Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Sawa, Asante kwa ushauri mkuu 😊🙏🏼Hebu msikikizeni dingi anavyosema,anajua hata yeye alikuwa hvyo wakati ana balehe.mwenyewe hii tabia nimekuwa nayo tangu nijitambue,japo inapungua kadri muda unavyosonga ila hakuna utamu kama kuwa alone with your thoughts.
Pengine kaingia kwenye mihadarati na ushogaHabari wanajamvi...
Nina imani humu kuna wazazi ambao walishawahi kua na watoto wenye tabia kama hizi naombeni msaada wenu wa mawazo na ushauri unisaidie na mimi.
Binafsi nina mdogo wangu aliyenifuata wa kiume, ana miaka 17...huyu mdogo wangu alikua ni mpole Sanaa, akiwa nyumbani ni mtu wa kushinda ndani mda wote ni kusoma kula na kulala, mara chache sana unaweza kumkuta anaangalia movie hata marafiki zake ni mpaka waje nyumbani kutembelea ndo apige nao story bila hivyo hatoi mguu nyumbani labda aagizwe mahali..
Shida kwamba sikuizi( yani miezi hii hapa miwili) amebadilika sana hadi tunaogopa,, amekua ni mtu wa kuondoka nyumbani bila kuaga na akiondoka asubuhi harudi nyumbani msipompigia simu anaweza asionekane kabisa hadi usiku,, sometimes tukimpigia simu anaweza akapokea halafu akajibu kwa ukali kua tusimfatilie na maisha yake, hataki kula chakula nyumbani, amekua ni mtu wa kufokafoka tu mda wote hadi mama akimuuliza kitu anajibu kwa kufoka tu sio kama alivyokua zamani.
Saizi amefikia hatua kwenda kanisani pamoja na sisi hataki anasema tumuache., alikua anaumwa hakutoa taarifa mpaka anapona na hatuelewi alikua anaumwa nini yani tumefanya tu kustukia kumwona anakunywa dawa, kuna mda alivyoondoka mama akaingia chumbani kwake kukagua akakuta dawa nyingi sana, hata hatuelewi zinatibu ugonjwa gani., baada ya mama kumuuliza alikua mkali sana na ametupigia marufuku kuingia chumbani kwake hata kama ni kufanya usafi.
Ajabu ni kwamba tukimuelezea baba tabia za huyu dogo sikuizi wala hata hatilii maanani anasema tu muacheni kama alivyowaambia mumuache...hasa tatizo ni lipo kwa mama amekua na wasiwasi sana na mabadiliko ya huyu mdogo wangu yani pressure inampanda mda wote, akijaribu hata kukaa nae chini kuongea nae dogo hataki kumskiliza yeyote zaidi ni anakua mkali ukimsogelea jirani anaweza akupige makofi...
Naombeni msaada wenu wa mawazo ili niweze kumsaidia huyu mdogo wangu maana napata shida sana kumuona mama akiwa na wasiwasi mda wote 🙏🏼
Wamchape fimbo mtu wa miaka 17 si watapigana nduguBangeeeee
Tafuteni fimbo atawaeleza tu
Angekua mpenda K asingekua na hasira.Kisha jua utamu wa K tu.Ngoja nitarudi
Aisee,, mbona tatizo hilo sasa.unaweza kunigusia hivyo vitabia labda ili nipate pa kuanzia kumchunguzaAngekua mpenda K asingekua na hasira.
Na dogo akishaanza kupenda chini mtajua tu maana hizo mambo kuficha ni ngumu. Maana marq nyingi atakua anapenda utani wa namna hiyo, marafiki kedekede si rahisi kua na sonona.
Ila Ke ndo anakua na vitabia vya kiburi na kutomsikiliza mtu zaidi ya huyo boyfriend wake.
Huyo dogo kuna vitabia vingine vya hovyo kavianza ama lah anaona nyumbani hawamjali.
Mfuatilieni kwa kina kwasababu haya majanga ndiyo yanayo tafuna watoto wetuAisee 🥺🥺🤔
Sawa, endapo kuna mtu wake wa karibu ambaye ni sawa na jinsia yake na huwa anamtetea sana pale ninyi mnapokuwa mnalalamika nae mumfuatilie kwa undani kwasababu anaweza kuwa ndiye anashiriki nayeSawa,, Asante kwa ushauri mkuu...nitajitahidi nimfuatilie
Kiukweli kwa nyumbani hakuna mtu anayeshirikiana nae,, yuko pekeyake tuSawa, endapo kuna mtu wake wa karibu ambaye ni sawa na jinsia yake na huwa anamtetea sana pale ninyi mnapokuwa mnalalamika nae mumfuatilie kwa undani kwasababu anaweza kuwa ndiye anashiriki naye
Kama ndivyo basi ana marafiki wa nje wabaya. Lakini namna nzuri ya kumsaidia kaa nae chini mkiwa nje ya familia yenu labda Restaurant kisha ongea nae kirafiki mfanye rafiki yako ili awe huru kukueleza. Mara nyingi mkizungumza mkiwa nyumbani anakosa confidenceKiukweli kwa nyumbani hakuna mtu anayeshirikiana nae,, yuko pekeyake tu
Ushauri mzurii huu pia😊🤗Kama ndivyo basi ana marafiki wa nje wabaya. Lakini namna nzuri ya kumsaidia kaa nae chini mkiwa nje ya familia yenu labda Restaurant kisha ongea nae kirafiki mfanye rafiki yako ili awe huru kukueleza. Mara nyingi mkizungumza mkiwa nyumbani anakosa confidence
Utafanikiwa, bado hajatumbukia kwenye mambo mabaya kuna mawazo yanamtesa, zungumza nae atakuelezaUshauri mzurii huu pia😊🤗
Samahani ni muumini wa dini gani huyo dogo?Asante,, tutajaribu kuufanyia kazi ushauri wako...ila kwenye suala la marafiki tumejaribu kuongea na marafiki zake wote nao wanasema wanashangaa mabadiliko yake yanatokana na nini