wavulana wakianza kusogelea uanaume wanapenda zaidi kushinda na wanaume wenzao, huyo alikuwa mkimya kwenye uvulana ila kwa sasa anasogelea uanaume, Nyumba yenu hiyo imejaa wanawake na mshua yupo bizi, haoni cha kumfanya abaki hapo, kwa sasa anashinda kwa wanaume wenzake, nyumbani kilichobaki ni kulala na kula tu.
Kwa sasa anashinda sana na wanaume wenzake ambao wengine tayari walishaondoka kwao wanaishi kwenye mageto, huko sasa huwa wanapiga story mtoto wa kiume inabidi ashinde na wenzake ama demu wake, kama anaishi nyumbani afanye jitihada ahame na asiruhusu mama au dada zake wampande kichwa ama kumfatilia fatilia maana ashakuwa mwanaume.
huyo mdogo wako ndio anaianza safari ya uanaume, sitashangaa hata chuo achague cha mkoa wa mbali ili apate geto awe na uhuru zaidi, na hizo dawa huenda ni ugeni wa mapenzi alipiga kavu huko gesti akapata ugonjwa, kwa sasa ameshajifunza umuhimu wa condom, kuna mammbo mengi anaendelea kujifunza atarudi kuwa poa tu,