Huwa kila siku natafakari umuhimu wa Baba katika maisha ya kila Familia

Huwa kila siku natafakari umuhimu wa Baba katika maisha ya kila Familia

Nna shangaa Sana Sasa hivi sifa zote anapewa mwanamke, Baba kasahaulika! Mama yangu mzazi alifariki nikiwa km na 3yrs unfortunately siijui hata saiti yake na Sina kumbukumbu yoyote na Mama yangu mpenzi lkn nnaona picha zake na sisi tulipokuwa wadogo! MUNGU ailaze roho yake mahala pema peponi Amina! Baba alioa tena Mama yetu mlezi alitulea vizuri tuu hakuwa shida maana tayari tulikuwa watano na yeye akapata watoto wawili.

Baba alikuwa akifanya kazi serikalini na alikuwa na wadhifa kimkoa. Ukisikia Baba wale wa enzi za mwalimu Sasa yeye ndo alikuwa mmoja wao. Yaani strict to the rules hakupindisha maneno, akisema A ni A. Kwa kweli baba alikuwa ndio nguzo yangu! Rip baba alijitoa zaidi ya 100% tusome na kuhakikisha tunakuwa na maadili na nidhamu. Hakubagua Mtoto! Alinifundisha kufanya kazi kwa bidii kujituma na ucha MUNGU! alikuwa kila jpili hakosi kanisani na nyumbani habaki mtu, wote church!

Alihimiza Sana kupendana na kuwa kitu kimoja. Nikiwa na 5yrs Kuna siku walipishana maneno na huyu Mama yetu mlezi, walizozana kidogo siku ikaisha, kesho yake kukawa shwari. Mpaka wote wamefariki sikuwasikia Tena wakigombana, wala mmoja kanuna sijui haongei na mwenzie.

Yaani wakitoka room km hakuna kitu, maneno nayakuja kuyapata kwa dad's yangu mkubwa, atakwambia unajua kwa Nini shangazi alikuja mwezi wa tatu? Sijui utasikia ohooo alikuja suluhisha ugomvi Mama anataka mwanae wa kike wa kwanza apatiwe ile nyumba yetu kubwa! Khaaaa ndo naajua kumbe Kuna issue hahahaa. Baba will always be my hero! Ingawa ma mlezi kwa kweli ametulea Kama watoto wake, alifariki bado nipo chuo lkn Kama angekuwepo leo hii ningemzawadia nyumba mpyaa.

Alikaa na sisi tukiwa wadogo, nakumbuka Kuna siku nilibanwa na asthma usiku saa nane alinibeba mpaka zahanati nikatibiwa alikuwa akinipendanoo. Akipika mie ndo mwonja chumvi, chumbani kwa baba na Mama mie peke yangu ndo nilikuwa naweza tumwa hukoo! Sasa hivi nnatamani angekuwepo nimwoneshe appreciation yangu kwake!
Duh uchungu sana umenipa jamani 😢
 
Mzee Abdul aliuza mpaka Redio yake ili akamlipie Mama Diamond hospital ila Leo Kaambiwa mtoto sio wake ni wa anko shamte [emoji20][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Mzee Abdul aliuza mpaka Redio yake ili akamlipie Mama Diamond hospital ila Leo Kaambiwa mtoto sio wake ni wa anko shamte [emoji20][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
[emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3]
 
Uko sahihi mm ninawatoto wakubwa wanne,mkubwa kabisa wa kiume ana 29 yrs huyo hana time na Mimi ila anaemfuatia wakike ana 26yrs huyo ananipenda Sana baba yake
Dah! Shikamoo! Nina umri sawa na mtoto wako. Ndio maana mimi huwa situkani mtu au kujibu hovyo hapa JF. Huwezi jua kumbe unatukana mtu sawa na babako.
 
Wakati fulani nikisoma shule ya Sekondari, baba alikuja kunitembelea shuleni, nikashangaa kwa nini amekuja kwa miguu na ana mavumbi mengi miguuni?

Akanikabidhi TZS 12,000/= yani 10,000/= ya kulipia hostel na 2,000/= ya matumizi. Nikamuuliza mbona leo huna baiskeli? (mara zote alikuwa akiendesha baiskeli 40kms kuja shuleni). Akanijibu "...nimekuja kwa basi", nikaamini ni kweli!
_
Miaka mitano baadaye, nikiwa Chuo Kikuu, wakati nimerudi likizo nyumbani, nikawa nimekaa nje saa za usiku mnene, niko na baba akinipigia stori za vita za Uganda, Msumbiji nk.

Ghafla akanipigia stori iliyomkuta miaka 5 iliyopita, kwamba alikuwa na shilingi 12,000 tu ndani, akapata taarifa kuwa wanafunzi wanarudishwa kwa kutolipa hela za hostel. Akafunga safari ya baiskeli kuja shuleni kwetu (alikuwa anaanza safari zake saa 8 au 9 usiku), ili kuniletea ile pesa, safari ya kilomita 40.

Alipofika kilomita 13 baiskeli ikaharibika, "tyre tube" ya nyuma ikapasuka, ikawa haifai. Akaamua kuacha baiskeli kwa wenyeji na kuanza safari ya saa nyingi kwa mguu hadi shuleni kwetu, zaidi ya kilomita 27.

Akafika ametabasamu ana furaha mno, akanikabidhi zile pesa na akaanza safari nyingine ya kilomita 27 + 13, ananiambia alifika nyumbani kesho yake.

Usiku nilipojua safari ile ya Mzee wangu nililia sana, sikulala, ilinipasa nijitafakari juu ya huyu mtu anayeitwa BABA, ambaye yuko tayari kufa na kutokwa jasho la damu kwa ajili ya familia yake.
_
Kila mwanaume 1 anaporudi nyumbani, anaenda kuipa matumaini, familia yake, hata kama hana senti tano! Uwepo wake na tabasamu na kurudi kwake, kunainong'oneza familia "IPO KESHO....KUNA MAISHA BADO....TUNA ULINZI WA KUTOSHA. BADO LIPO TUMAINI.."
_
Hadithi ya baba yangu mzazi, inatukumbusha mwanaume anatembea na mengi sana kichwani na moyo wake, na hawezi kuyasema, kama wanaume wangelikuwa wanawaeleza wake zao namna wanavyopambana kwa ajili ya familia zao, wanawake wangelikufa kwa mshtuko.

And you know what? Baba hakuwahi kumpigia mama hii stori, hadi mimi nilipomsimulia mama.

Si ajabu ndiyo maana wanaume tunakufa mapema, maana tunauawa na mengi!
Wapo wanao wathamini baba zao, lakini wengi hawajui thamani ya baba. Watoto wengi kuzaliwa kwao ni juhudi za baba kukataa wazo la mama kutoa mimba. Hata hizo mimba wakati mwingine ni juhudi ya baba baada ya chenga nyingi za mama. Lakini mwisho wa siku baba huwa ni daraja, ukisha vuka hugeuki nyuma.
 
Baba ataheshiwa akijua Sababu yake kuwa duniani ambayo ni kula kwa jasho lake, baba anatakiwa apambanie heshima hiyo na Kila mtu atamheshimu automatic, ila tatizo la kushikiwa akili na wanawake kwa kutengenezewa utamu uwe wa asili au wakufoji kumevuruga heshima ya wengi.
 
Mama yangu aliaga dunia miaka kadhaa kwa presha..ugonjwa huo wa moyo ukiangalia kwa makin baba ndio sababu.....simchukii baba namwambiaga nampenda sana....cha ajabu yeye analiaga sana anapokumbuka matendoyaliyochangia mauti....huwa tunamwambia baba sio kosa lako ni wanawake wanaovia wanaostaaffu, kuwarubini na kula pensheni ambapo mke aliyemfulia nguo ameingia mavumbini....wazee wetu wanastahili mapenzi

Mnappiga hizi stor anzeni kwa nje
Sasa aliyemtuma huyo baba yenu atembee na hao wanawake "wanaovizia wastaafu" ni nani
 
.
My father is not my role model and he will never haijalishi, alishauwa legacy yake tangu nikiwa mdogo he got no respect in our family.
Last time he kicked me out of house and we have never hold any conversation over a couple of years.
Pole sana, msameheni baba yenu kwa afya ya maisha yenu.
 
Shukuru Mungu kama Ulizaliwa na baba wa aina hiyo! Siyo watoto wote wana historia kama hizo na baba zao!

Sidhani kama kuna mtu anayemchukia baba yake bila sababu! Ukikuta mtu anamchukia baba yake tafuta kujua chanzo!

Na mara nyingi mtoto akimchukia baba yake lawama zote hutupiwa mama! Wamama wengi wana wakati mgumu sana!
Wakati mwengine wakina mama wanahusika sana kupandikiza chuki kwa mtoto hata kama tofauti ni za kwao wazazi, unakuta mtoto anamchukia baba kwa yale anayoyasikia kwa mama hata kama hayana ukweli
 
Tuzidi kuwapenda waume zetu na tuwafundishe watt thamani ya baba zao..Nilikua nampenda sana baba yangu alinikaa mdomoni mpk kuna muda namuita mam baba.
 
Exactly the same story .
Mshua wangu alitengana na bimkubwa kitambo sana Kabla ya kuzaliwa kwangu. Kusoma kwangu,kula na kuvaa ni mama mpaka nimemaliza chuo.kiukweli huwa najiuliza hata kama walitofautiana na mama basi angenionyesha ule upendo basi kama baba yangu lakini wapi .hali hiyo ya kukosa upendo wa baba imeniathiri kisaikolojia hadi sasa . Najiuliza kwanini asingenionyesha upendo hata basi wa kinafiki. Kwa kweli nikikumbuka maisha haya niliyoyapitia nasema anyway ...

Kuna mengi sana yamejificha na Mzee au Mama hawezi kukwambia....kama wewe ni wa kiume ukikua unaweza kujifunza kitu...Usimchukie huyo Baba yako muombee kwa Mungu na Omba sana siku utajua ukweli na utajua shida ilikuwa wapi...ni mitihani sana....(kipo kisa cha binti aliyeachika siku chache baada ya ndoa tena akiwa mna mzito, nikiiangalia picha inavyooenda wasiojua wanaweza kumhukumu mwanaume kulingana na maelezo ya huyu dada lakini ipo siri ambayo naona haizungumzwi na binti wala jamaa ambayo ni ujinga wa binti, hapo kiumbe kikizaliwa kikikua kinaweza kuwa na chuki kwa jamaa lakini ukweli mama anaujua..)
 
Dah! Shikamoo! Nina umri sawa na mtoto wako. Ndio maana mimi huwa situkani mtu au kujibu hovyo hapa JF. Huwezi jua kumbe unatukana mtu sawa na babako.
Tunashauriwa kuheshimu kila mtu ndg yangu
 
Wapo wanao wathamini baba zao, lakini wengi hawajui thamani ya baba. Watoto wengi kuzaliwa kwao ni juhudi za baba kukataa wazo la mama kutoa mimba. Hata hizo mimba wakati mwingine ni juhudi ya baba baada ya chenga nyingi za mama. Lakini mwisho wa siku baba huwa ni daraja, ukisha vuka hugeuki nyuma.
Kweli aisee
 
Niliwah lala stendi nyegezi na baba angu ili kesho yake alfajir niende chuo na nilkuwa mkubwa tu lakin alipenda nisindikiza ile usiku nilkuwa namuwazia sana,kwann huyu mzee anateseka hv kwa ajiri yangu.

Niliwah lazwa hospital siku 4,sku zote alilala kwenye kiti pemben mwa kitanda changu,nikawa najiuliza mbona hawabadilishan na yeye akapumzika akalala nyumban,maana nyumban kulkuwa na ndugu wengine ambao wangeweza kuniangalia ili kumsaidia
Angekuwa niwangu hilo la stendi ningetembea kutoka kayenze mpaka nyegezi kwa miguu bila hata kujua kama nimefika salama.

Kwenye wod hata hangekuja kabisa kuniona mpaka niruhusiwe kisha mi nikamsalimie senta anacheza bao. Inamaana hata ile ya mwanangu aliyekuwa anaumwa kaja niende nyumbani tukaonane isingekuwepo. I HATE MY DAD
 
Kuna jamaa ananipaga story kuhusu kusomeshwa na mama yake kuanzia school hadi chuo.

Anampa sifa zooote mama huku kazi yake mama ilikuwa kuuza mazao yaliyolimwa baba.

BABA YAKE HANAGA MAKUU ANAMUANGALIA TU NA KUMWAMBIA MAADAMU HUU MWANAUME INAPENDEZA.
 
  • Kicheko
Reactions: BRB
Wakati fulani nikisoma shule ya Sekondari, baba alikuja kunitembelea shuleni, nikashangaa kwa nini amekuja kwa miguu na ana mavumbi mengi miguuni?

Akanikabidhi TZS 12,000/= yani 10,000/= ya kulipia hostel na 2,000/= ya matumizi. Nikamuuliza mbona leo huna baiskeli? (mara zote alikuwa akiendesha baiskeli 40kms kuja shuleni). Akanijibu "...nimekuja kwa basi", nikaamini ni kweli!
_
Miaka mitano baadaye, nikiwa Chuo Kikuu, wakati nimerudi likizo nyumbani, nikawa nimekaa nje saa za usiku mnene, niko na baba akinipigia stori za vita za Uganda, Msumbiji nk.

Ghafla akanipigia stori iliyomkuta miaka 5 iliyopita, kwamba alikuwa na shilingi 12,000 tu ndani, akapata taarifa kuwa wanafunzi wanarudishwa kwa kutolipa hela za hostel. Akafunga safari ya baiskeli kuja shuleni kwetu (alikuwa anaanza safari zake saa 8 au 9 usiku), ili kuniletea ile pesa, safari ya kilomita 40.

Alipofika kilomita 13 baiskeli ikaharibika, "tyre tube" ya nyuma ikapasuka, ikawa haifai. Akaamua kuacha baiskeli kwa wenyeji na kuanza safari ya saa nyingi kwa mguu hadi shuleni kwetu, zaidi ya kilomita 27.

Akafika ametabasamu ana furaha mno, akanikabidhi zile pesa na akaanza safari nyingine ya kilomita 27 + 13, ananiambia alifika nyumbani kesho yake.

Usiku nilipojua safari ile ya Mzee wangu nililia sana, sikulala, ilinipasa nijitafakari juu ya huyu mtu anayeitwa BABA, ambaye yuko tayari kufa na kutokwa jasho la damu kwa ajili ya familia yake.
_
Kila mwanaume 1 anaporudi nyumbani, anaenda kuipa matumaini, familia yake, hata kama hana senti tano! Uwepo wake na tabasamu na kurudi kwake, kunainong'oneza familia "IPO KESHO....KUNA MAISHA BADO....TUNA ULINZI WA KUTOSHA. BADO LIPO TUMAINI.."
_
Hadithi ya baba yangu mzazi, inatukumbusha mwanaume anatembea na mengi sana kichwani na moyo wake, na hawezi kuyasema, kama wanaume wangelikuwa wanawaeleza wake zao namna wanavyopambana kwa ajili ya familia zao, wanawake wangelikufa kwa mshtuko.

And you know what? Baba hakuwahi kumpigia mama hii stori, hadi mimi nilipomsimulia mama.

Si ajabu ndiyo maana wanaume tunakufa mapema, maana tunauawa na mengi!
Basi tu mengine tumwachie mungu
 
Back
Top Bottom