Huu uzi ni maalumu kwa ajili ya kujadili uwekezaji ambao ni rafiki kwa Waajiriwa

Huna mda wa kusimamia achana kabisa na biashara ni Bora uishi kwa kipato hicho hicho kwa amani kuliko kulipia mkopo wa maumivu ya hela iliyopotea
Mkuu mimi nilifungua biashara,kwanza mtaji ulienda,gharama za uendeshaji zilikuwa zinatoka kwenye mshahara,kiufupi mimi ndio nilikuwa nahudumia ile biashara.
 
Mkuu mimi nilifungua biashara,kwanza mtaji ulienda,gharama za uendeshaji zilikuwa zinatoka kwenye mshahara,kiufupi mimi ndio nilikuwa nahudumia ile biashara.
Wasimamizi wanajelous sana na watu wa mshahara wanaamini wanapesa sana so lazima wakupige
 
Sasa mkuu tupeane mawazo,mishahara haitoshi,tunatokaje hapa tulipo?
Nimeona wadau wengi wanaongelea sana UTT,wengine nyumba za kupangisha na viwanja,wengine ufugaji...Je hizo ni sehemu sahihi kuweka hela zetu?
Sio kwamba biashara hautoboi shida ni mswahili chukua ndugu rafiki yako mpe asimamie mtoke wote jibu utalipata angalau wakinga,wachaga wapemba wana heshimu vya ndugu zao atakula lakini nawe utainuka.
Shida ni wanakula yote at the end wanabakia kuwa masikini.
Weka UTT,nyumba za biashara, umeshindwa nunua shamba au kiwanja utavulimia kesho ukikata vipande utaishi vizuri
 
chagueni moja utumishi wa uma au biashara acheni kuwaibia muda waajiri wenu,kwakufuatilia miradi yenu mkishawekeza
 
Sasa mkuu tupeane mawazo,mishahara haitoshi,tunatokaje hapa tulipo?
Nimeona wadau wengi wanaongelea sana UTT,wengine nyumba za kupangisha na viwanja,wengine ufugaji...Je hizo ni sehemu sahihi kuweka hela zetu?
bado huelewi tu watu wametoa mawazo hati page ya 7 sasa, jibu iliyonyooka anzisha biashara acha ajira kasimamie biashara yako
 
bado huelewi tu watu wametoa mawazo hati page ya 7 sasa, jibu iliyonyooka anzisha biashara acha ajira kasimamie biashara yako
mkuu unaona ni wazo zuri mtu aache ajira yake,chanzo cha uhakika cha mapato aende kubangaiza sehemu mbayo haina uhakika? Tunahitaji vyanzo vya ziada vya mapato sio kupoteza kidogo tulichonacho.
 
chagueni moja utumishi wa uma au biashara acheni kuwaibia muda waajiri wenu,kwakufuatilia miradi yenu mkishawekeza
Mkuu hakuna mtu anamuibia mwajiri muda,tuna haki ya muda wetu wa ziada,Nadhani unachanganya biashara na uwekezaji,mpaka sasa Biashara inaonekana ni mwiba mchungu kwetu,mawazo tunahitaji hapa ni ya uwekezaji.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…