Huwa mnadili vipi na ndugu wa aina hii?

Huwa mnadili vipi na ndugu wa aina hii?

Za jumapili wakuu moja kwa moja kwenye mada, hivi huwa mnadili vipi na ndugu wa namna hii yeye akikutafuta ni kukuomba hela tu,, na hakuna chochote anachokusaidia kwenye maisha yako.

Ni dada yangu mtoto wa mama angu mkubwa, kuna kipindi waliuza eneo lao kama milioni 30 hivi, wakapewa mamilioni yao na mama yao, sikuwa napigiwa simu nilitumiwaga elf30 tu, na kipindi hicho nilikuwa nahihitaji support ya pesa ya ada ila walijikausha, wakaenda kununua eneo huko maporini hatimaye kumewashinda huko wamerudi huku Dar wamepanga.

Ndiyo huyu dada sasa ni mara nyingi sana ananitumiaga meseji za mara nimkopeshe hela mara nimsaidie mimi, anadhani nimesahau walichonifanyia, naombeni ushauri wenu huwa mnafanyaje kwa ndugu kama hawa.
View attachment 3429287
Mtumie tu
 
Acha roho mbaya mkuu.

Kumsaidia mtu ni tendo la ibada na kwa hakika mtoaji ni Mwenyezi Mungu
Hilo nalijua mkuu lakini mtu ambaye hata hali yako hajui yeye ni kukutafuta kwaajili ya hela tu, hapana acha apambane na hali yake mimi mwenyewe nina matatizo yangu hapa
 
Mi kuna binamu yangu alikua anahiyo michezo..
Nikaanza na mimi kumfanyia ujinga kila akiomba pesa namwambia afate ghetto..

Tena nikawa namwambia njoo uchukue mchumba,,,, weee tangu hapo akawa hana huo ujinga..

Angejichanganya kuja ningemuweka ukuni alafu ndo awe anakula pesa kihalali

Ila ndgu wengine ambao ni tumbo moja na mimi hata iweje mi nampa tuu atajijua yeye napenda sana hawa wadogo zangu...
Sitaki waje wanyanyasike huko ndo mana mapema tatoa tu..
Ila hawa wadogo zangu wa kiume huwa nawapa kama kuna issue ngumu mybe anataka pesa aongezee afanye kitu flani
 
M
Asante sana mkuu nitafanya hivyo maana imezidi anatuma meseji juu ya meseji ya mwezi huu haijibiwi hajiongezi mwezi mwingine anaongeza nyingine
Mkuu nikwambie Kitu Kutoa ni Moyo na wala sio utajiri kama ambavyo walisema wahenga😂😂

Yeye hakuwa ma moyo wa kutoa na wewe kama unao huo moyo ukiweza kusaidia msaidie ukiwa huwezi basi mpotezee usijibu sms zake au block namba yake
Yeye mwenyewe atajiongeza kama wewe ulivyojiongeza mwazo

Habari ka kumchana waachie Kina Chidi Benz
Sana sana utazidisha maneno kwa familia
 
M

Mkuu nikwambie Kitu Kutoa ni Moyo na wala sio utajiri kama ambavyo walisema wahenga😂😂

Yeye hakuwa ma moyo wa kutoa na wewe kama unao huo moyo ukiweza kusaidia msaidie ukiwa huwezi basi mpotezee usijibu sms zake au block namba yake
Yeye mwenyewe atajiongeza kama wewe ulivyojiongeza mwazo

Habari ka kumchana waachie Kina Chidi Benz
Sana sana utazidisha maneno kwa familia
Asante kwa ushauri wako mkuu
 
Back
Top Bottom