Huu utaratibu wa kuhubiri injili kwenye magari ya abiria ni kero kubwa, LATRA muingilie kati

Huu utaratibu wa kuhubiri injili kwenye magari ya abiria ni kero kubwa, LATRA muingilie kati

Nachukia kwelikweli, kwa vile tu sina uwezo wa kumchomoa kwenye gari
 
Hatubishani sisi hapa tunafahamishana kama watu wazima tuliostaarika ,hata nikilinunua Hilo bus Bado usumbufu hauta koma .

Tukiwa na shida ya mahubiri tunafungulia redio tuwasikilize au tutakuja kanisani kwa ridhaa zetu na kama mnataka tupate mahubiri basi andaeni semina maalumu au jengeni majukwaa watu watakuja kwa hiari zao
ULITAKA APANDE BASI KWA RUHUSA YAKO...?
 
Nashukuru kwetu,msigwa alishawapiga stop,maana walikuwa wanamfukuzia wateja,

Sikh hizi burudani hamna kero ya mahubiti wala biashara zisizo na majina.
 
ULITAKA APANDE BASI KWA RUHUSA YAKO...?
Sitoi ruhusa kwa yeyote tunataka wawe watulivu kwenye mabasi kama wanashindwa kuvumilia kuhubiri basi waandike vipeperushi vya mahubiri wagawe kwa watu wanaopenda watasoma
 
Wakati utakuja ambao hao unao waona kero sasa utawatafuta wakupe Injili na hutawaona!
Injili ni habari njema ambayo ni kwa ajili ya watu wote, lakini wanaohubiri wanatakiwa pia kuwa ba busara katika kuhuhiri kwao. Kwa mfano kuomba sadaka ndani ya basi baada ya kuhubiri kwangu naona haijakaa sawa.
 
Nimefatilia Mjadala, nimebaki najiuliza hivi Hao wanaowajibu wenzao kwa Dhihaka kuwa Wana Mapepo badala ya Kujenga hoja nao ni Walokole?

Hoja hujibiwa Kwa Hoja....! Hivi humo ndani Ya Basi kila Mtu akaanza kwa Imani Yake kuhubiri Patakalika.

Kila Mtu ana Imani Yake, ni bora Watu Wasikwazane...!

Kila Jambo lina Sehemu Yake.
 
Mtu unasafri zako unahitaji mapumzko anatokea mtu anajifanya analeta neno la Bwana bila kujua watu waliopo ndani wanatatizo gani wengine hawataki kelele anajifanya anahubiri dakika 3 anaomba sadaka.

Hebu tufanye kazi tusijifiche kwa kivuli cha kuhubiri na kulazimisha sadaka.
Tukiwaendekeza watu kama nyie mtakuja kulalama pia azana inawapigia kelele asubh mkiwa na hangover ya jana
 
Napenda mahubiri...

Neno la Mungu ni taa na mwanga linatumulika popote tunapokwenda...
Neno la Mungu fanyia nyumban kwako na familia yako, acha kusumbua watu kwenye safari
 
Back
Top Bottom