Huwa najiuliza swali, Endapo waafrika weusi tungepewa utajiri wa mafuta kama ilivyo kwa waarabu je tungeudumisha kama kinachoendelea UAE?

Davido kwako ni dogo?
 
Makaburu waliitengeneza Johannesburg kupitia Dhahabu, johannesburg yetu ipo wapi?..

Mauritius ni kisiwa cha utalii na maisha yao yanaenda, sisi ukiitoa Zanzbar, hii coast yetu toka Tanga hadi Mtwara tumeifanyia nini?...

Vipi wenzetu Botswana, maisha wanaendesha kwa kutegemea almasi. Tuseme ni nchi ndogo, je shinyanga ina dalili zozote za kufikia standard ya maisha ya watswana?...

Tanzania hata tungepewa mafuta, tungeendelea kuwa na uhaba wa umeme kama Nigeria. Huo ndio uhalisia
 
Hhahahaa
 
Angola na Nigeria wana mafuta mengi tu, ila ni Ufisadi kwenda mbele, Raisi wa Zamani wa angola na Binti yake ndio wa Africa mwanamke na mwanaume wenye Utajiri zaidi. Wakati wao ni matajiri hivyo wananchi wao wana Umasikini wa kutupwa.
 
Raia wenye uraia wa UAE ni milioni 1.5 tu
 
Botswana ina raia milioni 2.5
UAE raia wake wenye uraia ni milioni 1.5, wengine wageni.
 
Tupewe mara ngapi sasa, madini yako kila mahala, gas ipo yakutosha kabisa tumevifanyia nini? zaidi ya wachache na familia zao kujinufaisha?.

Hata mafuta yangekuwepo zingekuwa story hizi hizi, za paka na panya.
Population nayo inachangia umaskini kama taifa haliko vizuri katika teknolojia.
 
Population nayo inachangia umaskini kama taifa haliko vizuri katika teknolojia.

Population inapaswa kuwa controlled sambamba na ukuaji uchumi, either mzae sana na upande mwingine mfanye kazi sana na kuzarisha sana kuendana na kasi yetu ya kuzarisha.

Kushindwa kubalance ukuaji wa population sambamba na ukuaji wa uchumi wenu NI umasikini mwingine huo.

Kila kitu kinapaswa kuwa kwenye control yetu kushindwa kwetu kucontrol kila kitu ni sababu nyingine ya umasikini wetu.
 
Wapo waliopewa kama Nigeria, Angola, Equatorial Guinea, Gabon ila Sasa wanakula wachache
 
Umemaliza Mkuu.

Hapa ndipo lilipo tatizo la Afrika.
 
Afrika kuna nchi zenye mafuta kama Nigeria lakini angalia matatizo yao mpaka leo na population yao ni kubwa sana
Wana vyuo vikuu zaidi ya 100 ila hakuna majizi kama hayo
Mtu anasoma ili aibe ni kama sisi tu hakuna tofauti
Kwanza mtu mweusi akili ni nzito sana kufikiri na kujifanya ujuaji mwingi
Kila leo wanasafiri ila hawajifunzi.
Unakuta mtu anajisifia kusoma vitabu 50 kwa miezi kadhaa ila hawezi kukujibu kwanini shule haina vyoo
Au hospital hazina madawa?

Nilijaaliwa kwenda falme za kiarabu mwishoni mwa miaka ya 70
Wakati huo walikuwa na TV zamani na nilikuwa nacheza Atari enzi hizo
Wao walipofanikiwa kupatiwa mafuta walisaini mikataba ya kulindwa na pia kuwatengenezea miundombinu na kila kitu ili wale neema ya nchi
Leo sisi tunasaini mikataba kwa maslahi ya watu wachache tu ila hawajali wananchi
 
Hata huyo muarabu hana jipya, hayo mafuta yaligunduliwa na mzungu, na huyo huyo mzungu ndiye mwenye teknolojia ya kuyachimba, muarabu amekaa kupokea tu na kuvaa kobaz huku akifadhili ugaidi wa dini.
 
Hata huyo muarabu hana jipya, hayo mafuta yaligunduliwa na mzungu, na huyo huyo mzungu ndiye mwenye teknolojia ya kuyachimba, muarabu amekaa kupokea tu na kuvaa kobaz huku akifadhili ugaidi wa dini.
Gesi ya mtwara na dhahabu ya bulyanhulu unajua inaweza kufanya hayo yote..? Muarabu apewe maua yake

Nenda kakola uone njaa na ukimwi ulivyojaa nenda nyagoto, kewanja tarime uone vijumba sijui vya msauth aloo πŸ˜…πŸ˜…πŸ˜­πŸ˜­πŸ˜­πŸ˜­πŸ˜­
 
Unadhani nani anaye own hayo Mafuta zaidi ya the Seven Sisters na hao wote ni ma cronies.., tofauti kinachopatikana kina kuwa shared vipi (percentagewise) sababu unaweza ukawa umesign mikataba kama ya Botswana au ya Kimangungo wa Msovero....

Pili hizo Nchi ni za Wafalme kwahio hao wameshanunuliwa na kupewa Rupia za Kutosha kinachoendelea wamekuwa tu kama part ya hizo Corporations....

Thus those Arabs ni Nyenzo za hao wengine wanaonufaika ndio maana hata Gadafi alivyotaka kuwabania na kuhakikisha utajiri huo unasambazwa kwa watu wake na huku Afrika kilichomkuta kila mtu anajua
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…