Huu uwekezaji kibiashara kwenye kambi zetu za JWTZ, nani kauruhusu?

Huu uwekezaji kibiashara kwenye kambi zetu za JWTZ, nani kauruhusu?

Sasa wewe unaona kutengeneza bunduki Ni technologia kubwa sana?

Hao JWTZ wakiwekewa budget wanatengeneza tu, Mbona hayo mambo madogo sna.

Mwal. Nyerere aliweza kuanzisha Viwanda vingi miaka ya 1967 ndo tushindwe leo 2025.

Siku Serikali ikiamua kwa dhati kabisa kutengeneza siraha kupitia JWTZ watatengeza tuu, ila sasa wataanzaje wakati wenye Tenda za kuagiza siraha kutoka mataifa ya Nje ni wao wenyewe?

Yaani mtengeneze hapa Tz kwa bei ndogo, watu wakose kupiga 20% kwenye uagizaji huko nje?

Mtalaumiana sana huku chini mpaka mtoane meno, huko juu ndo wanacho kipenda.
Bunduki ametoa tu kama mfano. Unaanza na bunduki, unakwenda katika mengine.
 
Ingetakiwa wapelekwe kutengene
Nataka nikujibu kwa kifupi sana.
Majeshi yote yana huu utaratibu toka zamani ila kwa nyuma kidogo walijikita zaidi kwenye Canteen (mabwalo) na duka moja au mawili kwa ajili ya ustawi na unafuu wa kambi zao.

Unafuu kwa maana ya bei ndogo za bidhaa ikiwemo vileo.
Baada ya kuja Mwanamalundi Junior alianzisha huu utaratibu wa majeshi kujitegemea kwa namna fulani.

Ndio maana leo hii karibu kila eneo la jeshi lolote kwa wale wenye maeneo mapana wanajenga ma business center makubwa na ndio yanayolipa
Majeshi hayatakaa yajitegemee, kwanza jeshi likiweza kujitegemea kiuchumi ni hatari hata kwa serikali yenyewe. Hiyo ni miradi ya kuneemesha watu wachache huko ndani na nje ya jeshi.
 
Kutoka Facebook kwenye account za JWTZ.
Na hizi ndizo comment za wananchi.

Screenshot_20260116_181716_Facebook.jpg
Screenshot_20260116_181740_Facebook.jpg
 
Kutoka Facebook kwenye account za JWTZ.
Na hizi ndizo comment za wananchi.

View attachment 3530659View attachment 3530660
CHADEMA mna akili za ajabu sana, mlitaka jeshi lifanye uasi kisa mnaongozwa na chuki na ubaguzi dhidi ya Rais mzenji!!.

Mpaka hivi sasa kuna biashara za watu zimekufa kabisa baada ya ule ushenzi wa October 29, yaani mlitaka Tanzania hii hii ya Mwalimu Nyerere ifanane na ile Somalia baada ya kifo cha Siad Baree wapuuzi kweli nyinyi.
 
CHADEMA mna akili za ajabu sana, mlitaka jeshi lifanye uasi kisa mnaongozwa na chuki na ubaguzi dhidi ya Rais mzenji!!.

Mpaka hivi sasa kuna biashara za watu zimekufa kabisa baada ya ule ushenzi wa October 29, yaani mlitaka Tanzania hii hii ya Mwalimu Nyerere ifanane na ile Somalia baada ya kifo cha Siad Baree wapuuzi kweli nyinyi.
Umekagua hao wote ukawakuta ni wanachama wa chadema?

Yule mtangazaji cloud fm alikuwa chadema

Huyu shekhe majini nae ni chadema?
Unadhani watoto wake kuna lugha mtaisema watawaelewa?

1768577825038.jpg
 
Nenda kamshauri Padre kitime namna ya kuimba taarabu kwenye mikutano ya waandishi wa habari huko unaweza kuwanufaisha zaidi.
 
SUMA JKT wana miradi mingi Sana
SACCOS
kampuni za usafi
Kampuni za fumigation
Kampuni za ulinzi
Kilimo, pembejeo na vifaa vinginevyo
Kampuni za ujenzi
Nknk
Nadhani wana mpango wa kufungua bank itakayojulikana kama SUMA MICRO FINANCE BANK
kirefu cha SUMA ni nini?!
 
Umekagua hao wote ukawakuta ni wanachama wa chadema?

Yule mtangazaji cloud fm alikuwa chadema

Huyu shekhe majini nae ni chadema?
Unadhani watoto wake kuna lugha mtaisema watawaelewa?

View attachment 3530687
Vita haina macho pole maalum kwa wote waliopoteza wapendwa wao katika ile siku nyeusi kuliko zote katika historia ya Tanzania.

Jiulize ni kwanini Mange na Maria walishindwa kuwashawishi watanzania waandamane mwezi wa 12 mwaka jana na tarehe moja January, waliyaona madhara makubwa ya machafuko ambayo chanzo chake ni CHADEMA na siasa za 'kukinukisha'.
 
Kuna member aliwai kuleta hili jambo hapa lakini si unajua tena kenge hasikii mpaka atoe damu masikioni
 
Salaam ipo mwishoni
  1. Kambi ya jeshi Lugalo pale kona kwenda Kawe kuna shopping centre imejengwa kwa mfumo wa frames. Ndani ya Kambi eneo la mazoezi ya kimedani kwa wanajeshi wetu
  2. Lugalo pembezoni mwa shule ya Makongo uelekeo wa Mwenge kuna yard kubwa ya mjezi wa barabara imejengwa ndani ya Kambi
  3. Lugalo maeneo ya Mwenge Mlalakuwa kona ya kuelekea Efatha kuna bar na ukumbi wa starehe umejengwa just nyuma ya bango la MILITARY BASE
  4. Ngome SACCOS social hall hapo kambini upande wa Mlalakuwa.....
  5. Mbagala Kizuiani upande wa Zakhem, kuna kituo cha Mafuta kimejengwa ndani ya eneo la JWTZ.
  6. Mbagala Kizuiani, kuna yard ya malori imejengwa ndani ya kambi ya JWTZ eneo alilojenga yard ya ujenzi mkandarasi kutoka China.
Hapo nimetaja kwa uchache. Ukiangalia makambi ya JWTZ yaliyopo mijini yamegeuzwa kuwa ya kibiashara, zipo kauli kwamba Waarabu webinafsishwa maeneo hayo ndo maana hata vituo vya mafuta vinajengwa humo bila kujali athari zake kiulinzi.

Kwa mtazamo wangu, maeneo ambayo JWTZ ya mijini wanayoona yapo pweke, wangejenga vituo vya mafunzo kwa umma na maabara za kiuchunguzi na utafiti kwa manufaa ya jamii.

Nimejiuliza maswali haya na nimekosa majibu, nimeona nishirikishane nanyi tuweze kuona athari zinazotujia coldly.
  1. Nani anafaidika na hizi mbanga za uwekezaji kwenye makambi yetu ya JWTZ?
  2. Hazina ina rekodi vipi mapato ya uwekezaji huu?
  3. Lengo ni nini?
Salaam za upendo kwenu nyote wema na wabaya
Hakuna Jeshi hapo siku hizi.

Ni MILITIA ya wahuni kina Rostam Aziz.

Hakuna Jeshi timamu limewahi muwageuzia silaha za kivita raia wake.
 
Vita haina macho pole maalum kwa wote waliopoteza wapendwa wao katika ile siku nyeusi kuliko zote katika historia ya Tanzania.

Jiulize ni kwanini Mange na Maria walishindwa kuwashawishi watanzania waandamane mwezi wa 12 mwaka jana na tarehe moja January, waliyaona madhara makubwa ya machafuko ambayo chanzo chake ni CHADEMA na siasa za 'kukinukisha'.
Kama chadema ndo waliandamana kwa wingi vile basi ccm hamna ushawishi tena
 
Huwa nawaona hawana maana wanapostaafu wanasifiwa kwa utumishi uliotukuka, huku hawajahi hata kupigana vita zaidi ya kwenda kupiga parade. Cha ajabu hata wao wakisikia maneno hayo wanachekelea!
Walitakiwa wawe na akiba ya kiu ya wito

Sawa, wao ni wanajeshi kipaumbele cha wanyonge kwenye Kujitoa mhanga, wala hatukatai.!

Lakini unapoishi na kumaliza muhula pasi na wito wa nia yako kutekelezwa, wewe ni kituko

Ndio maana inapozaliwa akiba ya wito, na vile wasivyo na haya wanaserereka nayo

Walitakiwa wahitimu pasi na utambulisho na ingefaa zaidi
 
SUMA JKT wana miradi mingi Sana
SACCOS
kampuni za usafi
Kampuni za fumigation
Kampuni za ulinzi
Kilimo, pembejeo na vifaa vinginevyo
Kampuni za ujenzi
Nknk
Nadhani wana mpango wa kufungua bank itakayojulikana kama SUMA MICRO FINANCE BANK
Hiyo benki itajiendesha kwa hasara. Wakomae na fremu na kokoto tu.
 
Back
Top Bottom