Huwa mnawashughulikiaje watoto wanaokuwa na tabia kama hii?

Ndio uanamume Ila sio kupiga kavu kavu noma
 
Poleni, kwa maelezo yako dogo anamiliki mda mwingi sana wa kufanya anachotaka, jueni anakoe da kushinda na marafiki zake.

Mpeni majukumu ya kufanya, miaka 17 bado samaki mbichi, mmuonyoshe vizuri.

Mkishindwa pelekeni polisi.
 
Sawa mkuu nimekuelewa
Hamkupiga picha la boksi la dawa ?

Alafu kama kaanza kuvuta bangi akirudi nyumbani macho yake ni mekundu ama ameanza kuvaa miwani mieusi ? kaongeza kiasi cha kula ?

Hapo kwenye pesa huwa mnampa sh ngap kwa siku, wiki au mwezi ?

Kamaliza form 6 au ?
 
Kwakweli sikupiga picha ila makasha yapo naweza nikapiga hata badae nikiwa nyumbani nikaweka,, kwenye suala la chakula sikuizi hataki kabisa kula nyumbani na hatujui anakula wapi, hana dalili yeyote ya kua anavuta bangi..na kuhusu pesa ya matumizi hua anapewa mara nyingi inakuaga 50k per month lakini pia kila akiomba hua anapewa...yupo likizo anasubiri kwenda form five mwezi ujao...hope nimekujibu maswali yako yote πŸ™πŸΌ
 
ah kumbe kamaliza 4, huyo balehe tu inamsumbua ila pia msimfatilie sana huwa inauzi sana kwa teenagers wanachukia wanadhani mnawaona bado watoto, hii inawafanya wawe na kiburi flani hivi cha kujibu kiukali ukali ama kukataa kufanya baadhi ya mambo maksudi ili kujengahali ya kuonekana nao wamekuwa wakubwa wanahitaji space na wanaweza kujifanyia maamuzi yao (kimombo inaitwa teenage rebellion).

msimlee kama yai kila mara kumuuliza kila alichofanya, kumsafishia chumba, n.k.

hajawa mtu mzima huyo ila kinafki nafki mjifanye kama ni mtu mzima ila kiakili kwa kumkumbusha majukumu ya utu uzima na consquences (iwe kijanja isigeuke aanza kuona mnampa darasa kama mtoto, ).

usisahau kuweka picha ya box la dawa na unitag
 
Sawasawa mkuu nimekuelewa Asante kwa ushauri mzurii πŸ˜ŠπŸ™πŸΌ
 
Kuna vtu anafanya huko nje. siku akitoka mfatilie anaendaga wap
 
Ila mara nyingi sana kwa nilio wahi kuwaona kama issue ni madawa ya kulevya lazima watambaini mapema sana huwa inaambatana na tabia zake, nina wasiwasi sana na ndumu.
 
Tafuteni afande mmoja mumpe ela amuadabishe
Ikibidi ampige biti atamlaza selo siku 2 asiposema anapoenda,atanyooka tu huyo!
 
Kunaweza kua na sababu nyingi ila kubwa nahis dogo atakua anapitia zle reaction za balehe, kama sababu ni hii haina shida sana kikubwa muwe na uwezo wa kum-truck asije akapotelea kwenye mikono ya makundi ya watu waovu!

Lkn pia huenda kaanza kujihusisha na matumizi ya bangi na aina nyngn za madawa ya kulevya, Aisee hyo niaje akianza kutumia mwanzoni itampeleka mpera mpera kinoma! siamini kama familia mtashindwa kugundua mapema hili kama kwel yaweza kua sababu.

Pia yaweza kua ni makundi tu ya mtaani kaamua kuadapt maisha, kachoka upweke wa home!


Ushauri wangu!
Sijajua age difference iliyopo Kati ya ww na yy lkn kama upo home means hujamtangulia sana dogo! Jaribu kutengeneza nae urafiki wa kawaida tu ikiwezekana uwe unatengeneza mazingira ya kumtuma mfano unampa buku teni akuweke Tigopesa buku sita then ile buku nne unamwachia lengo ni umtengenezee mazingira ya yy kuweka ukaribu zaidi na ww pia mpe assurance ya akikwama kifedha unaweza msaidia! akiingia kingi akawa anaomba hela! Ndo ufanye anticipation kwa mazingira yenu hicho kiasi Cha pesa anachoomba linaweza kua Cha nn


Mtafute rafiki yake moja weka ukaribu nae atakuuzia details zote hapa ndo sehemu pekee utapata details za uhakika!

Ila huenda mzee hana wasi wasi huenda kashamsoma dogo nje ndani na anajua kila kitu Nyie mnateseka tu
 
tatizo ni kwamba baba tumemshirikisha na hafanyi lolote anasema tumuache tu kama alivyosema mwenyewe..na bad luck nyumbani hatuna mwanaume mwingne zaidi ya yeye na baba tu
Huenda baba anahusika na tatizo, au si babake.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…