Huwezi kumiliki/ kumilikishwa/ kuendesha LC 300 kama hutumii nguvu za giza

Huwezi kumiliki/ kumilikishwa/ kuendesha LC 300 kama hutumii nguvu za giza

Kuchimba madini bila ushirikina hata 2M haupati.
Hivyo mtoa mada yuko sahihi kwa kiwango kikubwa.

Kuna kundi dogo mno miongoni mwa waliofanikiwa kumiliki zaidi ya Tsh 400M pengine chini ya 10% ambalo halina hisa kwa waganga.
Aende geita na kahama aone kwa macho yake,akitoka hapo aende kwa wavuvi ajionee,wanafanya ushirikina waziwazi
 
Kuwa ndogo au kubwa inategemea na ubongo wako unaona na kuwaza nini.....unajua dhana ya mafanikio hailingani baina ya mtu na mtu....kuna mtu kujenga nyumba , kusomesha na kumiliki chombo chochote cha usafiri hapo amemaliza na humwambii kitu....lakini ni tofauti kwa mwingine ambaye hayo kwake ni mahitaji ya msingi sio mafanikio....hatufanani na hatutafanana....na kutofautiana huko ndio raha na tamu ya maisha.
Vyovyote vile milioni 500 ni hela nyingi kwa Maisha ya Tanzania,
 
hapo sawa.
maana mimi nishaapa siwezi aga dunia bila kuliburuza hilo kwakua nishakua na watu ambao nawaona kabisa hustles zao mpaka wanazinunua hizo na sio wanga wala majambazi
Pambana mkuu nina maana kuandika hivi,mwakani lazima niliburuze tu bila kwenda jwa waganga japo jasho litanitoka kweli kweli
 
Hivi mtu kama Mimi unaweza nishawaishi vipi nikaamini mafanikio yanatoka Kwa Mungu,wakati napigika nilienda maeneo miaka ya nyuma huyu Mzee amefaliki aliniagiza nikachukue nywele za kichaa nikaenda kaliakoo nikakamata kichaa nakamnyoa usiku kesho nikapeleka kuanzia hapo mambo yakasonga miaka kadhaa nikaona kuyumba nikaenda Nyarugusu huko ndani ndani nikapata vya kupata nikasonga na kote huko nakutana na watu wa Mungu tena wale wakubwa halafu uje niambie eti omba Mungu Tu Acha tu nipambane na uchawi ilimladi naishi vyema,tusichokijua wengi wetu ukiona mtu anakwambia tegemea Mungu jiulize zaidi yeye anamtegemea, cc Nabii wa kitunda najua kabla hajawa hivyo tulikutana maeneo miaka ya nyuma na tukapelekwa makabulini tena alikimbia mara ya Kwanza baada ya kuona kabuli limegawanyika Acha niishie hapa kikubwa Imani sababu wengine kuandika hatujui
Kwa niaba ya wanajf wapenda story, tunaomba utuandalie uzi special wa story yako mkuu
 
Huna unalolijua Mimi nilitumwa nywele za kichaa zikawekwa kwenye chupa na dawa ya maji nikazika kwenye genge langu miaka ya 2002 maeneo ya Moshi bar nikawa nakimbiza Sana baada ya biashala kuanza kuyumba niliporudi nikaambiwa Yule kichaa atakuwa amekufa ndio sababu biashala inataka kuanguka hivyo nikabadilishiwa ndio chanzo cha kupelekwa makabulini kuingia maagano Acha nisizungumze Sana sababu wengi wenu Humu ni wale ambao Maisha mmeyakuta hamjawahi kutafuta kwenye ushindani mpk utoboe ujue umehangaika ebu tazama hapo nilikuwa na miaka 15 nimeanza Maisha na enzi zile unatoka Moshi bar gari unakuja kupandia mazizini au Mombasa ukipita lerini pale unakuta maiti za watu miaka hiyo kufanikiwa kunahitaji kujitoa
Inawezekana hakuna nalolijua kweli Mkuu ila hakuna ulichopewa hapo zaidi ya kudanganywa kwa sababu ya Ujinga wako ukiuliza mafanikio yenyewe chenga tu...
Maisha ni kupambana hao wajinga hakuna kitu wanawapa zaidi ya masharti ya kijinga jinga kama sasa unasimulia kabisa eti kichaa kufa hela zikapungua...
 
Back
Top Bottom