Huwezi nishawishi Nyerere alikuwa Rais bora

Nyerere ni raisi bora. Mwinyi akawa bora zaidi katika kuifungua nchi kiuchumi amabopo ilikua inaelekea kaburini. Mkapa akawa bora kwenye kuanzisha taasisi za kusimamia mambo muhimu ya nchi kama kodi n.k. Ila ni katika kipindi cha mkapa na kuendelea pesa za umma zikaanza kuibwa waziwazi kufadhili kampeni za chama. Baadae wakazaliwa mafisadi wanaodumu hadi kesho.
 
Nyerere ni the best, binafsi yangu sijaona taifa Africa ningependa niwe raia tofauti na Tanzania na hii imechangiwa na misingi aliyoiacha. Sema pia ni ujinga sana kuamini kwamba kila maamuzi yake yalikuwa sahihi.
 
Anapaswa kulaumiwa kwa sababu ameanzisha kujenga Msingi mbovu wa Uongozi katika Taifa hili.
Kumbuka: Nyumba imara huanza na ujenzi wa Msingi imara na ulio Bora.
 
Inasemekana aliyepewa tenda ya ujenzi wa uwanja wa Taifa kwa upande wa China aliporudi kwao na kugundulika kaiba huku Tanzania serikali yao ilimnyonga. Lakini mtanzania aliyeshirikiana nae wizi huo katika michakato ya ujenzi mpaka leo yupo hai.

Hiyo ni tofauti ya China na Tanzania, nidhamu zetu hazifanani hata kidogo.
 
Kimsingi alikuwa wa hovyoo kabisa yaani watu alitujegea hofu, alituharibia mfumo mzuri wa Elimu Kwa kuondoka mtaala wa Cambridge,aliamini katika umaskini,alipora mali za watu,alitutoa relini kabisa watanzania wanaomaliza vyuo vikuu vyetu ni kiwango cha kata, hawana fulsa ya kuajiriwa popote Duniani,leo hii Kila mwanafunzi aliyeko chuo kikuu wala hazingatii kusoma anawaza apate cheti Kwa vyovyote vile,avae nguo za kijani awe chawa Ili apate teuzi basi inasikitisha sana
 
Mkuu waafrica na watanzania mna low IQ
kama ndo ivo mbona ndege mmeshindwa kuendesha
Bandari mmeshindwa mmempa muarabu
Umeme bado hoe hae
Nipo mwanza kutoka ninapo ishi had ziwani km2 tu lakini mtaani hamna maji.

Singida dodoma kuna ukame lakini kila kona mmezungukwa na ukame ziwa tanganyika nyasa na victoria


Itoshe kusema Hata uachiwe Tirion ngap kama akili huna huna tu vitapukuchika kama vumbi.
Nyerere alikua geniuous kwene nchi ya mapopoma
 
Absolutely true.
 
Kuamini mtaala wa mzungu ni bora na kushindwa kudevelop mitaala yenu ni uwezo duni wa kufikiri.
We ulichobakiza ni kuolewa tu maana hata vitu inavobidi ujitengenezee unamuwaza mzungu
 
Kwa Afrika viongozi bora wote hawakudumu.
 
Kuamini mtaala wa mzungu ni bora na kushindwa kudevelop mitaala yenu ni uwezo duni wa kufikiri.
We ulichobakiza ni kuolewa tu maana hata vitu inavobidi ujitengenezee unamuwaza mzungu
Wakati tunapata uhuru tulikuwa na wataalamu wa kutosha kudevelop mitaala?wewe vipi? Kenya na Uganda iliwasaidia ndiyo maana wapo hapo.Mzungu hauwezi kumkwepa tunanini tulichonacho siyo Cha mzungu?hapo sisi tulipo Kwa Africa mashariki hatuuziki popote pale tumebaki kusifia sifia tu choka mbaya sana na bado tutatoka wenyewe bara barani Muda ukifika
 
Mbona hata ss hatuna mpango wa kukushawishi baki na mawazo yako na sie tubaki na yakwetu
 
Kupenda au kuuchukia uongozi wa mtu ni relative.
 
Unapingaje ubora wa Nyerere bila kuainisha mapungufu yake yanayokufanya usimuone bora Mzee?
 
Yaani nawe pia mmoja wao aisee
Unaishi mwanza karibu na ziwa kama una akili basi ungekuwa na meli na kiwanda cha samaki
Bora mimi niliondoka miaka ya 70 baada ya kuona hapaeleweki
Usikariri kuona nimechangia ukadhani niko Kasulu
Ulikuwepo miaka ya 70 wakati alileta uhujumu na kudhulumu watu mpaka radio?
 
Hakuna na bado Nyerere alirudisha hela zao kwa misimamo yake. Huyu mpiga mwingi anaweza?
Kasgindwa nyetrere atawea yeye, angekuwa nyerere karudisha pesa zao ingeshikwa ndege afrika kusini? Au umesahau kwanini ilishikwa?
 
Hakuna umoja wala nini

NI UOGA TU tumejazwa na huyo mwalimu
Vizazi na vizazi leo bado vinarithi uwoga na khofu
Na hii si afya kwa maendeleo
Vijana wenye hofu ni wale wa zamani, sio hawa watoto wa 2000.

Vijana wa sasa wanatembea na dunia nzima viganjani mwao kwa kutumia simu za kupangusa hawana sababu yoyote ya kuhofia chochote.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…