya kunywa supu ya pweza unaweza kuchukua nyongo ya mamba, ukaikausha, ukaisaga na kutumia unga wake kujiongezea nguvu za tendo.
 
Aiseee eti sumu ya nyoka ni kwaajili ya kujilinda???

Sawa mkuu. Ila ukae ukijua sumu ya nyoka haijaumbwa kwaajili ya binadamu ndomaana nyoka hawindi binadamu na anakung'ata baada ya kuona ni tishio. Tena hao vifutu mpaka huwa wanatoa sauti ya kuonya kabla kwakua hana mpango na wewe ila kwa ile misosi yake anakua kimya anawinda

Vyovyote iwavyo naomba nikutakie mwaka mpya mwema
Usiondoke bado tunaeleweshana tu hapa.

Sumu ya nyoka ina kazi nyingi wewe upo sahihi na mdau yupo sahihi.

Sasa swali langu la wasio na sumu digestion hufanywaje usilipite.
 
Usiwe mbishi,Nyongo ya mamba ni sumu kali sana,kuna maza mmoja wakigoma alimtwanga na hiyo sumu mme wake,alimuwekea kwenye chakula,aiseee,sasa hivi Mama ni mjane na wakulingwa wanajipigia tu..

Hivi ulishawahi ona mzoga wa kunguru ukiliwa na paka au panya?? Hata sisimizi tu hua hawagusi
Unajuaje kuwa alitumia nyongo ya mamba? Nyongo ya mamba haiui kitu, labda unywe debe zima, hata maji ukinywa debe zima unakufa.

Halafu ndiyo nyie mnasemaga kunguru hana damu!!
 
WIKI iliyopita tulizungunzumzia sifa za mamba na jinsi anavyoishi, makala ile hatukuweza kuimaliza kutokana na ufinyu wa nafasi. Wiki hii tunamalizi sifa za mamba na jinsi unavyoweza kumuepuka pindi unapokutana naye.

Juma lililopita tuliona sifa nane, leo tutaangalia kunzia sifa ya tisa hadi 22.

9. Wakati mwingine huigiza amekufa ili kuwakamata samaki wakubwa kwa urahisi, akiwa majini utaona anazunguka kama anapelekwa na maji, samaki wakubwa hubaki kumshangaa.

10. Kama ilivyo kwa tembo, mamba pia huwindwa na majangiri kinachomponza ni ngozi yake.

11. Aonapo hatari hukimbilia majini na akifika tu hugeuza kichwa chake alikotoka.

12. Mkia wake pia huutumia kama silaha, kumsukumia kiumbe anayejaribu kumshangaa nchi kavu, na ukishaingia kwenye maji naye huja.

13. Ni mnyama mwenye sumu kali ya nyongo, na nyongo yake ina sifa hizo kwa kuwa humsaidia katika mmeng'enyo wa chakula, kwani anapokula humeza hata mifupa.

14. Ni mnyama anayeua haraka, tofauti na wanyama wengine walao nyama, hivyo kifo chake si cha mateso kama ilivyo kwa simba au chui, ila kwa mtazamaji atapata hofu mara dufu kuliko akiona mauaji ya wanyama wengine.

15. Anaweza kunyata katika maji na kiumbe aliyepo pembeni asishtuke kabisa, akiwa mwanadamu ndio kabisa atakosa habari.

16. Mamba jike hapendi mambo ya mahaba, mara nyingi hutumia muda mwingi kulikimbia dume.

17. Madume kwa sababu ya ukubwa wao na uzito, wakati mwingine hutumia ubabe kulipanda jike lake.

18. Dume la mamba lina msaada mdogo kwa jike, msaada huo hutoa pindi linapokuwa na muda wa ziada.

19. Kutafuta chakula huweza kushirikiana ikiwa ni pamoja na kutengeneza mtego.

20. Mamba ni mnyama anayeweza kukumaki na akakutegea, kwa mfano ukiwa na tabia ya kuoga mtoni au kuchota maji kila ifikapo saa kumi katika eneo fulani, kuna siku anaweza akakutangulia nusu saa kabla na ukifika tu ndio umekwisha.

21. Anapopambana nchi kavu wakati wote hutumia kutishia zaidi kuliko kushambulia, ila wakati akili yake huielekeza kukuzubaisha ili akusukumie majini.

22. Anapong'ata huvunja kutokana na mfumo wa meno yake ulivyo, kwani meno ya juu na ya chini huyakutanisha pamoja
Hii habari imeandikwa bila kufanyiwa utafiti wowote. Nyongo haifanyi kazi ya umeng'enyaji
 
Mkuu hii habari kuwa sumu ya nyoka kazi yake kumeng'enya uliitoa wapi? Sumu ya nyoka ni kwaajili ya kujilinda na kuua. Nyoka kama koboko ana sumu inaitwa neurotoxin hii inaathiri mishipa ya fahamu na kufanya upalalyze. Nyoka kama kifutu ana cytotoxin hizi zinaua cell. Hizi ndiyo zinaozesha mguu. Huwezi ng'atwa na nyoka mwenye neurotoxin halafu mguu ukaoza.

Huyo muheshimiwa yupo sahihi, Sumu ya nyoka ni digestive agent yake pia, yaani inazo kazi mbili, moja ni silaha ya kujilinda na kukamatia mawindo yake na pili ni digestive agent. Mfano cobra au moma (puff adder) anapomgonga mtu hapo huwa anajilinda tu lakini anapomgonga panya hapo huwa ni silaha ya mawindo ndipo hapo hiyo sumu inapotapakaa ndani mwili wa huyo panya inaanza kummeng'enya ndani kwa ndani na hata huyo Moma anapommeza tayari huyo panya anakuwa kisha kuwa digested ndani kwa ndani na hata anapokuwa anammeza hutumia zile "fangs/(meno mawili yenye sumu)" zake kumvutia tumboni mwake na kipindi anamvutia tumboni kutumia hizo fangs ni wakati huohuo anapozidi ku inject sumu zaidi ndani ya mwili wa huyo panya na hivyo digestion inakuwa rahisi zaidi panya anapokuwa tumboni.

Koboko (Black mamba) yeye sumu yake ni mchanganyiko wa sumu zote mbili Neurotoxin na Cytotoxin.

Kifupi ni kwamba Sumu za nyoka ni digestive juice pia.
 
Ile ni nyongo kama nyongo zingine na research zinasema hivyo, sihitaji kuionja. Wewe unauhakika gani kuwa ni sumu, umewahi onja ikakuua?
Sasa si ndiyo umeambiwa ukaionje ili ulete mrejesho?kuhusu research kusema kuwa ni nyongo Kama nyongo zigine,vilevile research hizohizo zinasema ni sumu.
 
Hapo umezungumzia nyoka wenye sumu je nyoka kama common egg eater, chatu na rat snake ambao hawana sumu umeng'enyaji kwao hua inakuaje?
Hii mada nyingine. Ngoja nijaribu kuelezea kwa kifupi au ntakua naupdate taratibu. Nilimuelezea hivyo ili kuweka mlinganyo wa ikolojia na evolution ya kila kiumbe mpaka nimekua jinsi kilivyo

Sasa katika nyoka hao hao kuna baadhi ya exceptions kama hizo ulizozitaja. Nitaanza kumuongelea chatu kwa mfano yeye ana enzymes ambazo zinamsaidia kusaga kila kitu kasoro vile vyenye keratin tu(nywele, kucha,mapembe,manyoya nk). Na naomba niseme kitu kimoja katika kumeng'enya chakula Hcl(Hydrochloric Acid) ndo kitu kinachotegemewa sana(kitu muhimu) ila cha kushangaza acid iliyopo kwenye tumbo la binadamu no Kali(concentrated) zaidi tumewapita mbali sana chatu

Sasa bas nini kikubwa kinachomsaidia chatu kufanya digestion bila kung'ata kwanza. Kikubwa ni maumbile yake ya ndani ambapo ana uwezo wa kukuza organ zake hadi ukubwa mara tank zaidi akitaka kula. Na hivyo humsaidia kufanya kama anabana msosi tumboni na ile Hcl kidogo na enzymes nyingine bas chakula kinasagwa(kwa presha)

Napo huchukua hata wiki nzima kukamilisha hilo zoezi

So chatu akiwa amefikia muda wa kula moyo wake main I sijui organ gan zote pamoja na misuli ya tumbo inaanza kukua mpaka mara 4 ya saizi ya kawaida ili kuwezesha hilo nq pia akishamaliza kusaga chakula kuna hamna ambayo anaanza kujifanyia metabolism ya mwili wake mwenyewe(ni kama anajikula ndani) sijui kuelezea vizur kiswahili mpk viungo(organs) zinarudi saizi ya kawaida au ndogo kabisa na pia hii ni njia anayoitumia "kuconserve energy"
 
Back
Top Bottom