Huu utaratibu wa kuhubiri injili kwenye magari ya abiria ni kero kubwa, LATRA muingilie kati

Huu utaratibu wa kuhubiri injili kwenye magari ya abiria ni kero kubwa, LATRA muingilie kati

Kero Yao ndogo kulinganisha na hao wengine
Udogo wa kero unategemea kiroho uko vipi.
Ukiwa na nguvu za Mungu huwezi kuona kero mtu anaposema neno la Mungu.
 
Udogo wa kero unategemea kiroho uko vipi.
Ukiwa na nguvu za Mungu huwezi kuona kero mtu anaposema neno la Mungu.
Inatakiwa wakubaliene na kitu kimoja kwamba jamii yetu ni mchanganyiko watu wenye Imani,tamaduni na ustaarabu tofauti haiwezekani uje kwenye daladala utuhubirie kama upo kanisani na waumini wenzio .
Kila mtu anao uhuru lakini ustaarabu wa watu wengine ni jambo la kuzingati
 
Sasa Kama mnapenda hayo mahubiri si mwende kwenye Nyumba za ibada, na ma bus yabaki kua ni kwa ajili ya safari na si vinginevyo!!!
Mkuu acha kiburi cha uzima. Shetani anakuwa kazini sana kipindi cha safari. Ndio maana madereva wametulia hawapati kero ila wewe abiria unaona kero.
 
Hebu vuta picha wangekuwa waislamu au waislamu na wao wafanye kama hivyo tungepata utulivu kweli. Ibada inatakiwa ifanyike sehemu maalumu ambayo imeshatengwa (msikitini, kanisani) at least wanaojenga majukwaa mitaani ,sio hao wengine kila Kona wanahubiri tu inakuwa sasa kama wamekosa namna ya huwavuta watu kwenye dini wanaamua kulazimisha
Kwani wamekwambia wanavuta watu ama wanahubiri tuu
 
Inatakiwa wakubaliene na kitu kimoja kwamba jamii yetu ni mchanganyiko watu wenye Imani,tamaduni na ustaarabu tofauti haiwezekani uje kwenye daladala utuhubirie kama upo kanisani na waumini wenzio .
Kila mtu anao uhuru lakini ustaarabu wa watu wengine ni jambo la kuzingati
Kwa hiyo shida yako ni kero ya kelele au tofauti ya kiimani!
 
Hebu vuta picha wangekuwa waislamu au waislamu na wao wafanye kama hivyo tungepata utulivu kweli. Ibada inatakiwa ifanyike sehemu maalumu ambayo imeshatengwa (msikitini, kanisani) at least wanaojenga majukwaa mitaani ,sio hao wengine kila Kona wanahubiri tu inakuwa sasa kama wamekosa namna ya huwavuta watu kwenye dini wanaamua kulazimisha
Kwani wamekwambia wanavuta watu ama wanahubiri tuu
 
Mtu unasafri zako unahitaji mapumzko anatokea mtu anajifanya analeta neno la Bwana bila kujua watu waliopo ndani wanatatizo gani wengine hawataki kelele anajifanya anahubiri dakika 3 anaomba sadaka.

Hebu tufanye kazi tusijifiche kwa kivuli cha kuhubiri na kulazimisha sadaka.
huu utaratibu upo Kenya, zambia ,congo na Zimbabwe ...mabus yote huwa wanaingia watumishi na wanaomba na kusepa

hamna namna vumilia tu -kama mapepo yamechukua hatamu kichwani mwako tulia tu
 
Utaratibu ni jambo muhimu sio kuja kufuata ukwasi wa sadaka mungu wetu sote na neno tunalipenda na tunalijua ila
Approach yao hapana
 
Kwa hiyo shida yako ni kero ya kelele au tofauti ya kiimani!
Shida ni hizo kero Imani haiwezi Kuna tatizo kwangu kwasababu natambua kila mtu anayo haki ku-practice Imani yake lakini katika kiwango kisicho leta usumbufu kwa wengine ,ndio maana tunapiga kelele sauti za mahubiri jioni na za adhana asubuh zipunguzwe na sio zitolewe ,Kila kitu kifanyike mahala pake palipo kusudiwa
 
Mungu ni kila kitu jamani, ingekua kheri kumtukuza Mungu kila pahala. Mtu asiyependa mahubiri ana mapepo ya kutosha, kwake ni kero!
Kama kwako unaona unahitaji kupumzika, Mungu naye apumzishe Pumzi yake kwa wakati huo au aondoe macho yako kwa wakati huo - kisha tuone kama ungekataa mahubiri. Mungu ni Yote katika Yote.
Tena nakushauri umpokee huyo YESU maana bila YESU ni ubatili na kujilisha upepo.
Hivi atakuwa kweli hapendi mahubiri au anachoshauri ni mahubiri hayo kufanyika sehemu rasmi?
 
Mnaosema mleta uzi anunue gari lake ni maskini wa kipato hadi akili. Pia hamjawahi tembea hata hapo Nairobi. Gari kwa wenzetu sio luxury ni basic need. Watu huwa wanatoka na gari nyumbani wanapaki stesheni ya treni kisha kupanda treni na kwenda huko wanakokwenda baada ya kazi anarudi na gari lake home. Kwa hiyo unaweza kuwa na gari na pia ukatumia usafiri wa umma na wala sio umaskini. Mnaosema anunue lake mmejaa roho za kimaskini mno.

Hao wahubiri wa kwenye magari wajue kwenye usafiri wa umma kila mtu ana imani yake kwahiyo tusilazimishane. Tukisema kila imani ilete mhubiri kwenye basi tutaelewana? Na hao wahubiri wote ni wa kikristo lakini huwezi kuta mkatoliki, msabato, na madhehebu mengine ya kuheshimika wana wahubiri kwenye mabasi. Hao wa kwenye mabasi ni wapigaji style ya Geor Davie, Mwamposa, Nabii Mashimo, Mzee wa upako na kina Mwingira. Kwamba wao ndo wanazuia ajali kupitia mahubiri yao ni upumbavu mwingine unaopaswa kukemewa. Mungu ana upendo na huwa anaona nia zetu kwamba tunahitaji sana ulinzi wake tufike salama lakini Mungu hawezi kuja kuendesha gari mwenyewe. Na pia Mungu kwasababu alishatupa uhuru wa kutumia akili zetu hawezi mlazimisha dereva afuate sheria za barabara. Kwahiyo Mungu atatulinda safarini jinsi tunavyostahili sio hadi kwenye mambo ya kizembe.
 
Hivi atakuwa kweli hapendi mahubiri au anachoshauri ni mahubiri hayo kufanyika sehemu rasmi?
injili inahubiriwa na itahubiriwa - kila mahala mkuu, na kwa kila kiumbe.... nawewe unapinga injili nini?
kama pombe na miziki ya kidunia, na umbea (kazi za shetani) hujazipigia kelele unaanzaje kupinga kazi ya Mungu?
 
Shida ni hizo kero Imani haiwezi Kuna tatizo kwangu kwasababu natambua kila mtu anayo haki ku-practice Imani yake lakini katika kiwango kisicho leta usumbufu kwa wengine ,ndio maana tunapiga kelele sauti za mahubiri jioni na za adhana asubuh zipunguzwe na sio zitolewe ,Kila kitu kifanyike mahala pake palipo kusudiwa
Unajichanganya. Nishakusoma tatizo lako. Jaa nguvu za Mungu hutasumbuliwa na imani ya aina yoyote.
 
Aiseeee
Mleta mada naona Ana point NZURI Sana na watu mmemuelewa Ila watu mnajitoa ufahamu.
Hakuna mtu asiyependa Dini kusali na Kama wapo Basi wanamatatizo makubwa Sana.
Point ni kwamba waende sehemu maarumu au bus kabla ya safari waingie waombe waondoke.Jamani sio Siri utakuta mwingine lengo Ni Sadaka na Kama huamini akiona Sadaka hajapata anaanza kulaumu pengine na kuwalaani abilia eti hawamjui Mungu kumbe hawana kweli.
Point Ni kwamba tuheshimu wengine.
Mahubiri Ni mazuri Sana Ila yafanyike pahala pazuri panyenyekevu pa Mungu.
Hii kwamba wanaoshauri Basi Wana mapepo hapana hatutendi sawa labda hayo mapepo ndo hayo yamewaandikia

Sent from my Infinix X657B using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom