Huyu dada kanitapeli Tsh. 1,500 siku yangu imeharibika kabisa, sina hata raha

Huyu dada kanitapeli Tsh. 1,500 siku yangu imeharibika kabisa, sina hata raha

Huyu dada nilionana naye Hotel Flani Arusha tukawa marafiki. Ana issues nyingi sana sana za kusafiri kwenda Dubai n.k ni lidada hasa la ukweli aisee, toka kanda ya Ziwa huko. tukawa karibu na kadhalika.

Leo asubuhi kaniambia ameishiwa vocha nimtumie some amount nikamwambia nipo ofisini sina kitu kwenye simu. Akaomba hata kiasi chochote nikaangalia nikajikuta nina tsh 1,500 nikamrushia ili ajiunge maana kuna kitu alisema anataka aunge data then anitumie.

Toka saa tatu nimemtumia mpaka sasa hapatikani kwa simu nadhani ametupa na line kabisa maana nimewapigia kwenye mtandao jamaa zangu waniangalizie atakuwa wapi wanasema haiwezekani ku mtrace maana line imeharibiwa kabisa.

Mara ya mwisho alikuwa Zanzibar amabako nilimwacha jana nikaja Dar. Najiuliza huyu dada amewaza nini mpaka kunitapeli. Nimeumia miaka yote sijawahi tapeliwa why now? Je, nimeanza kuwa weak? Au ni nini hiki kitu, siku nzima ya leo sina amani kabisa, nikawaza je ningemtumia tsh elfu 5? maana hapo nimemtumia tsh elfu moja na mia tano. Wallah atakuja ilipa tu, jasho la mtu haliendi bure.
Ulianza kwa kusema huna kitu,halafu una1500.Unadharau hela.Usilalamike hapa hiyo umempa.
 
... Utoto Raha Sana! 1500/ unaanzishia Uzi? Zimeluuma Sana?
Kweli aiseee ...maana hata kuandika kwako ni shida. Usiache kwenda shule sasa angalau umalize darasa ujifunze na kuandika.
 
Nenda kamroge asee... Hio 1500 ungeongeza 150 unapata nusu lita ya petroli bro... Misele ya maana kabisa
 
Tafuta aspirini au klorokwini gongea na k vant bwamdogo, hawezi kuzulumu hela nyingi sana hiyo.
 
Back
Top Bottom