Huu utaratibu wa kuhubiri injili kwenye magari ya abiria ni kero kubwa, LATRA muingilie kati

Huu utaratibu wa kuhubiri injili kwenye magari ya abiria ni kero kubwa, LATRA muingilie kati

Mtu unasafri zako unahitaji mapumzko anatokea mtu anajifanya analeta neno la Bwana bila kujua watu waliopo ndani wanatatizo gani wengine hawataki kelele anajifanya anahubiri dakika 3 anaomba sadaka.

Hebu tufanye kazi tusijifiche kwa kivuli cha kuhubiri na kulazimisha sadaka.

Ndio wanazidi kuharibu akili za watu Na ndio maama ajali zinazidi maana watu wanaacha kutumia akili zao kutafakari na kuamini kutoka kwa mtu tu! Yaani hayo mahubiri hayaendani na tatwimunza ajali hapa Tanzania. Kama yangekuwa yanasaidia ajali zingepungua..... Mbona mambo haya kwenye usafiri wa ndege au Train hayapo.?
 
Shukuru unalipata hata dakika 3 kunamahali utalihitaji na utalipata.
 
Nawapenda San wanaohubiri ktk magari na masokoni Jana nilipita karume nikamkuta mama anahubiri pale machinga complex aisee roho ilimiuuma sna kwann sijampa sadaka yangu
 
Nawapenda San wanaohubiri ktk magari na masokoni Jana nilipita karume nikamkuta mama anahubiri pale machinga complex aisee roho ilimiuuma sna kwann sijampa sadaka yangu
Sasa kwa nini hukumpa?
 
Mtu unasafri zako unahitaji mapumzko anatokea mtu anajifanya analeta neno la Bwana bila kujua watu waliopo ndani wanatatizo gani wengine hawataki kelele anajifanya anahubiri dakika 3 anaomba sadaka.

Hebu tufanye kazi tusijifiche kwa kivuli cha kuhubiri na kulazimisha sadaka.
Binafsi sioni shida kwa kuhubiriwa neno la mungu kwa maana hata kufika salama huko niendako ni kwa neema za mungu.
 
Mtu unasafri zako unahitaji mapumzko anatokea mtu anajifanya analeta neno la Bwana bila kujua watu waliopo ndani wanatatizo gani wengine hawataki kelele anajifanya anahubiri dakika 3 anaomba sadaka.

Hebu tufanye kazi tusijifiche kwa kivuli cha kuhubiri na kulazimisha sadaka.
Kuhubiri pia ni kazi. Au unadhani mashehe, mapadre na wachungaji ni wazururaji?
 
Najua wengi watakukejeli kwa kusema ununue gari lako, wengi pia naona wameshasema, ila ukweli haupingiki hizi dini za ulokole ni shida.
Hao wanaosema kuwa ununue gari lako hautopata kadhia ya wachungaji wa kilokole wanaoganga njaa, wanasahau kuwa hao waganga njaa hawaishii kwenye mabus tu hata majumbani upita, na mafundisho yao ni ujinga mtu ( kupokea magari nk na kufunguliwa).

Kila mmoja ana uhuru wa kuabudu ila kuabudu kunapokuwa kero kwa watu wengine hilo ni tatizo na linaweza kuleta migogoro isiyo ya lazima​
 
Mathayo 24:14

Tena habari njema ya ufalme itahubiriwa katika ulimwengu wote, kuwa ushuhuda kwa mataifa yote; hapo ndipo ule mwisho utakapokuja.

Kama kanisani huendi , msikitini huendi, chaneli za dini husikilizi wala kuangalia, bora injili ikufuate hukohuko.
Biblia naipenda maana hutoa maonyo mapema, Mathayo 7:15-29 " Jihadharini na manabii wa uongo wanawajia wakiwa wamevaa ngozi ya kondoo, kumbe ndani ni mbwa mwitu wakali mtawatambua kwa matendo yao..."
Hao wanaojiita manabii mafunzo yao tu yanatosha kutambua kuwa ni wafanyabiashara kama wafanyabiashara wengine, mafundisho yao ni kutoa tu, yaani wanawaibia na kuwanyonya watu kwa mwamvuli wa dini.​
 
Biblia naipenda maana hutoa maonyo mapema, Mathayo 7:15-29 " Jihadharini na manabii wa uongo wanawajia wakiwa wamevaa ngozi ya kondoo, kumbe ndani ni mbwa mwitu wakali mtawatambua kwa matendo yao"
Hao wanaojiita manabii mafunzo yao tu yanatosha kuta​

Biblia naipenda maana hutoa maonyo mapema, Mathayo 7:15-29 " Jihadharini na manabii wa uongo wanawajia wakiwa wamevaa ngozi ya kondoo, kumbe ndani ni mbwa mwitu wakali mtawatambua kwa matendo yao"
Hao wanaojiita manabii mafunzo yao tu yanatosha kutambua kuwa ni wafanyabiashara kama wafanyabiashara wengine, mafundisho yao ni kutoa tu, yaani wanawaibia na kuwanyonya watu kwa mwamvuli wa dini.​

Rum 10:15 SUV​

Tena wahubirije, wasipopelekwa? Kama ilivyoandikwa, Ni mizuri kama nini miguu yao wahubirio habari ya mema!
SUV: Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia.🤝🏻🤝🏻🤝🏻

Avumilie dawa imuingie asijekuwa na sababu huko mbeleni
 
Mimi naziba masikio na kumwangalia mhubiri kwa dharau. Mwisho anaomba pesa ya maji kutuliza kiu, nimemtuma kupayuka?? Acheni kumpigia Mungu kelele!!!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ningejua ulipo ningekuhubiria hadi unavyoenda chooni, umekuwa mpinga Kristo
 
Back
Top Bottom