- Thread starter
- #61
Wameitoa wapi? Mbona imani zingine hazifanyi hivo wanabuni tu af waita dini .Siyo mbaya kwasababu hiyo ndiyo sherehe ya mwisho ya Marehemu.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Wameitoa wapi? Mbona imani zingine hazifanyi hivo wanabuni tu af waita dini .Siyo mbaya kwasababu hiyo ndiyo sherehe ya mwisho ya Marehemu.
Binadamu bwana. Alafu kila jambo ukitaka ku question mbona utateseka sanaMvua tu kidogo unakuja kulia lia huku, hovyo kabisa. Nyie mnavyokamua kimba maiti ina maana gani
Unafaidika na nini kufanya uzushi?@mdukuzi
Umeshawahi kuosha maiti ya kiislamu?Mvua tu kidogo unakuja kulia lia huku, hovyo kabisa.
Kuna Dini zinaendesha kiubepari sanaa "Capitalism has interpolated christianity" tena sio dini ni biashara nilikua sijawahi kuona kanisa ya RC inafungua maduka pembeni yake inao uza vitu mbalimbali vikiwemu na mashada, lakini RC siku hizi maduka yamekua mengi sio dini ni biashara sasa, hu utamaduni usio kua na ushahidi kwenye bibulia tuachane nao.Huu utamaduni umekuzwa tu hiv karibun na hasa baada ya tech kuongezeka watu kuona ona haya mambo.
Miaka 10 nyuma mikoani hatukuaga na huu utamaduni, mnazika mna fukia mnasepa..
NI ujinga ujinga tu baada ya biashara kuwa ngumu watu wanakuza mambo ilimrad biashara zifanyike.
Uliza bei za hayo maua sasa, utachoka!!
Tumetoka kumsindikiza jamaa wetu kafiwa na mama ake mzazi huko mkoani lakini mpaka mvua imetukuta uko porini wanasoma orodha ndefu ya watu watakao weka maua kwenye kaburi ya marehemu, tumetoka usiku na njia mbovu.
Hivi huo utamadini wa kuweka mashada kwenye undongo wa kaburi ulitoka wapi? Unasaidia nini? Umeandikwa kwenye Biblia?
Mwenye majibu sahihi tafadhari nijibu, mimi umenikera kweli kweli.
Hizi dini ni mila za jamii fulani tu. We tazama vizuri utagundua kila dini ina mila za kule ilikotoka.
Ukristo una mila za kizungu ndani yake japo mfano ukatoliki uko blended na mila za maeneo pia. WAfilipino kuna vitu huvifanya katika ibada zao ambapo Wakatoliki wa Brazili hawafanyi.
Wahindu nao utaona imani yao iko blended na mila za wahindi, same to Muslims na mila za Waarab mfano kufuga ndefu wakati Bw. zakayo Rwejuna hana ndevu ndefu kama waarabu.
So haya masuala ya kuweka sijui maua sijui whaat ni mila tu za wazungu huko.
Kuna haja gani kudandia utamaduni wa watu ukiacha wa kwenu?Utamaduni wa kuweka mashada ya maua makaburini ni mojawapo ya desturi zinazojulikana katika jamii nyingi duniani. Ingawa kila jamii ina sababu zake za kipekee zinazohusiana na tamaduni zao, kuna mambo ya msingi yanayofanana katika utamaduni huu.
Historia na Asili
Asili ya utamaduni huu inaweza kufuatiliwa katika tamaduni za kale. Katika historia, watu walikuwa na imani kwamba wafu wanahitaji heshima na kumbukumbu, na kuweka maua makaburini ilikuwa njia moja ya kuonyesha heshima hiyo. Katika tamaduni mbalimbali, kama vile Wagiriki na Wanaroma, ilikuwa kawaida kuweka maua kwenye makaburi ili kuwatunza wafu na kuwakaribisha katika maisha ya baadae.
Katika tamaduni za Kiafrika, kuweka maua na vitu vingine kwenye makaburi ilikuwa ni njia ya kuonyesha upendo na heshima kwa wafiwa. Watu walitumia maua ya ndani na nje ya maeneo yao, ambayo yalikuwa na maana ya kiroho na kiutamaduni. Kila aina ya maua ilikuwa na maana yake, na mara nyingi ilihusishwa na sifa za mtu aliyekufa.
Maana ya Maua
Maua yana umuhimu mkubwa katika tamaduni nyingi. Kila aina ya maua inaweza kuwa na ujumbe maalum. Kwa mfano, rose nyekundu mara nyingi inahusishwa na upendo, wakati lily inaashiria usafi na unyofu. Katika muktadha wa makaburi, maua yanatumika kuwakumbusha wafu na kuonyesha hisia za huzuni na upendo. Watu hujumuisha aina mbalimbali za maua, ikiwa ni pamoja na maua ya msimu, ili kuonyesha mabadiliko ya maumbile na maisha.
Utamaduni wa Kulea na Kukumbuka
Kuweka mashada ya maua makaburini pia ni sehemu ya utamaduni wa kulea na kukumbuka. Katika jamii nyingi, siku maalum kama Siku ya Wafu au Siku ya Kumbukumbu zinasherehekewa kwa kuweka maua kwenye makaburi. Hii ni njia ya kuonyesha kwamba wafu bado wanakumbukwa na wanahusishwa na maisha ya waliohai. Katika baadhi ya tamaduni, watu huenda kwenye makaburi kwa ajili ya maombi na kufanyika sherehe za kumbukumbu, huku wakileta maua kama sehemu ya sherehe hizo.
Mabadiliko ya Utamaduni
Katika nyakati za kisasa, utamaduni wa kuweka mashada ya maua makaburini umebadilika. Watu wengi sasa wanatumia mbinu za kisasa na vifaa vya kisasa, kama vile vyombo vya plastiki na maua ya bandia, ili kudumisha kumbukumbu za wafu. Ingawa kuna mabadiliko haya, maana ya msingi ya heshima na kumbukumbu bado inaendelea kuwepo.
Katika baadhi ya maeneo, watu wanatumia maua ya asili yanayokua katika mazingira yao ili kuonyesha uhusiano wa karibu na asili. Hii inasaidia kuimarisha utamaduni wa eneo hilo na kuonyesha umuhimu wa mazingira katika kumbukumbu za wafu.
Athari za Kijamii na Kihisia
Utamaduni wa kuweka mashada ya maua makaburini una athari kubwa katika jamii. Unawasaidia watu kushiriki hisia zao na kuonyesha huzuni na upendo kwa wafiwa. Kuweka maua kwenye makaburi ni njia ya kuungana na familia na marafiki, na kutoa nafasi ya kutafakari kuhusu maisha na kifo. Hii pia inaweza kusaidia katika mchakato wa kuomboleza, ambapo watu wanapata faraja kupitia shughuli hii ya pamoja.
Hitimisho
Kwa ujumla, utamaduni wa kuweka mashada ya maua makaburini ni wa kipekee na wenye maana katika jamii nyingi. Inaonyesha jinsi watu wanavyoweza kuonyesha heshima na upendo kwa wafu wao, huku wakikumbuka umuhimu wa maisha na uhusiano wa kibinadamu. Ingawa mitindo na mbinu zinaweza kubadilika, dhamira ya msingi ya kumbukumbu na heshima inabaki kuwa thabiti.
Utamaduni huu unaendelea kuungana na mambo ya kiroho, kihisia, na kijamii, na hivyo kuimarisha nafasi yake katika maisha ya kila siku ya watu.
ukristo umesambazwa zaidi na roman empire baada ya mfalme Charlemagne kuintergrate katika serikali ikafika kipindi hadi wao ndio wakawa kama wanao wacrown wafalme na emperors.Ukristo haujaanza kwa wazungu, Middle East ndio chimbuko la Uyahudi, Ukristo na Uislamu.
Elimu yako ndogo sana,unajua gata hiyo dini uliyonayo ni utamaduni wa watu,kama unaabudu mizimu swali lako lina hoja ,vinginevyo umepotokaKuna haja gani kudandia utamaduni wa watu ukiacha wa kwenu?
Elimu yangu haina uhusiano na kuweka mashada kwenye kaburi, nyie wenye elimu ndo mnafanya huo ujinga wa kuiga bila kutumia mantiki.Elimu yako ndogo sana,unajua gata hiyo dini uliyonayo ni utamaduni wa watu,kama unaabudu mizimu swali lako lina hoja ,vinginevyo umepotoka
Mkuu hakuna mahali Usabato umezungumzwa hapa,hapa unazungumzwa Ukristo!Ujinga unakujaje hapo?Maua yakiwekwa juu ya kaburi yanakukera nini?Huo usabato wako nao ni kero kwa wengine.
Ndo yaleyale tu,kuweka mashada/maua pamoja na kujengea makaburi ni Upagani!Ardhi haipanuki ukijengea kaburi ni ubinafsi.
Nadhani wewe pia unaweza ukawa unaongoza Kwa Ujinga kwasababu unachangia mada ambayo haikuhusu!Hata kama usingekuwa mkristo kwani ujinga wa wale unakuhusu nini?
Kwamba wewe unawaona wajinga, labda nao wanakuona mjinga. Nani wa kuamua hiyo kesi Ili mjinga adhihirike?
Kulikoni kuwashwa washwa na yasiyokuhusu?
Mambo ya Ngoswe tangu lini yakawa na wabia?
kwa P-DIDDY!!Tumetoka kumsindikiza jamaa wetu kafiwa na mama ake mzazi huko mkoani lakini mpaka mvua imetukuta uko porini wanasoma orodha ndefu ya watu watakao weka maua kwenye kaburi ya marehemu, tumetoka usiku na njia mbovu.
Hivi huo utamadini wa kuweka mashada kwenye undongo wa kaburi ulitoka wapi? Unasaidia nini? Umeandikwa kwenye Biblia?
Mwenye majibu sahihi tafadhari nijibu, mimi umenikera kweli kweli.
ikishachachamaa mitandaoni hii mijadala inaingia rasmi mitaani waziwaziNaona leo mmeamka na mashindano ya kuzika Wakristo vs Waislamu.
Huku wewe unahoji mashada na maua, kule jamaa yako amehoji "Kwa nini wanawake hawaruhusiwi kwenda kuzika makaburini?"
All in all, hii inadhihirisha Waafrika wengi mmeanza kuamka kutoka usingizi wa hizi dini tulizoketewa na kuanza kuhoji mambo ya msingi.
Mkuu hongera umeliweka sawa watu wamejaa unafiki mtupu, mtu katabika kashindwa hata kupata 50k za drip af akifa eti mnaonyesha upendo, kwani mashada na upendo wapi na wapi, huo sio utamaduni wetu mimi sijawahi kuona bibi yangu anapeleka maua ka babu yangu.Mkuu hakuna mahali Usabato umezungumzwa hapa,hapa unazungumzwa Ukristo!
Tafsiri ya Kuweka Maua kwenye kaburi maana yake ni Upendo Kwa Marehemu!
Ni mtu asiyekuwa Kuwa na akili akaipende maiti ashindwe kupenda walio hai!
WAKRISTO TUACHE UNAFIKI TUPONE!
Hizo fedha na gharama zilizotumika kununua hayo maua na mashada kwanini zisizumike kusaidia watu wenye uhutaji na wagonjwa ingali wakiwa hai?
Huyo Marehemu mnayemuwekea mashada na maua wakati akiwa hai yawezekana hata hayo maua hakuwahi kumnunulia ili kumuonyesha upendo,ila kwakuwa amekufa ndiyo anaonekana mzuri!
Sasa endelea kudhani kila ukweli unaosemwa ni kwakuwa asemaye ni Msabato!,Hii inachoma kwasababu wakristo wa kizazi Cha Sasa hawataki kitu inaitwa "UKWELI", wao wanataka maneno ya kufurahishwa mioyo Yao!