Huu utamaduni wa kuweka mashada ya maua makaburini umetokea wapi?

Mimi ni Mkristo,haya mambo ya Kijinga yanafanywa na wakristo WAJINGA!

Kuweka Shada juu ya kaburi la Marehemu ni UJINGA wa kiwango Cha Juu mno!
Ujinga unakujaje hapo?Maua yakiwekwa juu ya kaburi yanakukera nini?Huo usabato wako nao ni kero kwa wengine.
 
Ni upendo tu ni jambo nzuri la kuiga hakuna madhara hasi hapo.
Kuna faida gani mpaka mvua inatunyeshea, na kuna watu hawapewi nafasi kuweka hayo maua si ubaguzi huo? Tunafanya vitu bila muongozo wa bibulia si uzushi huo?
 
Ndomana Roma anataka apewe maua yake kabla hata hajafa
 
Muungo acha kushusha heshima yako hapa siko kiudini mkuu.
 
Kuna faida gani mpaka mvua inatunyeshea, na kuna watu hawapewi nafasi kuweka hayo maua si ubaguzi huo? Tunafanya vitu bila muongozo wa bibulia si uzushi huo?
Miongozo mingi ya kikirsto ni kutoka europe na hasa Italy Vatican na wala sio kwenye bible.
 
Kuweka mashada au maua makaburini ni tamaduni za kuiga kutoka kwa wazungu, haipo kidini.
Hata kuzika kwenye masanduku bado haipo kidini.

Nchi nyingi zilizoendelea (hususani za wazungu) kwa sasa maiti inapigwa moto mpaka kupata jivu, na ndugu hupewa sampuli ya majivu wapeleke popote, watupe, wahifadhi ndani au wafukie chini hiyo ni shauri yao. Hii njia ni safi sana, naikubali mnoo.
 
KUkamuliwa ni lazima
Lengo lako naona ni kukera wauslamu kakini naona wamekupuuza, wewe kama huna majibu ya mashada makaburini pisha wanao jua wajibu, chuki zako weka pembeni.
 
Hiyo ilikiwa mara Yako ya kwanza kuona? Na kila kinachfanuwa ni lazima kiandikwe kwenye biblia au Sheria jifunzeni kufata taratibu mnazozikuta . Okay wewe usiudhurie aina hiyo ya misiba
 
Huwezi kupata majibu mambo mengi tumekaririshwa...hatuwezi kuyaacha yameshaingia kwenye mishipa ya damu kiufupi niheshima za mwisho + unafki kwa marehemu..! ukute marehemu enzi za uhai wake alikosa hata fedha ya matibabu hakuna aliyemchangia sasa akifariki vitu vitakavyo nunuliwa hapo utachoka mwenyewe.
 
Lengo lako naona ni kukera wauslamu kakini naona wamekupuuza, wewe kama huna majibu ya mashada makaburini pisha wanao jua wajibu, chuki zako weka pembeni.
Majibu nimekupa kuwa ni tamaduni za wazungu wa kale kabla hata ya ukristo, hiyo ni sunna,sasa ulitaka waarabu waweke maua wayatoe wapi jangwani
 
Jukumu la kulinda uhai wako ni la kwako binafsi,ila kwa vile huwrzi kujizika sisi tutakuzika usitinukie,hakuna unafiki hapo
Linda uhai wako
 
Hiyo ilikiwa mara Yako ya kwanza kuona? Na kila kinachfanuwa ni lazima kiandikwe kwenye biblia au Sheria jifunzeni kufata taratibu mnazozikuta . Okay wewe usiudhurie aina hiyo ya misiba
Mkuu mengine yanafuata kutoka wapi kama sio bibulia, lazima tuwe na muongozo sio kufuata vitu hovyo mkuu, tuna marafiki wengi kutoka imani tofauti tunahaja ya kuelewa na kujifunza mambo mengine inao fanyika nao.
 
Siyo mbaya kwasababu hiyo ndiyo sherehe ya mwisho ya Marehemu.
 
Sasa hapo tunafuata dini au utamaduni usio kua na msingi youote, wakuristu kuna haja ya kusoma na kuelewa dini yetu zaidi na zaidi.
 
Mimi ni Mkristo,haya mambo ya Kijinga yanafanywa na wakristo WAJINGA!

Kuweka Shada juu ya kaburi la Marehemu ni UJINGA wa kiwango Cha Juu mno!
Ardhi haipanuki ukijengea kaburi ni ubinafsi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…