Huwa unafanya nini ukiwa na msongo wa mawazo na si mnywaji wa pombe?

Huwa unafanya nini ukiwa na msongo wa mawazo na si mnywaji wa pombe?

Ila hii kufua nayo ni Best option,, Tena uanike kama ikatike uanze Tena upya Hadi kutulia stress zote zimeisha😂😂.. Ms eyes
Umenichekesha kuna siku ilinitokea nna stress nikasema ngoja nifue nipoteze muda, nikatoa nguo na mapazia yote nikafua, wakati naanika kivivu kabisa nikawaza ivi hii kamba ikikatika inakuaje?(huwa nikihisi kitu huwa mara nyingi kinatokea hata kama sio kwangu). Ile nimemaliza kuanika nguo ya mwisho kamba ikakatika, nilijikuta nimekaa chini nguo zipo chini zaidi ya nusu saa 😂
 
Hua inategemea kama ni ile nimevurugwa sana naenda home kwa maza na mzeee hapa nikikaa wiki tu nakua vzr pia ntakutana na baadhi ya wanangu wa utotoni! Akili itakaa powa plus siku narudi town ntafungashiwa tuvitu vitu

Kama ni hz stress ndogo ndogo za hapa na pale mara Amina kanijibu vbya sijui euny kasema na pc yangu au kazini nimevurugwa hua napiga misele naenda huko kivule sijui kisemvule, mpaka jion ntakua nimechoka narudi geto nalala
 
Kutembea nayo ni best sana huwa naitumia pia hasa kagiza kakiingia, earpods masikioni mziki mkubwa mkono mmoja mfukoni natembea nashangaa shangaa dunia.
Mie huwa natembea kwa mguu masaa 12 huko nasikiliza wimbo wa Bob Marley - Stir up little darling kuondoa stress.

Nachoupendea huo wimbo ni ule mdundo wake na mtiririko wa zile sauti za waimbaji, huwa natembea huku nadunda kama Bob hadi stress inakata kabisa 😂
 
Umenichekesha kuna siku ilinitokea nna stress nikasema ngoja nifue nipoteze muda, nikatoa nguo na mapazia yote nikafua, wakati naanika kivivu kabisa nikawaza ivi hii kamba ikikatika inakuaje?(huwa nikihisi kitu huwa mara nyingi kinatokea hata kama sio kwangu). Ile nimemaliza kuanika nguo ya mwisho kamba ikakatika, nilijikuta nimekaa chini nguo zipo chini zaidi ya nusu saa 😂
Yani hapo stress zote zinahamia kwenye nguo😃😂😂
 
Mie huwa natembea kwa mguu masaa 12 huko nasikiliza wimbo wa Bob Marley - Stir up little darling kuondoa stress.

Nachoupendea huo wimbo ni ule mdundo wake na mtiririko wa zile sauti za waimbaji, huwa natembea huku nadunda kama Bob hadi stress inakata kabisa 😂
Mchungaji unatumia bangi? 😂

Mimi naweka dj mix kali ya riddim natembea mdogo mdogo sina muda na mtu tofauti na salam kwa kupunga mkono basi.
 
Nilimind haswa nikajikuta naongea na nguo naziapia walai sirudii kusuuza nazianika hivyo hivyo na sikuzisuuza nikaanika vilevile 😂.
Zilivyokauka ndio nikajua hasira hasara
Bora wewe ulipata na nguvu ya kuanika tena.. Niliziacha chini hadi siku ya pili asubuhi nikazikuta zimeoshwa na kuanika tena, sijajuaga nani ananionea huruma 😂😂🤦‍♀️
 
Mawazo yanatesa sana.
Sipendi kuwaza hovyo, naandika kwenye karatasi kila wazo linalosumbua ubongo wangu wakati huo.

Kisha nayasoma kuna mengine hayana maana yanakata, ya muhimu natafuta solution.

Muziki, pombe ni kuudanganya ubongo kwa mda tu, kabiliana nayo na tafuta suluhisho.
 
Back
Top Bottom