Huu utamaduni wa kuweka mashada ya maua makaburini umetokea wapi?

Halafu wengine hupigiwa mizinga..... 🙂
 
Mimi ni Mkristo,haya mambo ya Kijinga yanafanywa na wakristo WAJINGA!

Kuweka Shada juu ya kaburi la Marehemu ni UJINGA wa kiwango Cha Juu mno!

Hata kama usingekuwa mkristo kwani ujinga wa wale unakuhusu nini?

Kwamba wewe unawaona wajinga, labda nao wanakuona mjinga. Nani wa kuamua hiyo kesi Ili mjinga adhihirike?

Kulikoni kuwashwa washwa na yasiyokuhusu?

Mambo ya Ngoswe tangu lini yakawa na wabia?
 
Kwani utaratibu wa waislam kukafin ,kukamua maiti ulitoka wapi,hizi ni mila na tamaduni za walioleta hizi dini,wazungu na waarabu,Ni sunna,ukifanya sio dhambi,ukiacha sio dhambi rwlax
Katika uislamu maiti hakamuliwi.
Kama una uthibitisho tuwekee kitabu chochote cha fiqhi kinachotoa hayo maelekezo.

Kukafini ni kumvisha sanda maiti. Kwa kuwa maiti hawezi kujivalisha mwenyewe sanda basi anavalishwa. Hiki kitendo ndicho kinaitwa kukafini.
 
Majibu haya hapa! Why do we put flowers on the grave? - deBloemist.nl.
 
Ukiondoa uwekaji wa maua, mengine uliona ni sahihi? Kama ni ndio, sababu za usahihi ni zipi!?
 
Unajua wakuristu wa kiaAfrica hasa Tanzania tuna kiherehera cha kuiga wazungu kwa kila kitu bila kutumia akili zetu
Kabla ya wazungu na waarabu au kwa kifupi kabla ya kukutana na wageni, tulikuwa tunazika vipi? Au ndio ile kama ya Mamaasai kuhama boma na kucha mwili humo humo? Lakini, je kulikuwa na namna ya kuhama?
 
Mvua tu kidogo unakuja kulia lia huku, hovyo kabisa. Nyie mnavyokamua kimba maiti ina maana gani
Mbona wewe unaleta mambo ya kidini leta jibu la logic acha kukimbilia kwenye udini mimi siko kiudini plz.
 
Mdogo mdogo wasioelewaa dini n uhuni tu wataanzaa kuelewaa ...
 
Mkuu nilikubali kila kitu, badaye leo asubuhi ndo nauliza the logic yake, kwanza yale maua yameharibika siku hiyo hiyo mvua, kwanini tunafuata dini kiujinga bila kutumia logic.

Mkuu nikurejee tena kwenye andiko langu, na hasa sehemu hii:

"Bahati mbaya kwa namna hii, umejipunguzia wachangiaji ambao kama nia yako ilikuwa njema ungenufaika na michango yao."

Kwa hakika mada yako labda ingekuwa hivi:

"Kwanini watu hushughulika na marehemu?"

Tena hata bila kujali ni wakristo au waislam ilitosha mno, ambapo ungeweza kuweka maua makaburini kama mfano tu.

Kwa maana nani asiyejua marehemu hana thamani yoyote?

Au nasema uongo ndugu yangu?

Ninakazia:

Vionjo vyako vya adha zilizokusibu huko, wengine vimetuletea ukakasi!
 
Ni upendo tu ni jambo nzuri la kuiga hakuna madhara hasi hapo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…