Msanii
Platinum Member
- Jul 4, 2007
- 26,483
- 40,130
Salaam ipo mwishoni
Kwa mtazamo wangu, maeneo ambayo JWTZ ya mijini wanayoona yapo pweke, wangejenga vituo vya mafunzo kwa umma na maabara za kiuchunguzi na utafiti kwa manufaa ya jamii.
Nimejiuliza maswali haya na nimekosa majibu, nimeona nishirikishane nanyi tuweze kuona athari zinazotujia coldly.
- Kambi ya jeshi Lugalo pale kona kwenda Kawe kuna shopping centre imejengwa kwa mfumo wa frames. Ndani ya Kambi eneo la mazoezi ya kimedani kwa wanajeshi wetu
- Lugalo pembezoni mwa shule ya Makongo uelekeo wa Mwenge kuna yard kubwa ya mjezi wa barabara imejengwa ndani ya Kambi
- Lugalo maeneo ya Mwenge Mlalakuwa kona ya kuelekea Efatha kuna bar na ukumbi wa starehe umejengwa just nyuma ya bango la MILITARY BASE
- Ngome SACCOS social hall hapo kambini upande wa Mlalakuwa.....
- Mbagala Kizuiani upande wa Zakhem, kuna kituo cha Mafuta kimejengwa ndani ya eneo la JWTZ.
- Mbagala Kizuiani, kuna yard ya malori imejengwa ndani ya kambi ya JWTZ eneo alilojenga yard ya ujenzi mkandarasi kutoka China.
Kwa mtazamo wangu, maeneo ambayo JWTZ ya mijini wanayoona yapo pweke, wangejenga vituo vya mafunzo kwa umma na maabara za kiuchunguzi na utafiti kwa manufaa ya jamii.
Nimejiuliza maswali haya na nimekosa majibu, nimeona nishirikishane nanyi tuweze kuona athari zinazotujia coldly.
- Nani anafaidika na hizi mbanga za uwekezaji kwenye makambi yetu ya JWTZ?
- Hazina ina rekodi vipi mapato ya uwekezaji huu?
- Lengo ni nini?