Huyu huenda kweli akawa ni mwana wa Mungu aliye hai angalia Mayele, Dkt Biteko, Chalamila, Dkt Mwigulu, Dkt Samia, Dkt Tulia hata Paul Makonda

Ile pale ni Madhabahu yaani lango la malaika ndio maana watu wanasafiri wanakwenda pale,

Mwamposa ni kiongozi wa kusimamia na kuratibu kazi za lile lango,

Hivyo kwenda kuabudu au kukiunganisha pale ni muhimu sana
 
Muda wa Majibu yake bado haujafika Mungu lazima akutengeneze vizuri hasa maswala kama ya Utajiri na vyeo vikubwa lazima uwe-shaped,

Iko siku utamuona kwa tofauti sana,

Hata hivyo anapashwa kuweka imani kwa Mungu sio kwa Mwamposa
Sasa watu wanavutiwa na hizo shuhuda(matangazo) na katika hizo shuhuda hakuna anayeeleza kwamba ilimchukua muda mrefu kujibiwa maombi yake, wote wamefanikiwa kwa muda mfupi.

Unaposema waweke imani kwa Mungu na si kwa Mwamposa wakati Mwamposa anajitangaza zaidi ya huyo Mungu unakuwa unashangaza, watu Mungu wanamjua na wanajua kuwa anataka wamuombe yeye sasa unafikiri kwa nini wanaenda kwa Mwamposa?
 
Ile pale ni Madhabahu yaani lango la malaika ndio maana watu wanasafiri wanakwenda pale,

Mwamposa ni kiongozi wa kusimamia na kuratibu kazi za lile lango,

Hivyo kwenda kuabudu au kukiunganisha pale ni muhimu sana
Sasa mtu ambaye si mkristo haamini Mungu anayemuamini Mwamposa je atainua vp imani yake? Maana kilichomleta ni miujiza tu na si imani kwa Mungu wa Mwamposa.
 
Sasa mtu ambaye si mkristo haamini Mungu anayemuamini Mwamposa je atainua vp imani yake? Maana kilichomleta ni miujiza tu na si imani kwa Mungu wa Mwamposa.
Hata Yesu kilichomfanya wamwamini kama yeye ni mwana wa Mungu ni ishara na miujiza aliyoifanya ,

Kama Kanisa halina ishara Wala miujiza jua kabisa hiyo ni Club tu,

Mungu wetu ni Mungu wa udhihirisho,

Huwa hakai kimya tangu enzi za Elia, Elisha hata sasa,

Kanisa la kutoa sadaka na kuondoka hiyo ni Club tu au kikoba,
 
Mimi sio Mkristu ila Jumapili asubuhi Insha'allah nitafika hapo Kawe asubuhi
Mimi pia nataka wale wote wanaoniandama waangamizwe
Nitaenda jumapili nikijaaliwa na Mungu 🙏👍

Ngoja Tusubiri tuone wanaojifanya wao hawawezekani 🙏
 
Mleta mada,wewe si mwamposa kweli unanadi biashara yako! eti nenda katazame azam tv,sijui youtube. si ungejitambulisha tukakufahamu tu ndg yangu.BIASHARA MATANGAZO hili nalo ni tangazo la biashara ya mwamposa.
#kazi kweli kweli# job true true...!
 
Ninacho jua Mimi ni kwamba Boniface Mwamposa ndiye mungu halisi kwa hao wanategemea miujiza ya kumbewa na huyo mungu Mwamposa!
 
Mkuu Kuna wagonjwa huko hospital na vichaa huko sober house Kama huyo muigiza michezo jukwaani kweli anaponya mwambie akawaponye hao.
Baba mtumishi nilinunua mafuta nikamwaga kwenye waya za umeme sahivi mungu was mwamposa ananiponya mwenzangu umeme ukikatika kwangu unawaka aposto.
 
Mleta mada,wewe si mwamposa kweli unanadi biashara yako! eti nenda katazame azam tv,sijui youtube. si ungejitambulisha tukakufahamu tu ndg yangu.BIASHARA MATANGAZO hili nalo ni tangazo la biashara ya mwamposa.
#kazi kweli kweli# job true true...!
Hapana Mimi ni mfuasi tu wa Mwamposa natamani na wenzangu mfunguliwe kutoka kwenye vifungo vyenu mbalimbali
 
Húu sio utaratibu wa Mungu,

Watoeni muwapeleke wote watapona,

Imani ni kumtafuta Mungu,
Kutoka Hospitali mpka Kawe ni kitendo Cha imani lazima apone
 
Nitakuwepo kwenye mkesha tarehe 31 sikosi, Mungu nipatie nauli ya kufika Kawe Mimi ninayeamini nguvu zako
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…