Huwa najiuliza swali, Endapo waafrika weusi tungepewa utajiri wa mafuta kama ilivyo kwa waarabu je tungeudumisha kama kinachoendelea UAE?

Huwa najiuliza swali, Endapo waafrika weusi tungepewa utajiri wa mafuta kama ilivyo kwa waarabu je tungeudumisha kama kinachoendelea UAE?

Hata hao wachache wanaokula bado hawajala inavyopaswa.

Kwa nigeria kidogo naona wanajitahidi kuna familia za kina davido wale watoto wao wanazaliwa wanaukuta utajiri.

Kipindi davido kanunua ile RR sikushangaa sabab dogo hela kazikuta zinatiririka kwao kutoka kwenye visima vya mafuta.

Hao walaji bado kabisa hawajala inavyopaswa, wengi ni kama vibaraka tu
Davido kwako ni dogo?
 
Makaburu waliitengeneza Johannesburg kupitia Dhahabu, johannesburg yetu ipo wapi?..

Mauritius ni kisiwa cha utalii na maisha yao yanaenda, sisi ukiitoa Zanzbar, hii coast yetu toka Tanga hadi Mtwara tumeifanyia nini?...

Vipi wenzetu Botswana, maisha wanaendesha kwa kutegemea almasi. Tuseme ni nchi ndogo, je shinyanga ina dalili zozote za kufikia standard ya maisha ya watswana?...

Tanzania hata tungepewa mafuta, tungeendelea kuwa na uhaba wa umeme kama Nigeria. Huo ndio uhalisia
 
Hhahahaa
 
Jana nimemaliza safari yangu ya kikazi ya siku 4. Nilianzia Dubai nikakaa siku 1 kisha nikaelekea Abu Dhabi nikakaa siku 2. Nikamalizia Qatar siku 1. Na kila mara nikiwa kwenye ndege narudi bongo kutokea UAE huwa najiuliza hilo swali, hivi sisi waafrika weusi tungepewa huo utajiri wa mafuta, je tungekua matajiri kama walivyo waarabu?

Tajiri pekee mweusi alieweza kutengeneza utajiri wa kutisha na kuwaogopesha wazungu na wa-asia kipindi kile alikua ni mwamba Mansa Musa. Huyu jamaa yeye aliweza kudeal na gold na ikamtoa. Tukipata Mansa Musa mwingine tukampa North mara au GGM basi tutegemee kuwa namba 1 kiuchumi.

Unajua kuna hela, mali na utajiri hivo ni vitu tofauti kabisa. Mfano wazungu wengi tunasema wana hela, lakini sio kwamba ni matajiri kama miamba ya UAE, hao kina elon, mara billgates, na wengineo stock exchange ikireverse kidogo tu utajiri wao unashuka.

Mfano kampuni ya apple ina thamani ya Trillion 3 kwa sasa, lkn ukiangalia assets wala hazifiki hata billion 300. So ni pesa za namba tu.

Sasa njoo UAE, wale ni visima vya mafuta ambapo value zao sio kama kwa makampuni ya USA. Na ndio maana ukifanya deal na mwarabu yoyote au kampuni yoyote ya UAE wale jamaa wanakulipa cash, na wala sio stock au stock options.

Kuna banks kubwa kadhaa zilitetereka mwaka 2023 lakini mwarabu akajaza cash wakarudi mzigoni.

Ukitaka kujua utajiri ni nini basi nenda UAE, hela sio utajiri. Haiwezekani mtu una 100m bank halafu unajibania bania kula misosi ya maana au kuendesha ndinga za maana. Wewe sio tajiri bali ni una hela tu bank. Kaangalie kufuru za UAE, unapishana na ferrari imepakwa gold mwanzo mwisho.

Kufuru za utajiri wa UAE hakuna pengine duniani utaziona, labda kidogo sana Monaco, Italy wanajitahidi ila wao wengi ni familia na kimafia na wauza sembe
Angola na Nigeria wana mafuta mengi tu, ila ni Ufisadi kwenda mbele, Raisi wa Zamani wa angola na Binti yake ndio wa Africa mwanamke na mwanaume wenye Utajiri zaidi. Wakati wao ni matajiri hivyo wananchi wao wana Umasikini wa kutupwa.
 
Tumepewa na wanakula wachache.
Hapo nigeria wana hifadhi kubwa sana ya mafuta ila wanaofaidi ni kina dangote.
Angola pia anazalisha crude oil.

Hapo uganda nayeye soon atakuwa na mafuta kutoka Ohima to Tanga.

Tanzania tuna mafuta ya mwampossa. Raia tunayatumia kupata kazi na pesa na miujiza kupitia maombi.
Raia wenye uraia wa UAE ni milioni 1.5 tu
 
Makaburu waliitengeneza Johannesburg kupitia Dhahabu, johannesburg yetu ipo wapi?..

Mauritius ni kisiwa cha utalii na maisha yao yanaenda, sisi ukiitoa Zanzbar, hii coast yetu toka Tanga hadi Mtwara tumeifanyia nini?...

Vipi wenzetu Botswana, maisha wanaendesha kwa kutegemea almasi. Tuseme ni nchi ndogo, je shinyanga ina dalili zozote za kufikia standard ya maisha ya watswana?...

Tanzania hata tungepewa mafuta, tungeendelea kuwa na uhaba wa umeme kama Nigeria. Huo ndio uhalisia
Botswana ina raia milioni 2.5
UAE raia wake wenye uraia ni milioni 1.5, wengine wageni.
 
Tupewe mara ngapi sasa, madini yako kila mahala, gas ipo yakutosha kabisa tumevifanyia nini? zaidi ya wachache na familia zao kujinufaisha?.

Hata mafuta yangekuwepo zingekuwa story hizi hizi, za paka na panya.
Population nayo inachangia umaskini kama taifa haliko vizuri katika teknolojia.
 
Population nayo inachangia umaskini kama taifa haliko vizuri katika teknolojia.

Population inapaswa kuwa controlled sambamba na ukuaji uchumi, either mzae sana na upande mwingine mfanye kazi sana na kuzarisha sana kuendana na kasi yetu ya kuzarisha.

Kushindwa kubalance ukuaji wa population sambamba na ukuaji wa uchumi wenu NI umasikini mwingine huo.

Kila kitu kinapaswa kuwa kwenye control yetu kushindwa kwetu kucontrol kila kitu ni sababu nyingine ya umasikini wetu.
 
Jana nimemaliza safari yangu ya kikazi ya siku 4. Nilianzia Dubai nikakaa siku 1 kisha nikaelekea Abu Dhabi nikakaa siku 2. Nikamalizia Qatar siku 1. Na kila mara nikiwa kwenye ndege narudi bongo kutokea UAE huwa najiuliza hilo swali, hivi sisi waafrika weusi tungepewa huo utajiri wa mafuta, je tungekua matajiri kama walivyo waarabu?

Tajiri pekee mweusi alieweza kutengeneza utajiri wa kutisha na kuwaogopesha wazungu na wa-asia kipindi kile alikua ni mwamba Mansa Musa. Huyu jamaa yeye aliweza kudeal na gold na ikamtoa. Tukipata Mansa Musa mwingine tukampa North mara au GGM basi tutegemee kuwa namba 1 kiuchumi.

Unajua kuna hela, mali na utajiri hivo ni vitu tofauti kabisa. Mfano wazungu wengi tunasema wana hela, lakini sio kwamba ni matajiri kama miamba ya UAE, hao kina elon, mara billgates, na wengineo stock exchange ikireverse kidogo tu utajiri wao unashuka.

Mfano kampuni ya apple ina thamani ya Trillion 3 kwa sasa, lkn ukiangalia assets wala hazifiki hata billion 300. So ni pesa za namba tu.

Sasa njoo UAE, wale ni visima vya mafuta ambapo value zao sio kama kwa makampuni ya USA. Na ndio maana ukifanya deal na mwarabu yoyote au kampuni yoyote ya UAE wale jamaa wanakulipa cash, na wala sio stock au stock options.

Kuna banks kubwa kadhaa zilitetereka mwaka 2023 lakini mwarabu akajaza cash wakarudi mzigoni.

Ukitaka kujua utajiri ni nini basi nenda UAE, hela sio utajiri. Haiwezekani mtu una 100m bank halafu unajibania bania kula misosi ya maana au kuendesha ndinga za maana. Wewe sio tajiri bali ni una hela tu bank. Kaangalie kufuru za UAE, unapishana na ferrari imepakwa gold mwanzo mwisho.

Kufuru za utajiri wa UAE hakuna pengine duniani utaziona, labda kidogo sana Monaco, Italy wanajitahidi ila wao wengi ni familia na kimafia na wauza sembe
Wapo waliopewa kama Nigeria, Angola, Equatorial Guinea, Gabon ila Sasa wanakula wachache
 
Mwafrika hana akili,wewe na kwenda kote huko kwanini hujaulizia historia ya Dubai???Usomi wako uko wapi bwashee kwanini unashangaa na kutafakari kimyakimya😄😄😄au unaogopa kuchekwa kama kawaida yetu inferiority complex.

Mfalme wa dubai angeweza kujilimbikizia mali na kula na familia yake na ukoo wake, ila alikuwa na AKILI TIMAMU.Akaamua kuweka ubinafsi kando rasilimali za nchi zikaijenga Dubai,leo kila mtu anaenda kushangaa dubai mpaka wazungu wenyewe.

Ukija africa UBINAFSI na UKOSEFU WA VIPAUMBELE umetufanya tumekuwa mzigo,vituko na mazombie hapa duniani.

Leo uganda ameshindwa kukaza msuli awekeze pesa achimbe mwenyewe mafuta yake, kampa Ufaransa hapo kuna watu wamelamba 10% wametulia na familia zao mafuta yatatoka Uganda yatapita hapa kwetu yataenda Ufaransa😂😂😂😂😂 nabado unauliza mnafeli wapi,waafrica ni jamii iliyo LAANIWA.

Wazungu hawana kosa hata ukoloni unasingiziwa ukweli usemwe sisi hakuna kitu tunaweza. Ukirudi hapa kwetu tuna GESI hiyo tu inatosha kutufanya tuishi kama Libya ya Gaddafi ila yakuwapi.

Msitafute mchawi,wala wa kumtupia zigo la mavi UBINAFSI ndio shida ya AFRICA.Ajabu ni kuwa tatizo mbegu ya ubinafsi imemea vilivyo kiasi kwamba hata mtoto anayezaliwa leo anazaliwa na UBINAFSI.We as a continent, we are finished!!!
Umemaliza Mkuu.

Hapa ndipo lilipo tatizo la Afrika.
 
Afrika kuna nchi zenye mafuta kama Nigeria lakini angalia matatizo yao mpaka leo na population yao ni kubwa sana
Wana vyuo vikuu zaidi ya 100 ila hakuna majizi kama hayo
Mtu anasoma ili aibe ni kama sisi tu hakuna tofauti
Kwanza mtu mweusi akili ni nzito sana kufikiri na kujifanya ujuaji mwingi
Kila leo wanasafiri ila hawajifunzi.
Unakuta mtu anajisifia kusoma vitabu 50 kwa miezi kadhaa ila hawezi kukujibu kwanini shule haina vyoo
Au hospital hazina madawa?

Nilijaaliwa kwenda falme za kiarabu mwishoni mwa miaka ya 70
Wakati huo walikuwa na TV zamani na nilikuwa nacheza Atari enzi hizo
Wao walipofanikiwa kupatiwa mafuta walisaini mikataba ya kulindwa na pia kuwatengenezea miundombinu na kila kitu ili wale neema ya nchi
Leo sisi tunasaini mikataba kwa maslahi ya watu wachache tu ila hawajali wananchi
 
Hata huyo muarabu hana jipya, hayo mafuta yaligunduliwa na mzungu, na huyo huyo mzungu ndiye mwenye teknolojia ya kuyachimba, muarabu amekaa kupokea tu na kuvaa kobaz huku akifadhili ugaidi wa dini.
 
Hata huyo muarabu hana jipya, hayo mafuta yaligunduliwa na mzungu, na huyo huyo mzungu ndiye mwenye teknolojia ya kuyachimba, muarabu amekaa kupokea tu na kuvaa kobaz huku akifadhili ugaidi wa dini.
Gesi ya mtwara na dhahabu ya bulyanhulu unajua inaweza kufanya hayo yote..? Muarabu apewe maua yake

Nenda kakola uone njaa na ukimwi ulivyojaa nenda nyagoto, kewanja tarime uone vijumba sijui vya msauth aloo 😅😅😭😭😭😭😭
 
Unadhani nani anaye own hayo Mafuta zaidi ya the Seven Sisters na hao wote ni ma cronies.., tofauti kinachopatikana kina kuwa shared vipi (percentagewise) sababu unaweza ukawa umesign mikataba kama ya Botswana au ya Kimangungo wa Msovero....

Pili hizo Nchi ni za Wafalme kwahio hao wameshanunuliwa na kupewa Rupia za Kutosha kinachoendelea wamekuwa tu kama part ya hizo Corporations....

Thus those Arabs ni Nyenzo za hao wengine wanaonufaika ndio maana hata Gadafi alivyotaka kuwabania na kuhakikisha utajiri huo unasambazwa kwa watu wake na huku Afrika kilichomkuta kila mtu anajua
 
Back
Top Bottom