Huwezi amini Wazungu ndio wanalisha Hoteli za Kitalii Tanzania, Hii aibu kuu

Sio wazungu, ni capital fala wewe, uache ubaguzi, Tanzania's:

1. Dont have capitals.
2. Wamiliki wa hizo Hotel wengi wazungu wanapeana biashara.

Tatizo la Tanzania ni sera mbaya za serikali, na uongozi wa hovyo wa CCM.
Wamiliki hawana shida wanacho angalia ni Quality na Quantity, ukiwa na Products nzuri wa anachukua sana
 
Swala sio TBS swala ni hatuko Serious, Hizo nyota Tano zinalishwa sana, tusha uza sana mfano Starwberry Mount Meru Hoteli ni yota Tano ile, ishu sio TBS ishu ni kwamba hatuko Serious basi,
 
Hayo ni maneno ya Balozi wa Tanzania Nchini China Bwana Mbelwa Kairuki

Kuna wahindi walikuwa wakinunua Korosho Tanzania waliacha sababu ya Korosho Kontena 2 zilikutwa na Mawe
Korosho kontena 2 mawe duh
 
Kusema kweli waafrika sisi kwanza wengi roho mbaya na akili kidogo...
Wazungu hao wanapenda best solution available bila kujali ni nani mfano mwaafrika yupo tayari kumuharibia mwenzake badala ya kujifunza na wazungu wanasema ukweli ila african uongo au asikuambie chochote hata kama anajua utafeli wapi...hao wazungu wanaumoja wao mwingine analima karoti, mwingine hoho n.k. na wanapouza na kuandaa official documents za kutoa full vegetables supply inakuwa na nguvu na waonekana wako well organized tofauti na mwaafrica walio wabinafsi..
Government import ipo ila ubinafsi chuki na roho mbaya baina ya wakulima..
 
Uchumi wa kibepari hauna uraia. Ukiwa na wazo na mtaji unaweza kwenda popote duniani na ukatekeleza.
Tukiendelea kuwaza kijamaa hatutatoboa.
 
Watu watabisha ila hilo hata mm nimelishuhudia kwanza ubora we imagine upewe tenda ya maziwa linatia maji na ngano, mtu anatumia dawa ovyo (niliwahi kula mboga moja ya majani nilitapika hatari)

Nahisi kinachofanya tusiaminike ni tabia ya watanzania kutojali basi
 
picha nyingi kwangu hazifunguki natumia jf app nini shida wakuu?
 
Na ushirikina juu yupo radhi akuzibie hata njia ya kuingia kwako
 
Yaani huwa inaumiza sana, mie mwenyewe kwenye maziwa yalinikuta nikaachana naye.
 
Exposure gani wakati tunalima ndani ya nchi na kuuzia ndani ya nchi? İna maana kulima products za kuuza hasa kwenye hoteli tunahitaji Exposure? Mtaji sh ngapi?
Baadhi ya majibu unayopata yanaonyesha jinsi watanzania tulivyo na mtindio wa akili. Mtanzania huwa anasoma au kusikiliza ili afanye ubishi na siyo aelimike au kutafakari kabla hajajibu. Asanye sana kwa observation yako. Halafu nchi imejaa vijana wasio na ajira maelfu. Hili ni kosa la serikali japo hata wananchi wana share yao. Kwanza kwa nini mgeni aje Tanzania kulima wakati tuna ma-graduate wa kilimo wengi?
 
Exposure gani wakati tunalima ndani ya nchi na kuuzia ndani ya nchi? İna maana kulima products za kuuza hasa kwenye hoteli tunahitaji Exposure? Mtaji sh ngapi?
Kwa hiyo neno exposure umelitafsiri kuwa ni nje ya nchi? Hata ukiwa matombo ukishindwa kuonekasha biashara yako Moro mjini utakuwa umekosa exposure
 
Hebu
KHapana tuna ulizana watanzania make hiu ni kazi tulipaswa kufanya sisi, sio swala la wivu, mimi nafanya nai biashara fulani ila ukweli huwa nasikitika si kwamba nawaonea wivu, ila huwa najiuliza.

TUnaweza ubinafsi mwingi
 
Kwa hiyo neno exposure umelitafsiri kuwa ni nje ya nchi? Hata ukiwa matombo ukishindwa kuonekasha biashara yako Moro mjini utakuwa umekosa exposure
Maada ni kubwa kwako broo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…