Huwa mnawashughulikiaje watoto wanaokuwa na tabia kama hii?

Mmh πŸ€”πŸ€”,, mbona unanipa wasiwasi jamani
Si lazima niwe sahihi, Ila ongeza umakini na umvizie kwa uchunguzi mkubwa.Usijishughulishe nae wazi wazi ila mfuatilie kwa ukaribu.Kama ni mwanaume hakikisha kama yupo kamili.
 
Si lazima niwe sahihi, Ila ongeza umakini na umvizie kwa uchunguzi mkubwa.Usijishughulishe nae wazi wazi ila mfuatilie kwa ukaribu.Kama ni mwanaume hakikisha kama yupo kamili.
Sawa mkuu nimekuelewa,,Asante kwa ushauri pia πŸ™πŸΌ
 
Balehe Plus Bange vinamuendesha dogo!
 
Kwenye suala la chakula alikua anakula vizuri tu bila shida,, usafi pia yuko vizuri...kwamba ameanza kufanya mapenzi hapo ndo ninaposhindwa kuamini...ila tutaufanyia kazi ushauri wako mkuu[emoji1374]
17years asifanye mapenzi? Watoto siku hizi wanabalehe at tha age of 15yrs tu tayari vuzi limeota na wanapata ndoto nyevu.

Huyo dogo kwani unavyomuona bado hajabalehe?
 
*Kipigo hakitamsaidia.

*Nyie watoto wakike ndo mnamvuruga na hatoweza kuwaelewa zaidi ndo mtazidi kumchukiza kwa kumfatafata.

*Baba ndo mwenye huo uwezo.

*Short story

Mimi kipindi nipo kwenye iyo age niliwahi kutamani kumpiga jiwe dada yangu la kichwa na hatakama angekufa nisingejali.(hasira)
Nilitamani kua mbali na familia yangu nikae mwenyewe.(hasira)
Niliwahi kusimama mbele ya daraja marakadhaa nikitaka kujiua(hasira)
Niliwajibu dada zangu na kaka zangu ovyo samtimes(hasira)

Majibu ya kwanini.
-Wazazi, ndugu hawakuwahi kujua madhara ya maneno waliokua wakiyaongea kimzaa kuhusu mimi kumbe kwenye moyo wangu nilikua nayachukulia serious sana bila wao kujua.

-Walikua sametimes wakinisingiizia vitu au kunionea kwa kunisemea mambo yasikua ya kweli kwa wazazi, mda mwingine walipenda kunicontrol sababu waliona mi mdogo kwao bila kujua kua moyoni nilikua nayatunza na nikiwa mwenyewe nilikua nalia sana.

-Yapo mengi ila outcome mwisho wa siku ilikuja kuonekana nina kiburi pia najiona nimekua, mda huo kwenye akili yangu na moyo nishakata ile bond ya undugu bila wao kujua, na hatari zaidi wanaishi na mtu ambae ni (PSYCHO GUY) bila kujua wakidhani peer groups ndo zinaniharibia.

USINGESEMA ALIKUA MPOLE NISINGESEMA KITU ila kwa experience yangu including me, nakushauri ogopa sana watu wasio ongea, wakimya, in general wapole hao watu wanavitu vingi kwenye vichwa na mioyo yao unaweza kuta chanzo ya haya yote kuna jambo mlimfanyia miaka mitano ilopita saivi ni outcomes tuu,

Nakushauri kama unampenda mwache kwanza huru kama mzee alivosema pili kama kuna ndugu anayempenda kama shangazi au bibi mpelekeni akakae hata mwezi mmoja akirud jenga character tofauti usipende kujifanya unamchunguza au comhandle njia pekee yakuweza kumjua ni kua rafiki yake wa siri mpe uhuru wa kukuambia siri zake bila kujudge ndo mtaweza kujua anashida wapi na wapi na mkishajua ilo mtamuhandle bila tatizo.
 
Hili la msingi wajaribu kuwahusisha majirani,maaana huwenda wana umbea lakini wanashindwa kufikisha ujumbe kwa familia
 
Hapana hiii hali ni ya kawaida , mimi mwenyewe nimepitia hiii hali ,mpaka saivi ninayo kwa kiasi ,nikipata time ntaelezea.
 
Hili la msingi wajaribu kuwahusisha majirani,maaana huwenda wana umbea lakini wanashindwa kufikisha ujumbe kwa familia
Labda nao ni zile familia bora ambazo zimezungukwa na majirani hali ya chini hivyo hawachangamani kiivyo.
 
Ukiondoa baba, hakuna mwanaumwe mwingine azungumze nae....?
 

Mkuu huu ushauri hauwezi kupata summary ya Kiswahili?
 
Kwa fikra zangu anaweza akawa ameanza kuvuta bangi maan for some people ndo zinakuwaga side effects zake au ameanza tabia ya ushoga au amepata maambukizi ya ukimwi au magonjwa mengine ya zinaa yaliyopelekea kuharibu saikolojia yake.. ni vyema atafutiwe canceller wa kuzungumza nae haraka iwezekanavyo kabla mambo hayajaaribika zaid...
 
Mchunguzeni kwa umakini katika vitu hivi:

1.Muonekano wake wa mwili ukoje.Uko tofauti na zamani? Mfano kifua chake kimeongezeka kama mtu afanyaye mazoezi?,

Mikono yake imejenga mizuri na kiganja cha mkono wake kimejaa ?

2.Anatembeaje? Kama zamani au amebadilisha aina ya utembeaji?

3.Ana mwili mwepesi tofauti na zamani, au amekuwa mvivu mvivu?

5.Kuna siku amewahi kurudi nyumbani akawaambia anajisikia kuchoka sana?

N:B.Baba anafanya kazi gani au kwenye taasisi ipi? Sihitaji uitaje.

Nimeuliza hivi kwasababu baba amesema muacheni huenda anajua kila kitu kinachoendelea ndio maana haoni tatizo ila hataki kuwaambia ukweli.
 
Unafahamu rafiki zake wa karibu ?
 
Subirini wakutane na jela ....atanyoooka kuna kundi Nakutana nalo Huyo
 
Kufanya mapenzi pekee hakupelekei hali hiyo

Nina shaka na makundi
 
Nilicho kiona huyo dogo humo ndani kwenu anawazazi watatu baba,mama, na wewe ...maana umejivisha uzazi.


Na kikubwa huyo dogo mmekuwa mkimfuatilia Sana na kuingilia privacy zake nyingi na kumtreat kama mtoto mdogo.


Hivyo amekua na yupo kwenye balehe na anajiona amesha kuwa mtu mzima na nyie ni watu ambao mnapambana kumdogosha ili kuwakata vimidomo vyenu ndio maana anafanya hivyo hataki mazoea na nyie.


Halafu amesha pata demu na hizo dawa huenda aliambukizwa STDs so akawa anajitibia....wanao sema dogo ni shoga hao ni wapumbavu na ndio mashoga wenyewe angekua shoga angekua anakenua kenua meno na nyie.

Dogo yupo sawa muacheni mpeni uhuru
 
Uyo dogo atakuwa kaachwa labda stress tu

Yupo form ngapi?

Kwenda na nyie church ata mm namuunga mkono
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…