Huu utamaduni wa kuweka mashada ya maua makaburini umetokea wapi?

Huu utamaduni wa kuweka mashada ya maua makaburini umetokea wapi?

Tumetoka kumsindikiza jamaa wetu kafiwa na mama ake mzazi huko mkoani lakini mpaka mvua imetukuta uko porini wanasoma orodha ndefu ya watu watakao weka maua kwenye kaburi ya marehemu, tumetoka usiku na njia mbovu.

Hivi huo utamadini wa kuweka mashada kwenye undongo wa kaburi ulitoka wapi? Unasaidia nini? Umeandikwa kwenye Biblia?

Mwenye majibu sahihi tafadhari nijibu, mimi umenikera kweli kweli.
Halafu wengine hupigiwa mizinga..... 🙂
 
Mimi ni Mkristo,haya mambo ya Kijinga yanafanywa na wakristo WAJINGA!

Kuweka Shada juu ya kaburi la Marehemu ni UJINGA wa kiwango Cha Juu mno!

Hata kama usingekuwa mkristo kwani ujinga wa wale unakuhusu nini?

Kwamba wewe unawaona wajinga, labda nao wanakuona mjinga. Nani wa kuamua hiyo kesi Ili mjinga adhihirike?

Kulikoni kuwashwa washwa na yasiyokuhusu?

Mambo ya Ngoswe tangu lini yakawa na wabia?
 
Kwani utaratibu wa waislam kukafin ,kukamua maiti ulitoka wapi,hizi ni mila na tamaduni za walioleta hizi dini,wazungu na waarabu,Ni sunna,ukifanya sio dhambi,ukiacha sio dhambi rwlax
Katika uislamu maiti hakamuliwi.
Kama una uthibitisho tuwekee kitabu chochote cha fiqhi kinachotoa hayo maelekezo.

Kukafini ni kumvisha sanda maiti. Kwa kuwa maiti hawezi kujivalisha mwenyewe sanda basi anavalishwa. Hiki kitendo ndicho kinaitwa kukafini.
 
Tumetoka kumsindikiza jamaa wetu kafiwa na mama ake mzazi huko mkoani lakini mpaka mvua imetukuta uko porini wanasoma orodha ndefu ya watu watakao weka maua kwenye kaburi ya marehemu, tumetoka usiku na njia mbovu.

Hivi huo utamadini wa kuweka mashada kwenye undongo wa kaburi ulitoka wapi? Unasaidia nini? Umeandikwa kwenye Biblia?

Mwenye majibu sahihi tafadhari nijibu, mimi umenikera kweli kweli.
Majibu haya hapa! Why do we put flowers on the grave? - deBloemist.nl.
 
Tumetoka kumsindikiza jamaa wetu kafiwa na mama ake mzazi huko mkoani lakini mpaka mvua imetukuta uko porini wanasoma orodha ndefu ya watu watakao weka maua kwenye kaburi ya marehemu, tumetoka usiku na njia mbovu.

Hivi huo utamadini wa kuweka mashada kwenye undongo wa kaburi ulitoka wapi? Unasaidia nini? Umeandikwa kwenye Biblia?

Mwenye majibu sahihi tafadhari nijibu, mimi umenikera kweli kweli.
Ukiondoa uwekaji wa maua, mengine uliona ni sahihi? Kama ni ndio, sababu za usahihi ni zipi!?
 
Unajua wakuristu wa kiaAfrica hasa Tanzania tuna kiherehera cha kuiga wazungu kwa kila kitu bila kutumia akili zetu
Kabla ya wazungu na waarabu au kwa kifupi kabla ya kukutana na wageni, tulikuwa tunazika vipi? Au ndio ile kama ya Mamaasai kuhama boma na kucha mwili humo humo? Lakini, je kulikuwa na namna ya kuhama?
 
Mvua tu kidogo unakuja kulia lia huku, hovyo kabisa. Nyie mnavyokamua kimba maiti ina maana gani
Mbona wewe unaleta mambo ya kidini leta jibu la logic acha kukimbilia kwenye udini mimi siko kiudini plz.
 
Naona leo mmeamka na mashindano ya kuzika Wakristo vs Waislamu.

Huku wewe unahoji mashada na maua, kule jamaa yako amehoji "Kwa nini wanawake hawaruhusiwi kwenda kuzika makaburini?"

All in all, hii inadhihirisha Waafrika wengi mmeanza kuamka kutoka usingizi wa hizi dini tulizoketewa na kuanza kuhoji mambo ya msingi.
Mdogo mdogo wasioelewaa dini n uhuni tu wataanzaa kuelewaa ...
 
Mkuu nilikubali kila kitu, badaye leo asubuhi ndo nauliza the logic yake, kwanza yale maua yameharibika siku hiyo hiyo mvua, kwanini tunafuata dini kiujinga bila kutumia logic.

Mkuu nikurejee tena kwenye andiko langu, na hasa sehemu hii:

"Bahati mbaya kwa namna hii, umejipunguzia wachangiaji ambao kama nia yako ilikuwa njema ungenufaika na michango yao."

Kwa hakika mada yako labda ingekuwa hivi:

"Kwanini watu hushughulika na marehemu?"

Tena hata bila kujali ni wakristo au waislam ilitosha mno, ambapo ungeweza kuweka maua makaburini kama mfano tu.

Kwa maana nani asiyejua marehemu hana thamani yoyote?

Au nasema uongo ndugu yangu?

Ninakazia:

Vionjo vyako vya adha zilizokusibu huko, wengine vimetuletea ukakasi!
 
Tumetoka kumsindikiza jamaa wetu kafiwa na mama ake mzazi huko mkoani lakini mpaka mvua imetukuta uko porini wanasoma orodha ndefu ya watu watakao weka maua kwenye kaburi ya marehemu, tumetoka usiku na njia mbovu.

Hivi huo utamadini wa kuweka mashada kwenye undongo wa kaburi ulitoka wapi? Unasaidia nini? Umeandikwa kwenye Biblia?

Mwenye majibu sahihi tafadhari nijibu, mimi umenikera kweli kweli.
Ni upendo tu ni jambo nzuri la kuiga hakuna madhara hasi hapo.
 
Back
Top Bottom