Huwezi lazimisha Mwanamke akuheshimu, Mwanamke anamheshimu mwanaume anayempenda


Soma kwenye Torati utaona vile Yehova alivyokuwa analazimisha Watu waheshimu maagizo yake lakini iliishia wapi?

Tena huyo anayezungumzia mabaya yako mbele yako ni mzuri kuliko yule mkimya ambaye mabaya yako yapo kwa mashoga zake au huko mtañdaoni kwa utambulisho wa anonymous
 

Mwanamke anapenda kama ilivyo mwanaume. Tena anapenda zaidi ya mwanaume ndio maana huwa mtiifu.
Huwezi kumtii mtu usiyempenda.

Pesa haibadili moyo wa mtu akiwepo hiyo Mwanamke.
Pesa inampa uhuru mtu wa kuonyesha hulka yake halisi.

Mwanamke kama alikuwa hakupendi akiwa na pesa ndio wakati wa kuonyesha kile ambacho ulikuwa hukioni.

Pia elewa, hata ukizeeka au ukiishiwa au kufilisika ndio wakati ambao Mwanamke atakuwa huru kuonyesha yaliyomoyoni mwake. Kama alikuwa hakupendi ndio utajua lakini kuna kulipa kisasi.

Hata wanaume sisi tulipata hizo pesa mbona wengi tunaanzisha mahusiano mengine na kuwa na MICHEPUKO au kuoa kabisa wanawake wengine?
Sio kwamba pesa ndio zimetubadilisha, ila pesa zimetupa uhuru wa kujionyesha dhahiri sisi ni watu wa aina gani.

Mwanamke anapenda. Sema wengi hawapati bahari ya kuolewa na wanaume wanaowapenda ndio maana unasema ulichokisema
 
Mapenzi ya dhati yanaendana na kutimiza majukumu ipasavyo, mwanamke asipokuwa na stress upendo wake kwako utaongezeka, na hata kama ikitokea mara moja moja umekosa hawezi kuwa na shida.

Tatizo linakuja pale utaposhindwa kutimiza majukumu ipasavyo, akachoka kukuvumilia hata kama alikuwa anakuoenda kwa dhati, ukamlazimu mwanamke aanze kujichanganya kwa ajili ya kuihudumia familia, akishaanza kukutana na watu tofauti huku akiwa na akili ya kutafuta, penda usipende upendo wake kwako na heshima vitaanza kupungua.

Umeandika uzi wako kama vile upendo na heshima vya mwanamke kwa mwanaume ampendae ni constant, havipungui, no way, hivyo vyote lazima ujue namna ya kuvitunza kwa ajili ya manufaa yako.
 

Upo sahihi Mkuu.

Upendo na furaha hulindwa. Majukumu na wajibu ni sehemu ya kuvilinda.
Ningeeléza kila kitu uzi ungekuwa mrefu alafu waja wangekuja
 
 


Hili neno "nakuvumilia -namvumilia " ni neno la kisiasa Sana.

Hakuna binadamu anayemvumilia mwenzake ikiwa unamuhudumia mwanamke au yeye anakuhudumia hakuna anayemvumilia mwenzake hapo.

Ni tafsiri mbaya Sana kusema nakuvumilia .
 
Hujielewi
 
YAANI TAIKONI HUJAWAHI KUKOSEA SIJAWAHI KUKUPINGA UNAPIGAGA KWENYE MSHONO AISEE 🔥🔥
 
Mapenzi ya dhati yanaendana na kutimiza majukumu ipasavyo, mwanamket asipokuwa na stress upendo wake kwako utaongezeka, na hata kama ikitokea mara moja moja umekosa hawezi kuwa na shida.

Stress inategemea chanzo chake ni nini? Hata sisi wanaume tupo vivyohivyo
Mwanamke lazima aweze kuihudumia familia yake. Iwe yupo ndoani au hayupo. Mwanamke ni mtu kama alivyo mwanaume.
Na Mwanamke mtafutaji ndiye mwenye upendo wa dhati tofauti na yule ambaye anahudumiwa tuu nyumbani ambaye ndiye unayemuelezea hapo.

Umeandika uzi wako kama vile upendo na heshima vya mwanamke kwa mwanaume ampendae ni constant, havipungui, no way, hivyo vyote lazima ujue namna ya kuvitunza kwa ajili ya manufaa yako.
 
Bila shaka wewe ni mwanafalsafa na unaongozwa na hekima ,haki na upendo .

Iko hivyo.
Kuna vitu havilazimishwi hasa vitu vya asili ambavyo Mungu ameviumba. Vitu artificial vinaweza vikalazimishwa.

Kwa mfano mtu anaweza kulazimisha kujenga bondeni kwa kujaza kifusi lakini kiasili eneo lile ni bonde. Hivyo ipo siku isiyo na jina lazima mafuriko au madhara yatokee
 
Hili neno "nakuvumilia -namvumilia " ni neno la kisiasa Sana.

Hakuna binadamu anayemvumilia mwenzake ikiwa unamuhudumia mwanamke au yeye anakuhudumia hakuna anayemvumilia mwenzake hapo.

Ni tafsiri mbaya Sana kusema nakuvumilia .
Inategemea na muktadha, kweli kuvumiliana endlessly kunaweza kuwa kugumu, lakini kama pillars za upendo zipo kati yenu, basi upendo wenu hauwezi kuyumba.

Ndio maana huwa naamini sio kila mwanaume anayechupuka hampendi mke wake, anayechepuka huku akitimiza mahitaji yote ya familia yake kwangu anajielewa zaidi ya yule anayechupa huku akiwa haijali familia yake.
 
Wanawake ni kuwaacha kama walivyo, ila ukisema Unataka kudili na kilichomo ndani ya moyo wa mwanamke ni uwongozi. Ukiangalia hata kiimani ndiye kiumbe aliyeumbwa baada ya mwanaume lakini alikuja kuwa na nguvu hadi ya ushawishi ana na nyoka naku sababisha usaliti. Wanaume msijikite zaidi kuwafurahisha wanawake, hawatabiriki. We tenda mema ondoka zako vinginevyo natafuta magonjwa ya moyo na kesi za mauwaji.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…