Huu uzi ni maalumu kwa ajili ya kujadili uwekezaji ambao ni rafiki kwa Waajiriwa

Huu uzi ni maalumu kwa ajili ya kujadili uwekezaji ambao ni rafiki kwa Waajiriwa

Huna mda wa kusimamia achana kabisa na biashara ni Bora uishi kwa kipato hicho hicho kwa amani kuliko kulipia mkopo wa maumivu ya hela iliyopotea
Mkuu mimi nilifungua biashara,kwanza mtaji ulienda,gharama za uendeshaji zilikuwa zinatoka kwenye mshahara,kiufupi mimi ndio nilikuwa nahudumia ile biashara.
 
Sasa mkuu tupeane mawazo,mishahara haitoshi,tunatokaje hapa tulipo?
Nimeona wadau wengi wanaongelea sana UTT,wengine nyumba za kupangisha na viwanja,wengine ufugaji...Je hizo ni sehemu sahihi kuweka hela zetu?
Sio kwamba biashara hautoboi shida ni mswahili chukua ndugu rafiki yako mpe asimamie mtoke wote jibu utalipata angalau wakinga,wachaga wapemba wana heshimu vya ndugu zao atakula lakini nawe utainuka.
Shida ni wanakula yote at the end wanabakia kuwa masikini.
Weka UTT,nyumba za biashara, umeshindwa nunua shamba au kiwanja utavulimia kesho ukikata vipande utaishi vizuri
 
Maisha ya utumishi ni mafupi hivyo ni heri kujiandaa na maisha ya kustaafu mapema.

Kipato vya wafanyakazi wengi ni kidogo sana hivyo kuna ulazima kuwa na kipato cha ziada.

Changamoto ya wafanyakazi wengi ni muda wa kufanya biashara na projects kama kilimo na ufugaji haupo na risk ya kupoteza hela zako ni kubwa kuliko kupata faida sababu ya usimamizi duni.

Huu uzi ni maalumu kwa ajili ya kujadili uwekezaji ambao ni rafiki kwa mfanyakazi, hauhitaji muda mwingi,risk ya kupoteza pesa sio kubwa na wenye faida ya kueleweka.

Naongelea vitu kama UTT, treasury bills na Bonds, Hisa kwenye makampuni ya kitaifa na kimataifa na fursa nyingine nyingi na nzuri ambazo mfanyakazi anaweza kujiingiza ili kutunza na kuongeza kipato chake.

Nafahamu humu ndani kuna wataalamu wa mambo ya uchumi na uwekezaji, kuna wawekezaji wakubwa na wadogo, kuna matajiri wa kutosha, njooni mtushike mkono tujue namna gani tunaweza kukuza vipato vyetu vidogo na kuingia kwenye utajiri.
Karibuni.
chagueni moja utumishi wa uma au biashara acheni kuwaibia muda waajiri wenu,kwakufuatilia miradi yenu mkishawekeza
 
Sasa mkuu tupeane mawazo,mishahara haitoshi,tunatokaje hapa tulipo?
Nimeona wadau wengi wanaongelea sana UTT,wengine nyumba za kupangisha na viwanja,wengine ufugaji...Je hizo ni sehemu sahihi kuweka hela zetu?
bado huelewi tu watu wametoa mawazo hati page ya 7 sasa, jibu iliyonyooka anzisha biashara acha ajira kasimamie biashara yako
 
bado huelewi tu watu wametoa mawazo hati page ya 7 sasa, jibu iliyonyooka anzisha biashara acha ajira kasimamie biashara yako
mkuu unaona ni wazo zuri mtu aache ajira yake,chanzo cha uhakika cha mapato aende kubangaiza sehemu mbayo haina uhakika? Tunahitaji vyanzo vya ziada vya mapato sio kupoteza kidogo tulichonacho.
 
chagueni moja utumishi wa uma au biashara acheni kuwaibia muda waajiri wenu,kwakufuatilia miradi yenu mkishawekeza
Mkuu hakuna mtu anamuibia mwajiri muda,tuna haki ya muda wetu wa ziada,Nadhani unachanganya biashara na uwekezaji,mpaka sasa Biashara inaonekana ni mwiba mchungu kwetu,mawazo tunahitaji hapa ni ya uwekezaji.
 
Back
Top Bottom