Huwezi kumiliki/ kumilikishwa/ kuendesha LC 300 kama hutumii nguvu za giza

Huwezi kumiliki/ kumilikishwa/ kuendesha LC 300 kama hutumii nguvu za giza

LC 300 and alike is not for everyone.

Sugua sana goti msikituni na makanisani, omba sana Mungu utaishia kwenye prado mchaga.

Huku kwa ma LC 300 ni dunia nyingine, dunia ya maagano, lazima uwe na nguvu za giza sio kulinunua tu hata kuliendesha, hakuna mjinga atakubabidhi milioni 400 uzurure nayo mitaani kwenye kila aina ya risk.

Hakuna washirikina kama madereva wa serikali na mabasi ya mikoani plus malori, hizo kazi huzipata kwa kuroga na kuhonga sana, mjinga nani ajukabidhi na milioni upige nayo misele.

Tanzania ukichukua fomu tu ugombee ubunge watakuja wazee wakulazishe kukupa hirizi au wakufanyie kisomo.

Ikulu ya Magogoni kila siku ni ubani udi na madawa yanafukizwa tu.

Ukija kwa wamiliki the same, Mungu wetu kuna limit ya mafanikio ametuwekea sisi waafrica, kuna level tukifika huwa tunamkufuru, ndio maana misikitini na makanisani wale waumini wa kweli wanamaisha ya chini au ya kawaida sana, wale matajiri ukiwafuatilia ndio wamiliki wa majini, washirikina wakubwa.

Waafrica ni wanafiki sana, bado hatujaacha dini zetu za asili, kuanzia ijumaa mpaka jumapili tutaenda misikitini na nakanisani, tukitoka hapo tunapishana kwa waganga.

Asilimia kubwa tuko hivyo.

Tuendelee kuendesha crown tu ili tufike mbinguni.

Mimi binafsi sijawahi kwenda kwa mganga ila nimefanya kazi na watu ni washirikina hatari na nusu,Na yanapanda vyeo tu wanachodekiver hukioni.

Africa tukifika maendeleo kama ya ulaya makanisa ya kiroho ya akina mwamposa an a like yatafutika,tutabaki na yale madhehebu yetu makuu,Kuna watu wanajifanya kuombewa wakishafanikiwa huwaoni tena kanisani,
Pata picha unaamka asubuhi maji bombani hayakatiki,umeme haukatiki,ada ya watoto haisumbui,wakimaliza masomo wanaoata ajira,ukiumwa una uwezo wa kujitibia Agha khan,unadrive gari kalina una nyumba yako ya kuishi,??Mwanposa atabaki na wale wateule wachache wanaotaka kwenda mbinguni,na sio wapenda miujiza
Sijui kwanini kuna baadhi ya watu wanawaza ujinga ujinga tu, kila kitu unaweza kumiliki bila maagano wala ndumba

Ni uamuzi wako, bidii na kujituma kwako nakumtanguliza Mungu mbele

Vingine vyote ni fikra zako tu
 
It sad unawaza uganga kupata mafanikio to this day, ambu rudi tena kitaa
Amenikumbusha familia moja hivi miaka ya nyuma kijana wao alipambana akanunua gari mbili za maana ndani ya mwaka mmoja na akajenga nyumba. Mwaka uliofuata dada katika familia hiyo akaugua, ile familia ikamuweka kikao yule kijana na kumwambia dada yako akifa utamla nyama mpaka ummalize.
 
Halaf ikawaje
 
Halaf ikawaje
Dada hakufa, kijana alimpambania dada yake licha ya ndugu na wazazi wake kumzuia hata kutumia pesa zake kumtibu (ziliitwa pesa za kifreemason). Wao waliamini anataka kumtoa kafara dada yake maana ndio dada na kaka waliokuwa wameshibana zaidi katika familia.

Katika familia za kimaskini, ukifanikiwa kuishika pesa nyingi, omba sana asife mtu kwenye familia yenu.
 
HUo ndio uafrica sasa,
 
Back
Top Bottom