Huwezi kumiliki/ kumilikishwa/ kuendesha LC 300 kama hutumii nguvu za giza

Sijui kwanini kuna baadhi ya watu wanawaza ujinga ujinga tu, kila kitu unaweza kumiliki bila maagano wala ndumba

Ni uamuzi wako, bidii na kujituma kwako nakumtanguliza Mungu mbele

Vingine vyote ni fikra zako tu
 
It sad unawaza uganga kupata mafanikio to this day, ambu rudi tena kitaa
Amenikumbusha familia moja hivi miaka ya nyuma kijana wao alipambana akanunua gari mbili za maana ndani ya mwaka mmoja na akajenga nyumba. Mwaka uliofuata dada katika familia hiyo akaugua, ile familia ikamuweka kikao yule kijana na kumwambia dada yako akifa utamla nyama mpaka ummalize.
 
Halaf ikawaje
 
Halaf ikawaje
Dada hakufa, kijana alimpambania dada yake licha ya ndugu na wazazi wake kumzuia hata kutumia pesa zake kumtibu (ziliitwa pesa za kifreemason). Wao waliamini anataka kumtoa kafara dada yake maana ndio dada na kaka waliokuwa wameshibana zaidi katika familia.

Katika familia za kimaskini, ukifanikiwa kuishika pesa nyingi, omba sana asife mtu kwenye familia yenu.
 
HUo ndio uafrica sasa,
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…