Huwezi Kukwepa Historia Hii na Ukabakia na Historia ya TANU

Kuna muda nafikiria kukubaliana na hoja zako ila kuna muda naona kama hoja zako hazina mashiko.

Nikikubaliana na hoja zako manake natakiwa kuwasaliti wapigania uhuru mbalimbali Nchini kote ambao walitoa uhai wao kwaajili ya Taifa letu.

Kupatikana kwa uhuru ulikuwa ni mchakato wa muda mrefu sana na mapambano ya muda mrefu sana, kusema kwamba wazee wa kariakoo ndio waliopigania uhuru hapo napata shaka na uelewa wako kwenye hoja hii.

Hatuwezi kufifisha au kudogosha mapambano ambayo wazee wetu walipambana dhidi ya wakoloni, Tukumbuke kuwa hata Mirambo, Isike, Mkwawa, Mangi Meri, Kinjekitile Ngwale, Songea Mbano, Abushiri bin Makunganya,Machemba na wengineo walichokuwa wanapambana ni kutaka uhuru wa jamii zao na Taifa kwa ujumla.

Yes wazee wa kariakoo wana mchango wao kwenye kupambania uhuru, Bibi titi, mzee Kleist, Aziz Ally, Mwapachu na wengineo.

Hata Abraham Lincoln hakupambana peke yake kwenye kuiunganisha marekani, alipambana akiwa na watu wengi ila credit kubwa sana zinaenda kwake likewise kwa Mwalimu Nyerere, tunatambua mchango wa watanganyika mbalimbali na wasio watanganyika walipambana kwenye mapambano ya kudai uhuru wa Nchi yetu

Kwa mzee wangu Mohamed Said nadhani maandiko na tafiti zako zingejikita kutupa baadhi ya watu waliosahaulika as wapigania uhuru wetu na uwa-address kama wapigania uhuru wa tanzania bila kuweka imani zao za kidini.

Hao wote waliopigania uhuru wa Nchi yetu hawakufanya hivyo kwaajili ya dini bali walifanya ili kuondoa udhalimu wa kikoloni..

Kumpachika mtu mazuri yake au mabaya yake kwa kuangalia dini yake hapo ndipo unapokosea mzee wangu.

Hao wazee wako walipambana kwaajili ya Tanganyika na sio kwaajili ya imani zao.
 
Mzee hizo mada zako hazisaidii Taifa kwasasa. Lete mada amabazo zitwasaidia Gen Z kuondokana na tatizo la ajira, changamoto za mfumuko wa bei, kuimarika kwa mifumo ya utoaji haki na ustawi wa haki za Binadamu, matumizi mabaya ya madaraka na wizi wa fedha za umma.
Hizi ndiyo mada za kuliponya Taifa na kujikwamua dhidi ya umasikini. Achana na hizo ngonjera zako ambazo ni outdated na hazina tija kwasasa
 
Sykes!๐Ÿคฃ๐Ÿคฃ

Yaani ukilala, ukiamka, "Sykes"๐Ÿคฃ๐Ÿคฃ

Imetosha!๐Ÿ˜‚
 
Sykes!๐Ÿคฃ๐Ÿคฃ

Yaani ukilala, ukiamka, "Sykes"๐Ÿคฃ๐Ÿคฃ

Imetosha!๐Ÿ˜‚

๐Ÿ˜๐Ÿ˜๐Ÿ˜

Umeona eeh, kumbe unamjua๐Ÿ˜


Huyu mzee nishamwambiaga kuwa hakuna chochote alicho nacho cha maana zaidi ya itikadi ya dini yake iliyovaa utashi na logic yake sasa anakaa kuhimiza udini na uongo dhidi ya utanganyika ili tu afurashishe nafsi yake iliotekwa na dini yake ambaye babu yake alilazimishwa tena kwa mboko
 
๐Ÿ˜๐Ÿ˜๐Ÿ˜๐Ÿ˜

The Worst
M O N S T E R


Vijana wamechoka porojo za wavaa mashuka๐Ÿ˜๐Ÿ˜
Manipulating, distorting and selectively presenting facts to change how people perceive reality can never work if people are intelligent and do their own researches.
Spinning and twisting the truth is same as scamming.
 
Manipulating, distorting and selectively presenting facts to change how people perceive reality can never work if people are intelligent and do their own researches.
Spinning and twisting the truth is same as scamming.
Hakika.
 
Vishnu,
Matukio ndiyo hivyo yaliyotokea.

Uislamu na Waislamu ilikuwa sehemu ya mapambano dhidi ya ukoloni.
 
Digaller,
Ukiwakwepa Waislamu historia itakuwa siyo.

Kwa Kufanya hivyo ndiyo leo tuko hapa tunasoma kitabu cha Abdul Sykes.
 
Eli...
Kama ni historia ya Waafrika wa Tanganyika huwezi kuacha kuwasoma.
1. 1924 Kleist anakutana na Dr. Kweggyr Aggrey
2. 1929 Anaunda African Association
3. Anaunda Al Jamiatul Islammiya fi Tanganyika
4. 1929 - 1933 Anajenga ofisi ya African Association
4. Mjumbe Maulid Committee, Tanganyika Chamber of Commerce
5. Anajenga Al Jamiatul Islammiya fi Tanganyika Muslim School
6. Anakufa 1949 na kuacha mswada wa kitabu cha maisha yake na mengi aliyoandika nimeyaweka hapa.
7. Abdul na Ally Sykes
Wameendeleza kazi ya baba yao kama viongozi katika TAA.
8 Abdul Secretary 1950 na anakutana na Kenyatta, Peter Mbili Koinange, Kungu Karumba, Paul Ngei, Bildad Kaggia.

Abdul na Ally wanampokea Julius Nyerere Ally anaandikiana na Kenneth Kaunda 1953.

Historia hii ya Sykes huipendi.
 
Mini ...
JF kuna masharti katika kuandika uzi?
 
Mini ...
JF kuna masharti katika kuandika uzi?
Hapana. Ila kuna kanuni inahimiza matumizi sahihi ya kalamu ya mwandishi katika kuleta mabadiliko chanya kwenye jamii. Hii ni pamoja na kuakisi mahitaji ya jamii kwa wakati husika.
Ni matarajio yetu kuona watu wenye uzoefu kiumri na maarifa kuja na maandiko yatakayosaidia katika kuikomboa jamii kwa matatizo yanayoikabili. Ukitupa rejea za Great Depression, mapinduzi ya viwanda huko ulaya, tawala za kinazi, mikakati ya kufufua uchumi iliyotumika kuzinusuru nchi za ulaya baada ya vita kuu za Dunia na namna tunavyoweza kujifunza kujenga uchumi wetu na mambo kadhaa kama hayo.
Hizo mada za kupata uhuru ni irrelevant kwakuwa tayari uhuru tunao ila tuna changamoto kadhaa katika Taifa ambazo zinatakiwa kuwa addressed.
 
Harakati hizi za kudai uhuru zimeanza Dar es Salaam Kariakoo Gerezani... na walioanzisha hizi harakati ni wazee wangu."
Mikoa mingine huku Tanganyika hawakuwahi kuwa na hizo harakati?....

Hili liweke sawa...
 
Dini zenyewe zote tumeletewa na firauni!๐Ÿšฎ
 
Vishnu,
Matukio ndiyo hivyo yaliyotokea.

Uislamu na Waislamu ilikuwa sehemu ya mapambano dhidi ya ukoloni.
Uislam, ukristo wote ni ukoloni.

Unasemaje ulipambana na kuupinga ukoloni wakati unakumbatia na kutukuza the results "dini" of colonialism?๐Ÿšฎ
 
Mimi...
Naamini sina ulazima wa kukubaliana na fikra zako.

JF ni jukwaa pans huna lazima ya kuingia kunisoma.

Kitabu cha Abdul Sykes kimerejesha historia ya nchi iliyokuwa imepotea kabisa.

Si hilo peke yake imebadili hata historia ya Julius Nyerere.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn moreโ€ฆ