Huyu huenda kweli akawa ni mwana wa Mungu aliye hai angalia Mayele, Dkt Biteko, Chalamila, Dkt Mwigulu, Dkt Samia, Dkt Tulia hata Paul Makonda

Investigation Unit

JF-Expert Member
Joined
Nov 26, 2023
Posts
216
Reaction score
301



Habari Tanzania,

Kwa muda sasa kumekuweko mijadala mbalimbali kuhusu Ndugu yetu Apostle Bonface Mwamposa almaarufu kama Bulldozer.

Apostle Bonface Mwamposa anahudumu katika madhabahu ya Arise & Shine au kwakimombo " INUKA UANGAZE" ( Isaya 60:1 ) yaliyoko Kawe jijini Dar es Salaam Tanzania.

Apostle Bonface Mwamposa amekuwa na wafuasi wengi wanaoongezeka siku baada ya siku mwezi baada ya mwezi au mwaka kwa mwaka yaani ni mamilioni kwa mamilioni ya waamini toka nje na ndani ya bara la Africa,

Apostle Bonface Mwamposa, ibada zake zote hazina Misingi ya dini au dhehebu lolote ila " IMANI KWA YESU KRISTU NA MUNGU ALIYEMTUMA "


Apostle Bonface Mwamposa, anahudumia Watu wakristo kwa Watu Waisilamu au hata wale wote wasio na dini kabisa kama akina Yeriko Nyerere nao pia wakiamini wanapokea uponyaji wa mwili na roho pamoja na haja zao kutimilizwa na Mungu wa Boniface anayejibu kwa Moto,

Apostle Bonface Mwamposa, ndiye aliyemwambia Mhe Dkt Willium Ruto kwamba "Nenda Utashinda Uchaguzi" na mishowe Ruto akashinda Urais,

Bila Mungu ilikuwa ni ngumu sana mtu kama Mhe Willium Samoi Ruto kuwashinda Mhe Raila Omolo Odinga na Kenyatta Uhuru ila Mungu wa Boniface akafanya jambo pale Kenya na dunia ikashangaa kilichotokea,

Apostle Bonface Mwamposa, Ndiye aliyemwombea pia Mhe Dkt Tulia Ackson na akashinda na kuwa Spika wa mabunge yote Duniani ( IPU ) hata Leo,

Apostle Bonface Mwamposa, ndiye aliyemwombea kaka yetu Fiston Kalala Mayele na akawa mchezaji bora wa wakati wote Nje na ndani ya Tanzania nadhani sote tunakumbuka huyu kijana anayechezea timu Pyramids FC hivi Sasa,

Orodha ya waliosaidiwa na Mungu kupitia kwenye kinywa Cha Apostle Bonface Mwamposa ni wengi na hawahesabiki,

Wengine wanakwenda kwa Siri na hawataki mtu yeyote awaone maranyingi hawashuki kwenye magari yao but wanatendewa japo ni ujinga kujificha au kuficha Matendo Makuu ya Mungu wakati kwa waganga mnakwenda tena waziwazi.

Hoja yangu hapa ni , Je? Mwamposa kwa kuzingatia mafundisho yake na Upako alionao huenda ni kweli huyu bwana akawa ni mwana wa Mungu ila sisi imani zetu zimekamatwa na shetani na hivyo tunashindwa kutofautisha kati ya kazi za Shetani na kazi za Mungu?
====

Kama hujawahi kwenda au kumsikiliza Apostle Bonface Mwamposa jipe muda wa kumfuatilia kabla hujamsema vibaya kwani ni kujitafutia laana toka kwa Mungu ALIYEMTUMA MWAMPOSA.


Mfuatilie: Azam channel No 469
Startimes channel No 117

You tube: Mwamposa Live
You tube : Arise & shine Tanzania

Instagram: Arise & shine Tanzania
 
Mtalaaniwa bure subirini hukumu ya Mungu ipo pale pale.
 
Tatizo ni umeme
 
Kuna kichaa alipelekwa kwa Mwamposa, Aisee, wakati anaombewa akawazidi nguvu, akaleta fujo mbaya kabisa, vunja vunja maspika, watu wakakimbia akatoka nje, vunja vunja vibanda vya mama ntilie pale nje, ikabidi polisi waitwe, baada ya kumpiga virungu vya kutosha, wakampandisha kwenye karandinga na pingu, wakaondoka nae, manabii wa uongo, wanaotoa ushuhuda wamewapanga!
 
Hapana wewe ni muongo kama hujui Kaa kimya tena kuwa kimya kabisa yatakupata mabaya sana
 
Ndugu zangu wote walioenda kwa jamaa kupata uponyaji hawajasaidika.

Nimepoteza wengi kwa kudhani mwamposa angewaponya kwa maombezi
 
NAOMBA SIMBA SC WAFIKE MARA MOJA KAWE BILA KUCHELEWA,
Tutachukua kombe kupitia Mungu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…