Asant utajibiwa na mwehu mwenzioSasa aliyemtuma huyo baba yenu atembee na hao wanawake "wanaovizia wastaafu" ni nani
Nani huyo kawapiga??Oya hapo kwenye kilometer 40 umetupiga kamba, kilo mita arobain ni chache sana unaenda na kurudi labda ungesema kilometer 100, naweza kuamini ,
Sent using Jamii Forums mobile app
Huenda siyo baba yako mzazi. ChunguzaAngekuwa baba yangu hapo nisingekuwa shule muda huo. Kuna watu wengi wenye umuhimu kwangu kumzidi yeye, mtu anayekwambia mbona unanipigia sana kwani sijui kama upo unategemea maajabu gani kwake. Hapo ushamtafuta mwaka mzima hapokei sasa jichanganye umpigie kwa namba nyingine apokee atabadili gia angani kama hivi;
Mimi: Inaita
Yeye: Anapokea
Mimi: (Salamu na maelezo kwa mkupuo maana najua hatoongea sana, hela hazihusiki kabisa)
Yeye: Kumbe ni wewe, mbona namba nyingi. Simu yangu hii ina shida
Mimi: Siku nyingi hatuongei kulikoni
Yeye: Hello! mbona sikusikii
Mimi: Wazima uko
Yeye: Hello! Hello! Naona mtandao una shida, sikusikii ntakupigia nikikaa kwenye network.
Kuna siku usanii wake nikauchoka nikamtukana we mpuuzi nini kila siku mtandao unasumbua. Kesi nikaisikia kwa aunt yangu ikiwa na nyongeza ya mashtaka kwamba simpendi na natamani afe. Kazi yake kwangu ni kunifanya nisiitwe yatima, hafai hata kunipa ushauri.
Pole mkuu kazi kweli kweli! Kuna kijana jingine huku nahangaika nalo, Dunia hii kuna mababa hayana akili kabisa, kijana limemfukuza mke na watoto wanne eti linataka libaki peke yake kwenye nyumba lioe mke mwingine. Limesahau kama hiyo nyumba hata mke alichangia! Sasa mama na watoto wanahangaika kutafuta nyumba ya kupanga! Kijana ameapa hatakuja amsamehe babake na amesema kabisa yaani huyu baba ni takataka kabisa kwangu! Sasa kijana wa hivi atampenda babake saa ngapi?My father is not my role model and he will never haijalishi, alishauwa legacy yake tangu nikiwa mdogo he got no respect in our family.
Last time he kicked me out of house and we have never hold any conversation over a couple of years.
Key word: MAZAO YALIYOLIMWA NA BABA; still jamaa yako ANAJIMWAMBAFAI kuwa kasomeshwa na mama yake-hakika kuna shida mahala.Kuna jamaa ananipaga story kuhusu kusomeshwa na mama yake kuanzia school hadi chuo.
Anampa sifa zooote mama huku kazi yake mama ilikuwa kuuza mazao yaliyolimwa baba.
BABA YAKE HANAGA MAKUU ANAMUANGALIA TU NA KUMWAMBIA MAADAMU HUU MWANAUME INAPENDEZA.
Wewe nouma hongera kwa ujasiri wa upendo. Barikiwa sanaAngekuwa baba yangu hapo nisingekuwa shule muda huo. Kuna watu wengi wenye umuhimu kwangu kumzidi yeye, mtu anayekwambia mbona unanipigia sana kwani sijui kama upo unategemea maajabu gani kwake. Hapo ushamtafuta mwaka mzima hapokei sasa jichanganye umpigie kwa namba nyingine apokee atabadili gia angani kama hivi;
Mimi: Inaita
Yeye: Anapokea
Mimi: (Salamu na maelezo kwa mkupuo maana najua hatoongea sana, hela hazihusiki kabisa)
Yeye: Kumbe ni wewe, mbona namba nyingi. Simu yangu hii ina shida
Mimi: Siku nyingi hatuongei kulikoni
Yeye: Hello! mbona sikusikii
Mimi: Wazima uko
Yeye: Hello! Hello! Naona mtandao una shida, sikusikii ntakupigia nikikaa kwenye network.
Kuna siku usanii wake nikauchoka nikamtukana we mpuuzi nini kila siku mtandao unasumbua. Kesi nikaisikia kwa aunt yangu ikiwa na nyongeza ya mashtaka kwamba simpendi na natamani afe. Kazi yake kwangu ni kunifanya nisiitwe yatima, hafai hata kunipa ushauri.
Nimekuwa mkubwa ili bado naamini mzee alizingua pakubwa sana.Ukiwa mkubwa ndipo unapojua kwanini mzee alifanya baadhi ya maamuzi.
SIO WAMAMA WA THIS GENERATION WA HAKI SAWA KWA WOTE.Shukuru Mungu kama Ulizaliwa na baba wa aina hiyo! Siyo watoto wote wana historia kama hizo na baba zao!
Sidhani kama kuna mtu anayemchukia baba yake bila sababu! Ukikuta mtu anamchukia baba yake tafuta kujua chanzo!
Na mara nyingi mtoto akimchukia baba yake lawama zote hutupiwa mama! Wamama wengi wana wakati mgumu sana!
Naomba actual name ya huyo mkongwe pm, kama hautojali tafadhali.Wakati fulani nikisoma shule ya Sekondari, baba alikuja kunitembelea shuleni, nikashangaa kwa nini amekuja kwa miguu na ana mavumbi mengi miguuni?
Akanikabidhi TZS 12,000/= yani 10,000/= ya kulipia hostel na 2,000/= ya matumizi. Nikamuuliza mbona leo huna baiskeli? (mara zote alikuwa akiendesha baiskeli 40kms kuja shuleni). Akanijibu "...nimekuja kwa basi", nikaamini ni kweli!
_
Miaka mitano baadaye, nikiwa Chuo Kikuu, wakati nimerudi likizo nyumbani, nikawa nimekaa nje saa za usiku mnene, niko na baba akinipigia stori za vita za Uganda, Msumbiji nk.
Ghafla akanipigia stori iliyomkuta miaka 5 iliyopita, kwamba alikuwa na shilingi 12,000 tu ndani, akapata taarifa kuwa wanafunzi wanarudishwa kwa kutolipa hela za hostel. Akafunga safari ya baiskeli kuja shuleni kwetu (alikuwa anaanza safari zake saa 8 au 9 usiku), ili kuniletea ile pesa, safari ya kilomita 40.
Alipofika kilomita 13 baiskeli ikaharibika, "tyre tube" ya nyuma ikapasuka, ikawa haifai. Akaamua kuacha baiskeli kwa wenyeji na kuanza safari ya saa nyingi kwa mguu hadi shuleni kwetu, zaidi ya kilomita 27.
Akafika ametabasamu ana furaha mno, akanikabidhi zile pesa na akaanza safari nyingine ya kilomita 27 + 13, ananiambia alifika nyumbani kesho yake.
Usiku nilipojua safari ile ya Mzee wangu nililia sana, sikulala, ilinipasa nijitafakari juu ya huyu mtu anayeitwa BABA, ambaye yuko tayari kufa na kutokwa jasho la damu kwa ajili ya familia yake.
_
Kila mwanaume 1 anaporudi nyumbani, anaenda kuipa matumaini, familia yake, hata kama hana senti tano! Uwepo wake na tabasamu na kurudi kwake, kunainong'oneza familia "IPO KESHO....KUNA MAISHA BADO....TUNA ULINZI WA KUTOSHA. BADO LIPO TUMAINI.."
_
Hadithi ya baba yangu mzazi, inatukumbusha mwanaume anatembea na mengi sana kichwani na moyo wake, na hawezi kuyasema, kama wanaume wangelikuwa wanawaeleza wake zao namna wanavyopambana kwa ajili ya familia zao, wanawake wangelikufa kwa mshtuko.
And you know what? Baba hakuwahi kumpigia mama hii stori, hadi mimi nilipomsimulia mama.
Si ajabu ndiyo maana wanaume tunakufa mapema, maana tunauawa na mengi!
Ndivyo mama yako alivyokuaminisha.Mimi baba yangu naona ni kama vile sperm donor tuu hana tofauti na hilo.
Endelea kujikaririsha mkuuSIO WAMAMA WA THIS GENERATION WA HAKI SAWA KWA WOTE.
Dah!,pole sana,kuna wazee wa hvyoAngekuwa niwangu hilo la stendi ningetembea kutoka kayenze mpaka nyegezi kwa miguu bila hata kujua kama nimefika salama.
Kwenye wod hata hangekuja kabisa kuniona mpaka niruhusiwe kisha mi nikamsalimie senta anacheza bao. Inamaana hata ile ya mwanangu aliyekuwa anaumwa kaja niende nyumbani tukaonane isingekuwepo. I HATE MY DAD
Sio kila chuki ya mtoto kwa baba inakuwa planted na mama, shida ni kwamba mtoto anavyokuwa mdogo na mpaka utu uzima ndo anakuja kutambua aina wa wazazi alio nao, mzazi(baba) anaweza akawa hana kipato kizuri lakini akawa very responsible na familia yake kuliko yule ambaye mungu kaampa mali na uchumi ulio bora lakini hajali watoto wake anamuachia mama yao aangaike kwa maisha ya kuunga unga huku watoto wanajua baba yao ni nani na ana nafasi gani kwenye jamii .hao watoto kamwe hawawezi mpenda baba yao ndo hao type ya sparm doner.
Baba analima ndiz mama anaenda kuuza na kupata mtaji kidogo wa kuuza maandaz.Key word: MAZAO YALIYOLIMWA NA BABA; still jamaa yako ANAJIMWAMBAFAI kuwa kasomeshwa na mama yake-hakika kuna shida mahala.
Huwa zipo sababu zinazopelekea hayo. Ningekushauri ufanye utafiti. Ukiishia kupata story kutoka upande mmoja huenda ukawa unakosea sana.Sio kila chuki ya mtoto kwa baba inakuwa planted na mama, shida ni kwamba mtoto anavyokuwa mdogo na mpaka utu uzima ndo anakuja kutambua aina wa wazazi alio nao, mzazi(baba) anaweza akawa hana kipato kizuri lakini akawa very responsible na familia yake kuliko yule ambaye mungu kaampa mali na uchumi ulio bora lakini hajali watoto wake anamuachia mama yao aangaike kwa maisha ya kuunga unga huku watoto wanajua baba yao ni nani na ana nafasi gani kwenye jamii .hao watoto kamwe hawawezi mpenda baba yao ndo hao type ya sparm doner.