Huu upepo wanaJF wa kurudisha watoto kayumba kutoka EM wala sio maamuzi binafsi ni basi tu ukata umekuwa mkali

Huu upepo wanaJF wa kurudisha watoto kayumba kutoka EM wala sio maamuzi binafsi ni basi tu ukata umekuwa mkali

Mwenye akili timamu hawezi kuzisifua shule za serikali hata kidogo.wengi wetu tumesoma hizo shule tunazijua matatizo lukuki ya shule za umma ndiyo maana huwezi kumuona mtoto wa mkuu wa mkoa,wilaya,mkurugenzi,afisa elimu,waziri,rais au mfanyabiashara mkubwa kama gsm au Mohamed dewj.Lakini kapuku waliopauka wanajifariji eti mtoto kusoma Kwa shida ndiyo akili!Hawa wanajifariji elimu mbovu ya umma ndiyo wanaendekeza kizazi Cha kutumikishwa na watawala na siyo kujikomboa vizazi vyao.
 
Nikionaga mtu anaziita shule zetu za serikali ambazo wengi wetu sisi ndio zimetulea na kutupa msingi WA elimu na ufahamu tulionao leo hii, Huwa namdharau sana na kumuona mtu huyo Hana akili kabisa na ni LIMBUKENI MKUBWA.
 
Mi nimesoma kayumba nakumbuka form one lugha ilivyonisumbua hawa wangu hapana aiseee. Ntawalipia mpaka mwisho wangu washindwe wao tuuu.
 
Kiuhalisia hakuna CONNECTION yoyote atapata wewe kama huna hela usijisumbue kujitutumua misuli bure. Watu wakimaliza shule kila mtu anaelekea ustaarabu wake mwanao atabaki anasimulia tu nilisoma na fulani😀😀😀

Wekeza katika ujuzi, mtoto aende VETA akachukue ujuzi. Dunia ya leo ni ya ujuzi.Kwenda nje ya nchi ni swala la maamuzi tu hakutegemei na kwamba ulisoma Feza au st. Kayumba.

Waandalie watoto urithi kwa kuwanunulia viwanja na mashamba ya miti ya mbao na matunda.Wanunulie watoto HISA na BONDS katika makampuni mbalimbali huu ndo utajiri wa kurithishana kutoka kzazi kimoja kwenda kingine.Na sio kupoteza rasilimali kisa kuja kuomba ajita za serikali.

Mtaendelea kuona waindi na waarabu kama magenius ila hawa watu ni wa kawaida tu sema wanafikra tofauti kuhusu mali na utajiri.
Kumwandalia mshamba ya kulima bila kumwezesha elimu nzuri ya kujitambua ataishia kuyauza hayo mshamba ndani ya mwezi mmoja tu.kama unahela peleka English medium na kama unajimudu zaidi peleka international mwanao akafaidi elimu na siyo kuandaa mshamba ya urithi
 
🤣🤣 ndugu we sema hali yako ni ngumu kwa sasa.

Acha mambo ya kupigisha watu stori kwa kutunisha misuri ya typing fingers kuwa wanaosomesha em na international schools eti wana poteza muda.

Hata sisi tunapigika na "njaa-nuary" hii ila hauwezi kuta tunageuza wali kuwa ugali humu.

Sawa, Ngoja tusubirie wajukuu wa bakhresa waje mikorochini praimari
🏃🏃
 
Niandikie majina ya hao wazazi nikawaandikishe baby class niwalipie ada niwasomeshe wao na watoto wao
Kwamba umekosa kabisa watu WA kuwasaidia na badala yake unataka ukawasaidie hao wazazi wajinga wajinga wanalazimisha kuishi maisha yaliyo nje ya uwezo wao?

Mbona ukitembelea huko vijijini na mahospitalini hasa government hospitals Kuna watu wengi sana wanaohitaji msaada?
 
Kumwandalia mshamba ya kulima bila kumwezesha elimu nzuri ya kujitambua ataishia kuyauza hayo mshamba ndani ya mwezi mmoja tu.kama unahela peleka English medium na kama unajimudu zaidi peleka international mwanao akafaidi elimu na siyo kuandaa mshamba ya urithi
Kwani ukimpeleka EM au International School ndo atajitambua? Mfano wanafunzi wa BAOBAB.
 
Nikionaga mtu anaziita shule zetu za serikali ambazo wengi wetu sisi ndio zimetulea na kutupa msingi WA elimu na ufahamu tulionao leo hii, Huwa namdharau sana na kumuona mtu huyo Hana akili kabisa na ni LIMBUKENI MKUBWA.
Shule za serikali hazikukupa elimu Bora bila wewe kujua ndiyo maana unaona ni nzuri.lakini kama ungesoma international au English medium enzi zako ungekuwa zaidi ya hapo ulipo Sasa.
 
Kiuhalisia hakuna CONNECTION yoyote atapata wewe kama huna hela usijisumbue kujitutumua misuli bure. Watu wakimaliza shule kila mtu anaelekea ustaarabu wake mwanao atabaki anasimulia tu nilisoma na fulani😀😀😀

Wekeza katika ujuzi, mtoto aende VETA akachukue ujuzi. Dunia ya leo ni ya ujuzi.Kwenda nje ya nchi ni swala la maamuzi tu hakutegemei na kwamba ulisoma Feza au st. Kayumba.

Waandalie watoto urithi kwa kuwanunulia viwanja na mashamba ya miti ya mbao na matunda.Wanunulie watoto HISA na BONDS katika makampuni mbalimbali huu ndo utajiri wa kurithishana kutoka kzazi kimoja kwenda kingine.Na sio kupoteza rasilimali kisa kuja kuomba ajita za serikali.

Mtaendelea kuona waindi na waarabu kama magenius ila hawa watu ni wa kawaida tu sema wanafikra tofauti kuhusu mali na utajiri.
The smartest comment in this thread.

Umetisha sana mkuu, natamani tuichambue zaidi hii comment yako Kwa faida ya wengine hasa hapo kwenye para ya pili na ya tatu.
 
Kumwandalia mshamba ya kulima bila kumwezesha elimu nzuri ya kujitambua ataishia kuyauza hayo mshamba ndani ya mwezi mmoja tu.kama unahela peleka English medium na kama unajimudu zaidi peleka international mwanao akafaidi elimu na siyo kuandaa mshamba ya urithi
Acha ushamba na ulimbukeni yaani kulima mashamba nayo mpaka AKASOMEE ENGLISH MEDIUM (EM)😀😀😀😀

Njoo na hoja yenye mashiko kijana acha mbambamba,mtengenezee mtoto vyanzo vya utajiri acha kupoteza hela.Huko EM zaidi ya kulemaza watoto hata kufua tu hawafui watoto hawajui hata kufagia mnaenda kutengeneza watoto ambao wakitoka huko EM wanakuwa mzigo kwenye jamii.Hawa ndo kila siku wanakuja na mada za kuomba ushauri mambo madogo madogo ya kutumia tu akili ndogo.

Kujenga nyumba kwa kazi za kuajiriwa ni mtiti hahaaa yaani laki 7 mpaka millioni 2 ndio mishahara ya hizi ajira za serikali sasa hapo hata kupata kiwanja low density area ni mtiti ndo hao unakuta wanaenda kukenga nyumba viwanja vya 20×20.
Wekezeni kwenye vitu vimavyopanda thamani acheni ujinga kufata mkumbo na kuogopa kusimamia UKWELI kisa unahofu watu wanaokuzunguka watakuonaje!!!!
 
Halafu wakija huku wanajidai wanatoa ushauri,

Nani anasikiliza walioshindwa? Heri waongee ambao hawakupeleka kabisa watoto EM toka awali!

Ushindwe beer,urudi kwenye mataputapu halafu utuambie beer ni kupoteza hela!!! Kulewa ni kulewa tu!!!
 
Wazazi wengi wakishapiga hesabu ya kwamba anamsomesha mtoto kwa gharama alafu mwishowe anakosa ajira na status yake inakuwa sawa na aliyesoma Kayumba ndo huchukua maamuzi ya kuwapeleka watoto wao Kayumba.
Kuna shule ukisoma hutakosa ajira. Kwa sababu kama hautaajiriwa, utajiajiri kwa mafanikio makubwa!
Unemployed wengi wamesoma shule za kubahatisha tu.
 
Tuulize saint kayumba tunavyoteseka, ukiingia interview room kiingereza kinabaki njee kikikusubiria hadi utoke, wakati huo ushakosa opportunity 😁
Inasikitisha sana unakuta mtu anajua vitu ila kujieleza kwa Kingereza ni mtupu kabisa.
 
The smartest comment in this thread.

Umetisha sana mkuu, natamani tuichambue zaidi hii comment yako Kwa faida ya wengine hasa hapo kwenye para ya pili na ya tatu.
karibu mkuu,

Shida watu wanaishi kwa kuigana na wanaendeshwa na wanawake zao.Sahivi kumeibuka mashindano ya wanawake huku mitaani kupeleka watoto hizi EM😀😀😀😀sasa kwa wanaume wasio na dira wanajikuta wamenasa mtego na wanapukutisha pesa kuzikimbiza huko EM.
 
Back
Top Bottom