Huwa unamuamini asilimia ngapi mwenyeji wako anapokwambia usiogope, Mbwa wake hang'ati?

Huwa unamuamini asilimia ngapi mwenyeji wako anapokwambia usiogope, Mbwa wake hang'ati?

Mbwa hafai, kuna nyumba moja iko jirani na tunakoishi kuna Mzungu alikuwa anaishi hapo na anafuga mbwa wakubwa tu. Na yana sauti kubwa yakibweka, na yeye huwa anatoa kauli hiyo hiyo. Sasa kuna siku nilikatiza hapo kwake mchana, na nilikua nimejisahau kama kuna mbwa wakali, sijui nilikua nawaza nini!! Ghafla mbwa wanaunguruma pembeni yangu, kugeuka kuangalia, naona mbwa wawili wako spidi wananifuata. Sikujiuliza mara mbili, nilifyatua mbio huku napiga mayowe. Na ndala niliziacha palepale getini kwake!! Ila nilishangaa kuona watu wananicheka, halafu wala hawana mpango na mimi. Baadaye nikasimama baada ya kuona kimya, kuja kufuatilia, kumbe wako ndani ya fence, zile za waya, kwa nje kumepandwa michongoma. Kwahiyo ukicheki kwa haraka, utaona michongoma tupu. Nikazirudia ndala zangu, nikasepa.
Hahah
 
Mbwa akishakuwa karibu yako hautakiwi kukimbia, maana kitendo cha kugeuka ili ukimbie mwenzako atakichukulia kama vile unapanga shambulizi dhidi yake, so atakuwahi na atakuchana chana vibaya sana.

Unapomuona ashakufikia karibu, unachotakiwa kufanya ni kuuvaa ujasiri kwa kujifanya umemzoea, unampenda na uko tayari kucheza nae. Kwa kuwa mbwa wamepewa fahamu, basi ataweza kufahamu kuwa wewe sio adui yake bali ni rafiki yake, na hapo ule mpango wake wa kukuvamia ili akudhuru utakuwa umekufa kibudu.
😂😂😂
 
Mnawaogopa hawa[emoji23][emoji23]
JPEG_20221224_195456_262589265487541352.jpg
 
Kuna jamaa nilienda kumtengenezea gari kwake. Kufika kwake nikakuta anafuga mbwa wawili, yan pit bull wakubwa walioshiba.

Akanambia wewe fanyakazi tu wala usiogope. Kwa vile ilikuwa mara yangu ya kwanza kufika kwake, nikajifanya sina uoga na viumbe wale.

Nikiwa katika harakati zangu za kazi mara jamaa akanifuata na kuniambia kuwa anatoka mara 1 kwenda kumfuata mtoto shuleni (sio mbali sana na anapoishi) akasema wewe usiwe na wasi wasi hao hawawezi kukufanya chochote.

Dah kukataa nikashindwa na kukubali pia nikashindwa nikabaki kumeza fundo la mate huku nikijifanya sina wasi wasi na viumbe wale. Jamaa akaniachia funguo 1 ya gate la nje akafungua gate akatoka na kutuacha sisi watatu, yani mimi na ile mi pit bull miwili, basi ikawa inaniangalia huku inanikazia macho kama vile inataka nijichanganye kidogo tu inichane chane, maana tayari ulimi uko nje, huku mijino kama vidole vya mtu mzima.

Kitu cha kwanza nikatoka chini ya gari na kuingia ndani ya gari. Sasa wakati nikiwa ndani ya gari nikasikia honi ya gari inaita kwa nje ya nyumba, nikajiuliza huyo ni mshikaji amerudi anataka nikamsaidie vitu au ni mtu mungine anapiga honi nyumba ya pili, honi ikaendelea wale mbwa wakakurupuka na kukimbilia mlangoni wakawa wanabweka ile mbaya.

Hapo nikajua anaepiga honi yuko mlangoni na pia inaonesha sio mwenyeji wa nyumba ile maana ingekuwa ni mwenyeji wasingebweka vile, kidogo simu inaita jamaa ananambia nichukue funguo alioniachia nikamfungulie mgeni wake.

Hapo ndio palikuwa patamu maana jamaa nilikuwa nishamuonesha kuwa wale mbwa siwaogopi, sasa naanzaje tena kumwambia kuwa naogopa kwenda kufungua? Ikabidi nimwambie kuwa niko msalan nakata gogo, akasema poa fanya fasta basi ukamfungulie.

Jamaa akampigia akamwambia mgeni asubiri nikimaliza kukata gogo nitamfungulia. Baadae akanipigia tena bado tu, nikabidi nimwambia ndo najisafisha natoka sasa hivi.

Nikasema potelea mbali wakinivamia atanilipa, nikaanza kulifuata gate la nje kwa kunyata kumbe washanisikia ghafla nikaona hao wanakuja mbio upande wangu, nikaona nikikimbia watanivamia, ikabidi nioneshe ukakamavu ghafla hawa miguuni, sasa nilichofanya nikamshika yule dume kichwani kama nampalaza palaza likatulia huku likionesha kuelewa ninachokifanya nikawa natembea mdogo mdogo kuelekea getini huku wakinifuata kama vile ni mtu wanaenifahamu, ile kufika getini nafungua na mwenyeji namuona yule kwa mbali anakuja. Basi wakaingia wote mwenyeji, mtoto na mgeni tukafunga geti.
Aisee siku ile sintoisahau.

Kwa wale wasiomjua pit bull, huyu hapo pichani kulaleki 😂
kwanza mimi siwapendi mbwa. kubwa ni kwamba siwaamini kabisa
RIP mzee Kingunge Ngombari mwiru
 
kwanza mimi siwapendi mbwa. kubwa ni kwamba siwaamini kabisa
RIP mzee Kingunge Ngombari mwiru
Mbwa kwa upande mmoja ni mlinzi na rafiki mzuri sana kwa binadam, lakini kwa upande wa pili ni hatari na adui mkubwa sana kwa binadam.
 
Bata mzinga wanashida gan
Mimi ninachojua hawa bata tunaofuga ndo noma. Kuna bata ambao ni wakali, wakorofi na wagomvi. Unaweza kupita karibu yake ukashangaa anakufuata na kukurukia, na kila utapomfukuza ndo unamtuma aendelee kukufuata zaidi mpaka mtu mungine anaamua kutoka mkuku ili kuepusha shari 🤣🤣🤣
 
Mimi ninachojua hawa bata tunaofuga ndo noma. Kuna bata ambao ni wakali, wakorofi na wagomvi. Unaweza kupita karibu yake ukashangaa anakufuata na kukurukia, na kila utapomfukuza ndo unamtuma aendelee kukufuata zaidi mpaka mtu mungine anaamua kutoka mkuku ili kuepusha shari 🤣🤣🤣
Heh nikajua wapole wanavodema na shingo zao
 
Aisee sio tu ningeisoma namba bali pengine leo hii ningekuwa naitwa marehem fulani, au wangeniachia ulemavu wa kudumu, maana hakuna mbwa mkali, hatari na mwenye nguvu kama pit bull. Huyo german shepherd mwenyewe akikutana na pit bull ujue siku hiyo hata wenye mbwa wao wenyewe watashindwa kuwaamua.

Na isitoshe walikuwa wakubwa last namba afu wameshiba haswa, wakitembea unasikia chini ti ti ti ti.
Wasingekuua ila chamoto ungekiona kwasababu wenyeji wako walikua karibu wangewahi kukuokoa[emoji28][emoji28]
 
Heh nikajua wapole wanavodema na shingo zao
Aisee sisi tushawahi kufuga bata nawajua vizuri. Ni wakorofi vibaya mno afu bata anaweza kudindishiana hata na mbuzi. Kwa watu ambao washafuga bata au kuishi karibu na wafuga bata nazani wanafaham ninachoandika.

Ila kama tulivyo binadam kuna bata wengine ni wazembe wazembe ukisogea linatoka nduki.
 
Back
Top Bottom